Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Nimapito magumu na yenye huzuni na masikitiko ktk historia ya ukombozi wa taifa letu.
Tumempoteza mpambanaji. Ni mapenzi ya mungu tutakuombea na kukuenzi daima,. Tunaamini kwakua ulilitendea taifa hili na watanzania mema yote mungu atamlipa kadri ya matendo yake.

Wote tu marehemu wtarajiwa. Tuishi katika mungu na kutimiza wajibu wetu.
Tumuenzi Regia kwa kuyaenzi aliyo yaamini. Kufa kwa mpambanaji mmoja kulete dhamira na mwamko wa wapambanaji 100 kuziba pengo na kupigania haki za watanzania wasio na wakuwasemea.
Mapambano aliyoyaanzisha hayatakoma kamwe.. Tutakosa sana taarifa za mikutano,matokea mbali mbali ya chama na maandamano ya chama.

Tunahitaji mbadala
 
Yani Regia kama vile nilikufahamu miaka mingi ni ngumu sana kuamini umeondoka milele. Jamani kifo hakielezi.

Really gonna miss heading your articles about our Tz, chat with you and dadas talk..Pole sana kwa familia&Tz nzima.

[video=youtube_share;NxIYxPiK1c4]http://youtu.be/NxIYxPiK1c4[/video]

Asante kwa huu muziki kaka,angalu nimefarijika kidogo.....Its tru We gonna miss you Regia...RIP
 
Yaani ni kama ndoto......

Kwangu mimi Regia alikuwa ni zaidi ya Mbunge/Mwanasiasa ndani ya JF.......Alikuwa ni mtu maalum hasa......Hakika nimeumizwa sana na taarifa hizi na hata nilipopigiwa simu kuelezwa kwamba mpendwa wangu Regia amefariki sikuamini,nilikataa katakata.....Ameondoka mapema sana Regia wetu....

Regia pamoja na kupata ubunge hakuitenga/kuiacha JF......Daima alikuwa nasi katika shida na raha na alijitahidi kuutumia muda mchache anaoupata kuja humu kutujuza mambo mbalimbali yanayojiri bungeni na katika medani za siasa kwa ujumla......She was born for JF na JF tutamlilia daima....


Yeye ni tofauti sana na wanasiasa wengine ambao waliitumia JF kama daraja la mafanikio yao kisiasa na mara baada ya kufanikiwa kisiasa wanaacha kabisa kuingia JF,Regiia/GS hakuwa hivyo........Yeye daima tulikuwa nae JF,hakuchagua jukwaa....Jukwaa la siasa utamkuta,MMU kama kawa, kule kwetu kwenye Michezo na Burudani kulikuwa kwake pia.....Chit Chat ndo usiseme, yaani alikuwa anaingia kila jukwaa tofauti na wanasiasa wengine ambao wao kila siku ni SIASA tuuuu.....

Kwangu mimi Regia alikuwa zaidi ya ndugu,sikujuana na Regia tangu utotoni wala sehemu yoyote nyingine, nimekutana nae JF na tangu tumefahamiana nae tumekuwa zaidi ya ndugu.......Kwa hakika hili ni pigo,sisi tumempenda lakini Mungu amempenda zaidi....

Upumzike kwa amani dada yangu mpendwa Regia...

 
Last edited by a moderator:
Sisi kama wana JF tulimfahamu mwanzoni kama "Gender Sensitive" Na kwakweli alikuwa anatoa hoja nzito na michango yake mingi wengi wetu humu tuliipenda, ilikuwa ni kama safari yake ya kisiasa ilianzia hapa JF.

Ndipo akajitambulisha rasmi kuwa yeye anaitwa Regia Mtema na kwamba ni mwana CHADEMA, pia kwamba atagombea ubunge, wengi humu walimsapoti kwa hali na mali, wengi just ushauri, positive criticism, na wengine just words of encouragement.

We will definetly miss you Regia Mtema.

Its so hard to absorb, but then it is the fact that we are all gonna leave this world one day.

RIP Regia Mtema.
 
TUNAOMBA MUONGOZO WA INVISIBLE ..INAPOTOKEA MEMBER KAMA HUYU KATUTOKA HASA WALE AMBAO WAMEAMUA KUWA MSTARI WA MBELE KWA KUWEKA MAJINA YAO DHAHIRI.....BASI KWENYE HOME PAGE TUKIFUNGUA TUONE PICHA YAKE KWA SIKU ZITAKAZOKUBALIKA...NA BENDERA YA JF..ambayo ina nembo ya JF ..IONESHWE IKIPEPEA NUSU MLINGOTI..

NAOMBA KUTOA HOJA!!!
[/QU NAUNGA MKONO HOJA

Naunga mkono hoja asilimia mia moja kwa mia moja
 
Nenda dada,tangulia na sisi twaja mpendwa,
umeimaliza kazi, vita umevipiga vema,
tutakukumbuka kwa wema wako kujituma na kujitolea kwa watanzania.
ulipigana bila kuchoka mchana na usiku,jamvini hukukosa kutuletea habari.
Mbeya hukukosa,Mwanza ulifika, Arusha nilikuona, Igunga ulitisha.
Bungeni hukulala mpaka kilipoeleweka,kilombero kama kawa, hata jangwani ulishiriki.
Ulikuwa front line,kuitafuta Tanzania tunayoiota,kwenye jua ulisota huku umepiga kaki.
kaki ilikuwa ishara kwako, kwamba hakuna kulemba.

mpendwa dada, najua utaonana na makamanda wengi ila kwa leo naomba kipekee kabisa
unisalimie hawa wafuatao; Chacha Wangwe, Shirembi (IGEMBE),Sylvester Rwegasira, Martini Luther king,Samora Machel,
John Garang,Robert Owuko,Edward Sokoine, Lucky DUbe,Mohamar Gadaf,Patrice Lumumba,Solomon Mahlangu, Jaramog Oginga na Ken Saruiwa. Waambie tunawakumbuka sana na kwamba tunaendeleza mapambano MPAKA KIELEWEKE.

La mwisho kabisa dada mpenzi, nakuomba uniwekee kiti karibu na wewe ili nikija nikae karibu na wewe.

"NOT YET UHURU, ALLUTA CONTINUA"!

Wasalaam,
Mtolewa.
 
Rip Regia. Thank you for all that you have been able to do for your people. Thank you for reminding us it is not what we take when we leave this world behind, but it is what we leave behind us when we go. You blessed and inspire so many people more than you can realize; you affected those around you in profound ways. Rest be assured that; your work in this world will never be forgotten. We surely wish we could have you around for many more years; but who are we to say? God does not always grant our wishes however; his decision is always right and final. We love you Sis.
 
Ni pigo na pengo lisilozibika,
Tumkumbuke kwa mapenzi mema na kujali kwake. Alikuwa ni msikivu, mkweli, jasiri na machangamfu. Nyota yake ilianza kung'ara lakini itaendelea kung'ara hata baada ya kuondoka kwake.

Mungu atufariji wafiwa na watanzania wote.

Natoa pole zangu binafsi na familia kwa ninyi nyoote na jamaa wa marehemu.
Amen.

HIZI AJALI hizi?!!
 
tutakukumba daima dada yetu regia



safi sana invisible and management.....this befits a hero....na uwe utamaduni wetu ..huu kuwaenzi wenzetu...watakaotutangulia....jf ni hazina kubwa nchi hii na ni chachu ..ya mapinduzi ya kweli..yeyote aliye mwanachama humu ndani yupo vitani....na akifa anakufa kishujaa.......askari hata akifa kwa malaria..amefia vitani na anazikwa kikamanda kwa heshima zote....
 
Nalia nalia nalia...umeniachia deni kubwa sana!!!! Kuna kitu uliniuliza hapa ofisini ili nikupe data kamili bt nilikuwa nakuzungusha kila siku! Regia pumzika kwa amani!
 
ngoja nipumzike kidogo kwani toka mchana nilipopata hizi taarfa nilikuwa niko powa tu nikijua ni jambo la kawaida na mipango ya Mungu lakini kila ninavyozidi kusoma hizi pos hapa naona machozi yanataka kunitoka kwani wadau wanavyomchambau hapa ni kweli hakustahili kuondoka mapema kiasi hiki ...nakumbuka sana wakati akijiita GS na akatangaza kuwa atagombea ubunge wote tulipatwa na msisimko na badae akajitangaza hapa JF kuwa anaitwa Regia ..so sad guys and RIP our beloved sister.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom