Uchaguzi 2020 Salumu Mwalimu: Biashara zote za Serikali kubinafsishwa

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,072
28,267
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi. Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
 
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi.
Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
Ukiwa na sera nzuri mashirika yataendeshwa kwa ufanisi mkubwa sana! Na hapo kwenye sera ndipo serikali ya CCM imefeli vibaya
 
Hatuwezi kufanya majaribio kwa nchi nzima. Watanzania ni waelewa sana!
====
Kwamba Tanesco itabinafsishwa, TTCL, ATCL, TRL, nakadhalika....! Vyote watapewa " wakwepuaji" wa chama cha Mbowe,Chadema! Maajabu hayeshi!
Unaikumbuka PSRC chini ya Mkapa ilifanya nini? Je unawajua NET SOLUTION sijui unaijua Simu 2000. TRL Tanzania hakuna kitu kama hicho.
 
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi.
Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
Kwa utumbo huu bado kuna mtu anakaa na kupigia debe wapewe nchi
 
Wanasiasa huwa mara nyingi wanaongea vitu katika mtazamo wa kisiasa na sio katika uhalisia Kuna vitu wanavozungumza havina uhalisia kabisa
 
Sera zilikuwa mbovu, aidha Magufuli kataifisha kwa sera mbovu kabisa kabisa. Lipo shirika moja amelichukua kimabavu ila ni mwaka sasa kalitelekeza. Nyie hamuwezi kuelewa kwa undani ila sisi tuliopo huku juu tunajua ushenzi mwingi sana aliofanya Magufuli.
Wewe upo juu sisi tupo juu katikati na chini.
Hivi TTCL ilikuwa hoi kwa sababu gani na imerudi kuwa hai kwa sababu gani?
 
Mkapa alikuwa CCM au Chadema??? Sera za Mkapa ndo za Chadema kwani???

Mbona CCM mnakuwa vilaza hivyo???? Embu niambie ni biashara gani ya Serikali inayojiendesha kwa faida na ufanisi???!
Muulize ambaye nimemuuliza mimi anayesema CDM haiwezi kuwa na sera nzuri.
 
Back
Top Bottom