Someni Lena Maria Klingvall. Na Yule mwanariadha wa south Africa ambaye ni mwenye matatizo ya miguu na anataka kushiriki michezo na watu ambao wana miguu.
Thread hii inakera sana ili inabidi tujifunze kuwa watu handicapped wana uwezo wa kufanya vitu vingi sana kuliko hata watu wa kawaida.
Tuamke!!!!!!!!
Mkuu kama kwa kuuliza hivyo ni ujinga basi wajinga tuko wengi, mimi nimejiuliza hilo swali toka jana nilivyopata habari kwamba alikuwa anaendesha mwenyewe, tunajua kifo hakizoeleki lakini kila siku tunalaumu madreva ajali zinapotokea nyingi ni ubovu wa barabara na uzembe wa madreva pia, hii ya Mheshimiwa lazima watu wajiulize ilikuwaje akaendesha yeye with physical disability tena umbali mrefu kiasi hicho, Mheshimiwa ametangulia mbele za haki na wahenga wanasema ajali haina kinga lakini kuchukua tahadhari kwa ajili ya usalama wa maisha yetu na wengine ni muhimu sana.Nimeuliza swali la msingi sasa natukanwa mimi ni mjinga haya....nabaki na ujinga wangu lakini I promise....road accidents will continue to take its deadly toll if the authorities continue with business as usual
Jamani tusiwe na dabo standadi hapa, kama kuna hoja ya maana ijadiliwe.
Wamekufa wangapi na maswali kibao yakulizwa?
Kusema kweli we need to know this, je kuna utaratibu gani kwa watu wenye haloi kama yake kupata leseni na aina ya magari wanayotakiwa kuyatumia.
Itakuwa ni upuuzi kukwepa hoja ya msingi kwa kisingizio cha majonzi, na je kama majonzi hayo yameletwa na uzembe wa hoja inayoulizwa?
Kuna watu humu tayari wamesha fungua sredi eti kuna mkono wa serikali na wakaungwa mkono kwa nguvu zote, lakini inapotokea mtu akadadisi uhalisia anakua amekosea timing kipindi cha majonzi
Tujadili now, pamoja na kifo na majonzi tuliyo nayo lazima maisha mengine yaendelee, tujuwe tatizo right now kuokoa wengine na janga hili
Mkuu unahita investigation gani iwapo taratibu zipo wazi kabisa mtu mwenye hali kama yake anatakiwa kuendesha gari lililokuwa modified kwa hali yake, Gari alilokuwa anaendesha halikufanyiwa chochote.
Hapo kwenye red kuna exemption kwa kesi hii ya kifo cha Mhe Regia au ni kwa wote...............what a double standard
Kwanini tunakimbia vivuli vyetu kwa kisingizio cha majonzi, Misiba imejadili mingapi humu kwa style hii? Tusiendeshwe na hisia binafsi zaidi kuliko uhalisia
Labda nikupe maelezo ya wenye mamlaka ya kutoa matamko kuhusu ajali hii
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.
Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.
Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka, alisema Mbaga.
Chanzo HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu
Kwa mfano mimi leo ndo najua kuwa hilo eneo la ajali ni baya sana,ina maana bila huu mjadala nisingefahamu.So ndugu tuna majonzi lakini yale ya msingi tuyajadili tu ili tuendelee kujiokoa wenyewe maana tukiwategemea wenye mamlaka bado wako likizo ya x mas na mwaka mpya.
Umepitwa na wakti ww, nenda pale nssf akiba ulizia mlemavu anaendesha gari,
Tena gari yenywe mbenz!!!
Utaonyeshwa kijana niliyesoma nae, tukiwa shule alikuwa akitamba kwa magongo hadi leo hii.
Cha ajabu nini hapo?
Kwa ajali hili; taarifa ya polisi inaonyesha kama tayari wameshahitimisha chanzo cha ajali, jambo ambalo siyo sahihi. Swali la msingi ni kwanini mheshimiwa alishindwa ku-control gari baada ya kutaka kurudi upande wake. Je ni kutokana na hitilafu ya barabara (kama wengine wanavyo-comment), hitilafu katika gari au makosa ya dereva? (kivipi).
Wote tuna uchungu,inashangaza watu wanatukana!
Niswali la msingi na wala siladhiaka kama Brugita ulivyodhani yakupasa kuwa nasubira japo yawezekana unahusika mojakwamoja na msiba huo nakama alikuwa anaendesha gari ambayo haikuwa nanyenzo za walemavu basi serikali has Bunge la JMT wanatakiwa kushitakiwa!
baadhi ya majibu yapo kwenye habari leo.Gari ilikuwa RHD,RIP dada Regia,I will miss you.mpaka sasa mnasisitiza swali, toeni majibu basi.
Kwa ajali hili; taarifa ya polisi inaonyesha kama tayari wameshahitimisha chanzo cha ajali, jambo ambalo siyo sahihi. Swali la msingi ni kwanini mheshimiwa alishindwa ku-control gari baada ya kutaka kurudi upande wake. Je ni kutokana na hitilafu ya barabara (kama wengine wanavyo-comment), hitilafu katika gari au makosa ya dereva? (kivipi).