TANZIA Rubani wa Ndege iliyotekwa 1982 kushinikiza Nyerere ajiuzulu afariki dunia

Ndege ya ATC ilitekwa kwa mabomu na pistol za mbao, seriously. Captain na crew yake walitaka kwenda London, na siyo kwamba walihofia maisha yao. Baada ya kufika London, hakuna abiria waliyoomba hifadhi ya kisiasa au kugoma kurudi zaidi ya Watekaji?
Hujui kitu wewe, walioteka walipofika Stanstead Airport waliomba hifadhi ya kisiasa na wakafungwa. walipotoka wakaishi kikimbizi,. Moussa Memba, Yasin Member na vijana wawili wa kizanzibar waliokulia Dar. Moussa alirejea bongo akakamatwa alifia jela. Yasini nae alirudi bongo kwenye 2000s bahati mbaya nae alifariki.Wale vijana wa kizanzibar mpaka leo wapo hapo London.
 
Hujui kitu wewe, walioteka walipofika Stanstead Airport waliomba hifadhi ya kisiasa na wakafungwa. walipotoka wakaishi kikimbizi,. Moussa Memba, Yasin Member na vijana wawili wa kizanzibar waliokulia Dar. Moussa alirejea bongo akakamatwa alifia jela. Yasini nae alirudi bongo kwenye 2000s bahati mbaya nae alifariki.Wale vijana wa kizanzibar mpaka leo wapo hapo London.
Huna jipya kaa kimya. Najua hayo yote na zaidi. Nilikuwa nafuatilia hii kesi kwenye magazeti ya Uhuru na Mzalendo pamoja na Daily News enzi hizo. Wee nadhani ulikuwaa aidha hujazaliwa au toddler unanyea nappy.
 
Walitua Stanstead, London kipindi cha winter wakitokea Dar es Salaam hali wamevaa mashati na wengine T-shirt.

Walipigwa na baridi ambayo walidai wasingeweza kuisahau maishani mwao. Huu ni ushuhuda wa mmoja wa wazee waliokuwa wahanga wa hiyo hi- jack.

Walipata msaada wa mavazi ya kujikinga na baridi baada ya kuonewa huruma na bi kizee mmoja aliyekuwa akitembeza mbwa wake jirani na uwanja huo ambako aliwaona wakitetemeka kwa baridi.
Kwahiyo wale abiria mateka waliruhusiwa kuingia mitaani London baada ya kuwasili Stanstead Airport hadi waonane na bii kizee na mbwa wake? Kuna ukweli wowote hapa?
 
lord rajipar nyumba zake pale mikocheni wamepewa maafisa wa polisi
Lord Rajjpar alikuwa rafiki wa karibu sana wa Rashid Kawawa, kwani walitoka Wote huko kusini mwa nchi kwa hiyo mara nyingi akimkingia kifua alipopata matatizo!! Kuna wakati walimuandama sana SIMBA WA VITA juu ya uhusiano wake na Rajjpar, akawajibu mbona hamumsakami Nyerere juu ya uhusiano wake na Amir Jamal? Akawaambia kila MTU na MUHINDI WAKE !! Ngoma Ikawa droo na ukawa kwisho wao kumuhasama Kawawa kwasababu ya Rajjpar!
 
Mwaka 1985, age, 9 years ndio mmeingia kwenye Boeing 737 kuelekea mwanza. Mnatangaziwa captain Leo wa ndege atakuwa George Mazura.

That feeling ilikuwa ndio definition ya adventure enzi zile
kweli miaka imeenda.

RIP Mazura,


Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
 
Hii Family ya kina Mazula ilikuwa na Rubani mwingine akiitwa George Mazula baba yake Walter Mazula aliyeuwawa kinyama huko USa 2006. Nilikuwepo kwenye Msiba wa Walter na Mchumba wake Vonetha Nkya. Captain George Mazula alisoma Risala Bora kabisa na Mwanae Brian. Daah 2008 nikasikia Captain George Mazula alifariki, kumbe alikuwepo nduguye naye ni Rubani wa Ndege. Miaka hiyo ya 80+ na 90+ ukisikia Rubani unamheshimu na George Mazula tulimfahamu na kumpenda he was down to earth Mpenda Watu pamoja na umaarufu wa kuwa Rubani wa ATC. RIP Mazula George, Walter na Deo.
 
Walikuwa ni mtu na kaka yake, na wote brand cars zao zilikuwa ni Volvo, enzi hiyo mawaziri gari zao zikiwa ni Pegeot 504 number zikiwa STC na STD!. Gari za polisi zilikuwa Landrover 109, na escort ya Nyerere ilikuwa Peogeot 404. Benzi yenyewe ya Nyerere naomba nisiseme, ila kulikuwa na mhindi tajiri kwa jina la Lord Rajipar, akaleta Benz kali kuliko ya Rais, S Class 500 miaka hiyo!. alitiwa ndani kwa uhujumu!.
Rip Capt. Mazula umetukumbusha mbali!.
P
Hahaahaha ila huyu mzee sometime alikuwa wa ajabu sana.
 
Humu kuna Babu , Baba zako hivyo ni lazima uwe na heshima ama sivyo unaweza pata laana VIRTUALLY!!!!
Na mimi nilishagundua hilo, unaweza kuwa unatukana kisela-sela-jinga kumbe unamtukana baba/mama/ babu/nyanya yako.

Bora tu kuwa na adabu na lugha hadhimu ya staha!
 
Back
Top Bottom