Rungwe: DC Haniu atoa neno Maadhimisho ya Siku ya Lishe, asema lishe imesaidia kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi kupanda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,925
12,208
Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya yamefanyika leo Oktoba 30, 2023 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Katumba II , Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu.

Haniu amepongeza kwa hatua nzuri ya lishe iliyofikiwa katika Wilaya ya Rungwe akitaja kuwa Udumavu kwa watoto kwa sasa umefikia Asilimia 26%.

Haniu Oc.jpeg


Haniu ameeleza kuwa Takwimu hizi zimewezekana baada ya Wananchi kuanza kuitikia wito wa kula chakula bora chenye viini lishe na hivyo kuondoa Utapiamlo pamoja na Udumavu.

Ameeleza kuwa changamoto ya ukosefu wa lishe itazidi kutokomezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya uelewa wa masuala ya lishe katika jamii, ngazi ya familia, watendaji na viongozi wa Serikali.

Aidha, lishe imesaidia kupandisha kiwango cha ufaulu ambapo katika mitihani ya utamilifu (MOCK) pamoja na Taifa (NECTA) Wanafunzi wamekuwa wakifanya vizuri kutokana na lishe.

Haniu Oktoba 30.jpeg


Kwa miaka mitano mfululizo Rungwe imekuwa ikishika nafasi ya pili katika Mkoa wa Mbeya baada ya Jiji katika mitihani yote na mpango ni kushika nafasi ya kwanza 2023/2024.

Mpaka sasa Wanafunzi wanapata chakula cha mchana kwa Asilimia 100 (100%) katika Shule za Msingi na Sekondari.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya haya ni "Lishe bora kwa vijana Balehe, Chache ya Mafanikio yao".

Kauli hii imepewa kipaumbele kwa Vijana kuelimishwa kuwa lishe bora husaidia kujenga mwili, kulinda mwili pia husaidia kumuandaa kijana kuwa mzazi bora kwa kuimarisha mifumo ya uzazi.

Naye Afisa Lishe Wilaya ya Rungwe, Halima Kametha ameongeza kuwa Lishe Bora hutunza mwili wa kijana na kumfanya achelewe kuzeeka, hivyo kuongeza muda wa kufanya kazi (Productivity time) na kuongeza pato la Taifa kwa kupunguza wategemezi (Dependence Population).
 
Huyu huyu Haniu aliyeshindwa kuandika kiasi cha fedha kwa maneno hadi akaondolewa kitengo cha habari pale ikulu? Bado unataka tuendelee kusikiliza na kuamini anachosema?
 
Udumavu wa mwili pia huchangia udumavu wa akili, ndio maana tuna raia wengi sana wanaonekana hawana akili kila wanapozungumza.
 
Back
Top Bottom