Salim Kikeke ajiunga rasmi na Crown FM & TV

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,772
54,058
Mtangazaji Nguli, Mwanahabari na Mwandishi wa habari mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Salim Kikeke amejiunga na Redio/TV ya Crown FM/TV inayomilikiwa na Alikiba.

Hii ni baada ya Alikiba kusasisha video inayoonyesha Salim Kikeke akikataa kupokea simu ya Wacha Fu FM inayotafsiriwa kuwa ni Wasafi FM, ya Kisingeli FM (EFM) na Icecream TV (Azam TV) kisha kupokea simu ya Alikiba (Crown FM/TV). Katika Video hiyo, Alikiba ameandika yafuatayo:

"My Brother @salim_kikeke hii ilikuwa ndoto na maono tuliyokuwa nayo muda mrefu. Wakati unafanya maamuzi ya kurudi Nyumbani Tanzania tulipata nafasi ya kuzungumza na nikakueleza kiu yangu yakutaka kufanya kazi na wewe Gwiji, Nguli na Mtaalam wa Tasnia hii ya Habari Afrika na Dunia.

Najua Simu zilikuwa nyingi sana lakini uliona CROWN ni sehemu sahihi sana kwako. Karibu kuwa sehemu ya Historia tunayoenda kuiandika pamoja.

Nimekuvisha Taji na CROWN Media tunaamini Hesabu zetu za Kimkakati zimekaa Sawa. Karibu sana Nyumbani @crownfmtz na @crowntvtz" ameandika Alikiba, Msanii wa muziki wa Tanzania na Mmiliki wa Redio/TV Crown.

FB_IMG_17143933406267793.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom