John_Anthony
Senior Member
- Mar 27, 2024
- 190
- 314
Natumaini wote mko poa ndg wana JF,, lakini poleni sana kwale wote wenye changamoto yoyote ya kiafya au maisha kwa ujumla poleni sana Mungu awasaidie mkae sawa 🙏
Ndg zangu nimeamua kuandika uzi huu kutokana na mambo yanayo fanyika kwenye jamii zetu haya mambo yanaumiza sana😭 mitaani kumekuwa na vifo vingi sana vya watu baadhi vinaeleweka vizuri na wana jamii huku vingine vikiwa ni vya kuhisiwa tu kuwa huenda amefanywa hivi au
Lakini la kusikitisha zaidi kuna kuwa na watu wanao shuhudia kabisa mwanzo wa tukio mpaka mwisho lakini wanakausha kama vile hawajaona chochote ila mtu ndio tyr kafa hivo inabaki tu minong'ono ya chini chini wakifika polisi hao watu hujitenga kabisa tena wengine huondoka kabisa eneo la tukio,,, haya yote hutokea kwa sababu ya sheria na mifumo kwa askari walio wengi, shahidi akijitokeza kutoa ushahidi wake wana shughulika zaidi na huyo shahidi kuliko kushughulikia tukio zima yani yanageuka kuwa majuto kwa mtoa ushahidi hawafikirii kuwa huyo mtu ameguswa na matukio yanayo fanywa na baadhi ya watu wao hufikiria mtoa taarifa kuwa ana kiherehere kwahiyo wanakula sahani moja na shahidi tumeshuhudia watu wengi walio jaribu kusaidiana na askari kushughulikia waharifu lakini mwisho wa siku shahidi ndio anakuwa mwaharifu yaani,, yani askari badala ya kumpongeza mtoa ushahidi lakini wao wana mchallenge kupita kawaida hadi mwisho wa siku shahidi anashindwa anakuwa mtuhumiwa mwenyewe
Kwa kifupi hiyo ndio taswira tu ya mambo yanayo endelea kwenye jamii hadi kwenye suala la vifo kutoa ushahidi inakuwa ni kiherehere
Kuna siku moja nilipita barabara flani hivi nilikuta mtu amegongwa na gari gari lililo mgonga huyo bwana lilikuwa limepitiliza haraka kwahiyo halikueleweka kuwa ni gari gani japo kuna wengine walilitambua hilo gari lakini walikausha, huyo bwana alikuwa liye gongwa alikuwa amebaki pale barabarani hakuna mtu aliye msogelea wala kumgusa na vyombo vingine vya usafiri viliendelea kumkwepa akiwa pale pale,, mimi nilivoona watu wanashangaa tu hawataki kuenda kumsaidia nilijaribu kuwa hamasisha "jamani tuendeni tumsaidie mwenzetu..." watu walisema wanaogopa wakimgusa yule bwana eti wataacha alama za vidole itaonekana wao ndio wameua 😭😭 kwahiyo tuliendelea kumshangaa pale huku wengine wakihangaika kuwaita polisi mwisho mimi uvumilivu ulinishinda niliamua kuenda hivo hivo bahati nzuri kuna jamaa mwingine alikuwa ameguswa na hilo tukio yeye alikuwa ana bajaji kwahiyo tulimbeba yule hadi hospitalini alikuwa bado hajapoteza maisha ila alikuwa amepoteza fahamu,, lakini kitu kingine cha ajabu tulivo mfikisha hospitalini tulijielezea na kueleza hali ilivo kuwa madaktari wakasema huu msalaba tunaubeba sisi tulio mpeleka pale kwa kuna gharama tulitakiwa tulipe kwa sababu haikujulikana kama ana bima au la! hivo sisi tulitakiwa kuullipia gharama zinazo husika kwenye ufunguaji wa faili bahati mbaya sana hiyo siku mimi na mwenzangu hatukuwa na hela za kutosha kulipia pale kwahiyo mgonjwa aliwekwa kando kwa muda 🥲 tukisubiri ndg zake waje na hii kesi siku sikia lolote mpaka sasa wala haikusemwa popote wala hakuna askari yeyote akijihusisha na hili tukio
Hii ndio hali halisi zinazo endelea kwenye jamii, watu wanaogopa kushiriki kwenye kutoa ushahidi hatakama mtu amepatika amekatwa katwa mapanga ikionekana tu uwezekano wa kupona huyo mtu ni mdogo watu wanakula kona,,
Mimi nimeandika tu huu uzi wala sifahamu kama unaweza kubadilisha chochote 🥲 lakini huku kwenye jamii zetu kumejaa maovu sana kama kuna mtu upo kwenye cheo fulani huko serikalini au upo kwenye harakati hizo nawaombeni mlitazame hili pia 😐 raia wanateseka sana watu wanapoteza ndugu zao bila sababu zozote za msingi HII AMANI INAYOSEMEKANA KUWA NCHI INA AMANI TUNATAMANI IWE NI AMANI YA KWELI KWA RAIA WOTE
Asanteni sana kwa kuvumilia kusoma huu uzi 🙏🙏 naamini nimeeleweka maana yangu ni ipi