Salaam za Kisukuma: Eeng'washi, Eeminza, Ng'waguku, Ng'wanene... Msaada

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,256
Bagalu bichane, aliyoneyo, nandje kwa kubagisha pye!

Salaam kwa wote. Samahani wakuu, inaniwia vigumu kuandika kwa kutumia lugha moja kuwasilisha hoja na maswali yangu. Ningelipenda sana lakini inanishinda.

Kwa waelewa na wataalam wa lugha ya Kisukuma, naomba msaada kufafanuliwa matumizi fasaha ya vitambulishi na vipokeo vya ukoo na ukubwa kiumri katika salaam.

Kuna mameno kama: eeng'washi na eminza, yananitatiza. Nambelejagi babehi, naduma geteh oukwelelwa. Nakoubiza nabona majonginjongi douhu!! Anguh lekaga nafunye mifano ahaseleleh ahah:

-- bibi na babu mzaa mama unamsalimia kwa vipokeo vipi?
-- bibi na babu mzaa baba unamsalimia kwa vipokeo vipi?

--mjomba unamsalimia kwa vipokeo vipi?
--shangazi unamsalimia kwa vipokeo vipi?

--mama mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?
--baba mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Na salaam nyinginezo mbalimbali ambazo utaweza kuzielezea. Akhsante.

Steve Dii
 
-- bibi na babu mzaa mama unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Hao watakupiga ng'wanene halafu wewe uajibu, kutegemea na 'lwimbo' wao i.e. Inkwimba, Insega, Ing'washi, Iminza, n.k.

-- bibi na babu mzaa baba unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Hawa nao vivyo hivyo.

--mjomba unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Mjomba atakupiga 'ng'waguku' au 'ng'wamayu' halafu na wewe utampa 'lwimbo'

--shangazi unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Shangazi atakupiga 'ng'wabhabha' halafu wewe utampa 'lwimbo'

--mama mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Hao ni 'ng'wamayu'

--baba mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Hao watakupiga 'ng'wabhabha'.
 
wasukuma ni kabila kubwa na lina mataba mengi sana kuna (wagalu na wagika) ndaniyake kuna waminza,wasega, washola nyo,wakwemba,wadaki, wanega,waseya,wakamba,ng'washi,wakendegele, na NK. hizi ni tabaka za koo ndani ya wasukuma, eng'washi ni salamu ya
 
eng'washi ni salamu ya kitoto yani kama (HI) kwa wazungu, salamu mkato. inatumika sana mkoa wa Mwanza. hatahivyo wazee wengi ukimsalimia ukamwitikia eng'washi, bila kumuuliza lwembo(heshima yake) atakujibu mh'wamashi. yaani babuyako ni mavi(kinyesi)
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Kina babu na Bibi watakuambia Ng'wanene na wewe utaitikia Lwimbo Kama Eminza, En'gwashi, Emongo, Enkwemba au Eseya n.k

Wajoba,Shangazi,Kina baba na mama Hao ni wazazi.
Wao watakuambia Ng'wamayo au Ng'wabhaba;
Na wewe ni kuitikia Lwembo Kama hapo huu kwa mababu na Bibi!

Kaka zako Wa Tumbo Moja au Wa baba mkubwa au mama mkubwa Hao watakusalimia Ng'wagoko, nawe utaitikia Lwimbo Kama hapo awali!

Watoto Wa kike Wa Tumbo Moja na Wa baba mkubwa na Mdogo na mama mkubwa na Mdogo Hawa wote ni wadogo kwa watoto Wa kiume ata Kama wanakuzidi umri!
Hawa wote unawasalimu Ng'wagoko na Wao wataitikia Lwimbo Kama kawa!
Watoto Wa Mjomba na Shangazi!
Hapa kwa kawaida abana Ba nsheke na batale!
Yani Hapa watoto Wa Shangazi ndio wakibwa!
Nao watakusalimia baba au mayo ng'wagoko nawe utaitikia Lwimbo!.
Nawe ukishakua na watoto utafanya Kama baba zako au wajomba zako na ukiwa na wajukuu utafanya Kama babu au Bibi zako!
Welelwa ahene bahebu?
 
bhe bhe Ntuzu. ubhese abha NG'HWANZA, ung'wana ong'o sengi ate ntale alendo, uwang'wa mami huntale, hanumayaho utayombage geke welelwa, ulayombage geke odeba nulu omana
 
Na mtu yeyote baki asie ndugu yako mkiwa mnasalimiana lazima umsalimie kwa jina la babu yake nae atakusalimia kwa jina la babu yako!

Hii kitu wasukuma wanaamini kua katika salamu hizi waweza kutana na ndugu yako kutokana na hiyo historia ya salamu za mababu!

Onepandeka Bhageshi?
 
nimeona post zote hapo juu, mie sio msukuma ila naona kama wakubwa ndio wanaanza kusalimia? wakati sie tumezoea "shikamoo inatolewa na mdogo halafu mkubwa anaitikia" ila kisukuma naona salaam zinaenda kinyume nyume, au mie ndio sielewi?

Je mkeo au mmeo, ama demu wako wanasalimianaje?
Je salamu za kisukuma ni all weather? nina maanisha asubuhi,mchana na jioni zinakuwa costant? kote ni "shikamoo" habari ya asub?
Kina babu na Bibi watakuambia Ng'wanene na wewe utaitikia Lwimbo Kama Eminza, En'gwashi, Emongo, Enkwemba au Eseya n.k

Wajoba,Shangazi,Kina baba na mama Hao ni wazazi.
Wao watakuambia Ng'wamayo au Ng'wabhaba;
Na wewe ni kuitikia Lwembo Kama hapo huu kwa mababu na Bibi!

Kaka zako Wa Tumbo Moja au Wa baba mkubwa au mama mkubwa Hao watakusalimia Ng'wagoko, nawe utaitikia Lwimbo Kama hapo awali!

Watoto Wa kike Wa Tumbo Moja na Wa baba mkubwa na Mdogo na mama mkubwa na Mdogo Hawa wote ni wadogo kwa watoto Wa kiume ata Kama wanakuzidi umri!
Hawa wote unawasalimu Ng'wagoko na Wao wataitikia Lwimbo Kama kawa!
Watoto Wa Mjomba na Shangazi!
Hapa kwa kawaida abana Ba nsheke na batale!
Yani Hapa watoto Wa Shangazi ndio wakibwa!
Nao watakusalimia baba au mayo ng'wagoko nawe utaitikia Lwimbo!.
Nawe ukishakua na watoto utafanya Kama baba zako au wajomba zako na ukiwa na wajukuu utafanya Kama babu au Bibi zako!
Welelwa ahene bahebu?
 
bhe bhe Ntuzu. ubhese abha NG'HWANZA, ung'wana ong'o sengi ate ntale alendo, uwang'wa mami huntale, hanumayaho utayombage geke welelwa, ulayombage geke odeba nulu omana

Wandya nanho emihayo yako!
On'gwana ommami nd'oo ale ng'wana womsengi!
Ong'gwana onsheke ntale nkoi!
Nayene; Welelwa,odeba ne omana pyeyose yene mihayo yakesukuma ne maanayayo emo do! Got it, gotcha, understand,
 
nimeona post zote hapo juu, mie sio msukuma ila naona kama wakubwa ndio wanaanza kusalimia? wakati sie tumezoea "shikamoo inatolewa na mdogo halafu mkubwa anaitikia" ila kisukuma naona salaam zinaenda kinyume nyume, au mie ndio sielewi?

Je mkeo au mmeo, ama demu wako wanasalimianaje?
Je salamu za kisukuma ni all weather? nina maanisha asubuhi,mchana na jioni zinakuwa costant? kote ni "shikamoo" habari ya asub?

Demu au Mke unamsalimia Ng'wagoko na yeye ataitikia Lwimbo!
 
Je na salamu anaanza nani? yoyote, mkubwa au mdogo? je salamu za kisukuma zipo Constant muda wote jioni au asub?

Salamu anaanza yeyote na mkisha onama kwa Mara ya kwanza ndo mnasalimiana hivo kwa Lwembo lakini mkiwa mnaona kwa Mara ingine tena katika siku hiyo mnasalimiana Kama kawaida bila Lwimbo!
Kwa kawaida wewe unaemkuta mtu ndio unaanza kusalimia
 
thanteee, hivi wasukuma wote mpo sawa hakuna tofauti yoyote? i mean msukuma wa Lamadi,Magu,Kahama, Sengerema, Misungwi,Bariadi,etc hakuna tofauti,behviours, matamshi,miiko,tambiko,etc sitaki kuleta mgawanyiko au matabaka
Salamu anaanza yeyote na mkisha onama kwa Mara ya kwanza ndo mnasalimiana hivo kwa Lwembo lakini mkiwa mnaona kwa Mara ingine tena katika siku hiyo mnasalimiana Kama kawaida bila Lwimbo!
Kwa kawaida wewe unaemkuta mtu ndio unaanza kusalimia
 
Wasukuma ni jamii kubwa sana na Ina matabaka mengi!

Yes ni jamii kubwa inawezekana ndio yenye eneo kubwa tanzania hii, covering maeneo ya Mwanza ya zamani,shinyanga ya zamani, sehemu ya mkoa wa mara na Kagera,Tabora,Singida, hivi wasukuma wote wapo sawa hakuna tofauti yoyote? i mean msukuma wa Lamadi,Magu,Kahama, Sengerema, Misungwi,Bariadi,etc hakuna tofauti,behviours, matamshi,miiko,tambiko,etc sitaki kuleta mgawanyiko au matabaka
 
Tofauti zipo
 
Wasukuma Karibu wote wanalingana desturi miko tamaduni na kusikilizana bila kujali ni Wa eneo gani!
Ila kuna baadhi katika matamshi wanaweza pishana na Wa sehemu ingine! Kama ilivyo kiingereza cha Us na Uk na Australia! Lakini chote ni kiingereza!
 
Back
Top Bottom