Rais Samia, tafadhali usianzishe mchakato wa Katiba mpya mpaka ujiridhishe usimamizi wa mchakato huu

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,383
Wakuu,

Mwanzo kabisa napenda ku-declear interest kwamba mimi natamani nchi yangu Tanzania ipate katiba mpya.

Mjadala wa katiba mpya ni mjadala mrefu sana unaohitaji umakini, utashi na ujuzi juu ya mambo yahusuyo sheria na uendeshwaji wa nchi.

Katiba ni mjumuisho wa taratibu, sera, sheria na miongozo mbali mbali ambayo jamii flani inaitumia kujiendesha.

Katiba ya sasa ya Tanzania ilipitishwa/ ilipewa mamlaka kisheria kutumika kama katiba rasmi mwaka 1977, na ndio maana inaitwa Katiba ya 1977.

Pamoja na katiba hii ya 1977, TANZANIA imepata kuwa na katiba tatu hadi sasa ambazo ni:-

1) The Interim Constitution of United Republic of Tanganyika and Zanzibar(1964)- Ilipatikana kupitia mamlaka aliyopewa Rais wa JMT kupitia notisi ya serikali nambari 246 ya tarehe 1 Mei 1964, akiifanyia mabadiliko iliyokua ikiitwa Republican Constitution ya mwaka 1962 (ambayo kimsingi ilikuwa ni katiba ya Jamhuri ya Tanganyika) na sio ya Tanzania.

2) The Interim constitution of United Republic of Tanzania (1965), katiba hii ilitoa mamlaka ya juu kwa vyama vya siasa, Kupitia kamisheni aliyoiunda Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Nyerere, bunge la muungano lilitangaza "act" iliyoitangaza "Interim Constitution of Tanzania na ikaeleza uwepo wa chama kimoja ndani ya Tanzania na ndani ya Zanzibar ambapo tulikuwa na TANU na ASP.

3) The Constitution of United Republic of Tanzania (1977), katiba hii ilipatikana kutokana na muungano wa vyama vya TANU na ASP vilivyozaa CCM. Tangu kutungwa kwa katiba hii, imefanyiwa mabadiliko mara kadhaa ili kukidhi haja na matakwa ya yakati husika.

Mchakato wa kutunga katiba mpya hugharimu muda mrefu na fedha nyingi mno, inahitaji kuwa ni mkakati wa kitaifa na agenda hiyo ibebwe na serikali kwani budget ya gharama za mchakato huo inabidi iwepo. Mbali na rasilimali hizo mbili, katika mchakato huu rasilimali muhimu kabisa ni WATU. Watu wa kusimamia mchakato huu. Unahitaji watu wazalendo haswa, ukweli wa neno lenyewe UZALENDO na sio Wazalendo wa aina ya Serikali ya awamu ya tano. Watu ambao watakuwa na mapenzi ya dhati ya nchi yao na vizazi vya nchi yao. Watu ambao labda kwa asilimia kubwa hawatoangalia maslahi yao kama kizazi, bali wataangalia zaidi maslahi ya Tanzania ya sasa, ya baadae na vizazi vijavyo.

Msingi wa mada hii ni kumshauri Mheshimiwa Rais wetu kipenzi Mama yetu Samia Suluhu Hassan ASIANZISHE mchakato huu mpaka atakapojiridhisha juu ya weledi, uwezo, uzalendo na nia njema ya wale ambao anataka au inabidi awateue. Tunaweza kuwa na muda wa kutosha wa kuliendea suala hili, tukawa na fedha za kutosha za kuliendea suala hili lakini kama hatutakuwa na watu sahihi wa kuwakabidhi ushughulikiaji wa suala hili basi mchakato mzima unaweza ukawa useless.

Mimi naamini Mheshimiwa Rais Mama Samia amedhamiria kuipatia Tanzania katiba mpya kabla ya mwaka 2025, zipo kelele nyingi sana kwamba inabidi mchakato huu uharakishwe, kumeanzishwa movement za kuharakisha suala hili, mimi nadhani Mama anahitaji muda kupanga mambo mengi sana yahusuyo suala hili. Huu si wakati muafaka wa kum-pressurize Rais, tunamuhitaji awe kwenye good state of mind katika kulitekeleza suala hili vinginevyo anaweza kulifanya suala hili ili kuwaridhisha watu flani na hatimae tukaja jutia juu ya uamuzi huu wa kupiga kelele juu ya suala hili.

Wananchi wanapaza sauti juu ya uhitaji wa katiba mpya ya JMT, ni watu wangapi kati ya watu milioni 60 wenye uelewa juu ya suala la katiba? Nikionacho mimi ni kwamba watu wengi wana uhitaji wa mabadiliko ya baadhi ya mambo tu kwenye katiba ya sasa. Kwa mfano
  1. Aina ya muungano tuliokuwa nao una mashaka kwa hiyo inabidi ubadilishwe, uwe wa serikali moja au serikali tatu.
  2. Mamalaka makubwa aliyokuwa nayo Rais wa JMT ni makubwa sana inabidi yapunguzwe.
  3. Upatikanaji wa baadhi ya Taasisi na Mamalaka za kitaifa zifanyiwe reforms ya hali ya juu. Kwa mfano Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kama hivyo ndivyo, na kwa kuzingatia mambo niliyoyataja hapo juu, basi ni dhahir kuwa ikishindikana kuwa na mchakato mzima wa katiba mpya basi kufanyike japo marekebisho tu ya baadhi ya vifungu ambavyo vinaonekana kukwaza watu wetu (Watanzania).

Wananchi ni lazima wafahamu kwamba katiba yoyote ile itakayokuja, bado wapo watu tu itabidi wakabidhiwe mamlaka ya utendaji wa mambo, mamlaka hayo yanaweza pia kuwa makubwa kama ambavyo sasa hivi mwenye mamlaka hayo ni Rais. Kwa mfano, kwa mujibu wa katiba ya sasa ya India, Chief Justice na all judges of supreme court wa India wanachaguliwa na rais wa India. Watu hao tunaweza sema wasiteuliwe na rais lakini lazima mamlaka hayo ya uteuzi yatakwenda kwa mtu mwengine tu. Haiwezekani kusema watu hao wawe wanapigiwa kura. Kwa mujibu wa katiba ya India, Rais wa India anachaguliwa na members of electrol college consisting of elected members wa parliament na legislative assemblies tu. Yaani kunakuwa na watu wachache waliochaguliwa kwa mfumo flani hivi ambao watu hao ndio wana jukumu la kumchagua Rais wa India, je hii hatuoni kama ni mbaya zaidi??

All in all, mawazo yangu na Ushauri wangu kwa Mheshimiwa Rais ni kwamba, ASIUANZISHE mchakato wa katiba mpya mpaka pale ambapo atayapata majina ya watu SAHIHI watakaounda tume ya kuhusika na suala hili. Unless kama tunataka kuendelea na rasimu ya Jaji Warioba. Lakini hata kama tunataka kuendelea na rasimu ya Jaji Warioba, basi personell wa bunge litakaloshughulikia mchakato huu itabidi wabadilike. Kwa mfano, Mama yeye alikuwa ndiye Makamu Mwenyekiti wa kudumu wa bunge lile maalumu la katiba, sasa hivi ni rais na itabidi tuwe na mtu mwengine kwenye nafasi yake. Tunachokiomba ni watu hao lazima wawe ni watu sahihi, hususan kama mchakato unaanzwa upya.

Wana JF wenzangu, huu ndio uwanja wa Great Thinkers. Hebu tumsaidieni Rais kwa angalau tu kujadili issues hizi,

(a) Je, mama inabidi ateue tume mpya ili ianze upya mchakato wa ukusanyaji maoni na kuandaa rasimu nyengine? au twende na rasimu ya Jaji Warioba? toa sababu za kwanini unapendekeza unalolipendekeza.

(b) Kama unashauri tuanze upya, je ni nani anafaa kuteuliwa kama mwenyekiti wa tume hiyo? kaimu mwenyekiti na wajumbe?? Tuchukulie nafasi ni watu 30 tu kama alivyoteua Mheshimiwa Kikwete.

Kupitia issue hizo mbili tu, tutaona ni namna gani suala la katiba mpya lilivyo gumu na linavyohitaji ustadi na weledi wa hali ya juu kulitekeleza.

Karibuni Tujadili na I stand to be corrected.
 
Katiba inahitaji watu makini sana mzee warioba alitakiwa kurudishwa kumalizia

R.I.P DR MVUNGI
Ni kweli mkuu,

Ila pengine Mzee Warioba hayupo tena na uwezo kiafya na kiakili kuendeleza alipoishia. Hebu toa maoni yako juu ya hoja zilizomo kwenye bandiko hili maana tutafanya tujuavyo ili link ya huu uzi umfikie Mheshimiwa rais, apitie maoni yetu wan JF ajue tulisemalo huku.
 
Suala la muungano aliweke pending.

Baada ya hapo afanye constitutional ammendment kwa mambo yafuatayo.
1. Tume Huru ya uchaguzi.
2. Sheria ya vyama vya siasa.
3. Madaraka makubwa ya raisi.
4. Kupeleka madaraka zaidi kwenye halmashauri.

Mabadiliko mengine yatafuata, lakini hayo kwa maoni yangu yanaweza kutufungulia milango ya kuandika katiba bora zaidi.
 
Naunga mkono hoja. Katiba Mpya ni muhimu sana kwa mustakabari wa Taifa letu. Kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, kinaweza kusababisha machafuko siku za usoni iwapo kitaendelea kufumbiwa macho na watawala.

Na binafsi ningetamani Mheshimiwa Rais aanzie kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba.
Halafu aitishe upya Bunge la Katiba lenye Wataalamu wengi (walau 80%) kutoka makundi tofauti katika jamii, halafu Wanasiasa wawe 20% pekee kutokana na ukweli kwamba Wanasiasa ni wabinafsi sana.

Na hao wataalamu wawe ni wale tu wasio na harufu ya kujihusisha na siasa za upande fulani, ili kuepusha kile kilichotokea wakati ule kwa baadhi ya wajumbe kuegemea ccm na wengine UKAWA! Na mwisho wa siku ule mchakato kuishia kusikojulikana.

Kuhusu aina ya Serikali, sina tatizo juu ya hilo. Hata kama CCM watashinikiza iwe ya Serikali mbili kwa kigezo cha kuwaenzi Waasisi wake, basi wakubali yale mahitaji mengine ya Wananchi. Mfano kuondoa vyeo vya Wakuu wa Wilaya, Mikoa, nk. Kupunguza ukubwa wa Bunge, kupunguza mamlaka ya Rais, kuwepo na Tume Huru ya Uchaguzi, Kuimarisha Uzalendo wa kweli kwa Wananchi, nk.
 
Nyie ndio mnaocheleweshaga mambo. Hivi suala la katiba mpya ni geni nchi hii? Umesahau mpaka posho zaidi ya Tsh.bilioni 400 zimelipwa kwaajili ya kuandaa katiba mpya?
Halafu iliishiaje mkuu?? Unataka twende tukapoteze tena Bilioni 400 nyengine???
 
..suala la muungano aliweke pending.

..baada ya hapo afanye constitutional ammendment kwa mambo yafuatayo.
1. Tume Huru ya uchaguzi...
Okey, kwahiyo hakuna haja ya kuandika katiba mpya. Ni constitutional amendments tu sio?

Kiukweli mkuu hayo mambo uliyoyataja ndio mambo ambayo yanawakwaza wengi. Hivyo je, tunaweza kuyafanyia mabadiliko mambo hayo tu na tukabaki na katiba hii hii?
 
Katiba nikurasmisha na kuapprove ya jaji warioba

Rasim ya jaji warioba ndio maoni stahiki na halisi ya wananchi.

Kuanza kupata vigugumizi nikupoteza muda nakuchelewesha mambo muhimu ya msingi kiutekelezaji
 
Okey, kwahiyo hakuna haja ya kuandika katiba mpya. Ni constitutional amendments tu sio??

Kiukweli mkuu hayo mambo uliyoyataja ndio mambo ambayo yanawakwaza wengi. Hivyo je, tunaweza kuyafanyia mabadiliko mambo hayo tu na tukabaki na katiba hii hii???

Nadhani hizo amendments ndio zita-set the stage ya kuwa na mazingira rafiki na wezeshi ya kuandika katiba mpya.

Watu wametoka "GEREZANI" muda mfupi uliopita, kuna wengine bado wako "EDA," halafu unataka wakae pamoja waandike katiba mpya?
 
..suala la muungano aliweke pending.

..baada ya hapo afanye constitutional ammendment kwa mambo yafuatayo.
1. Tume Huru ya uchaguzi...
Uko sahihi katiba hii inahitaji some amendments baadhi ambazo ni mahitaji ya wakati huu kwa Sasa kama kuhusu tume ya uchaguzi, baadhi ya vitu ambavyo vimepitwa na wakati kwenye katiba yetu.
 
Naunga mkono hoja. Katiba Mpya ni muhimu sana kwa mustakabari wa Taifa letu. Kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, kinaweza kusababisha machafuko siku za usoni iwapo kitaendelea kufumbiwa macho na watawala...
Mchango murua huu.

Hapa nimepata mawazo kama ambavyo natamani iwe. Tuchangie kwa kujibu maswali ya msingi yaliyokuwepo kwenye mada.

Mkuu unasema tuanzie na rasimu ya Jaji Warioba na tuendelee mbele, hakuna haja ya kukusanya maoni mapya. Naamini hii ni ili kuokoa rasilimali muda na rasilimali fedha, au sio?

Kuhusu suala la kuitisha bunge la katiba, tena lenye wataalamu 80% unaweza pendekeza angalau watu 10 tu. Yaani majina kumi tu ya watu ambao unadhani wawemo kwenye bunge hilo?? Ukizungumzia wataalamu ambao hawana harufu ya kujihusisha na siasa ya chama flani je hapo upo realistic? Siasa ni maisha na kila mtu anajihusisha na siasa. Either unakubaliana na hoja za upande huu au upande ule.

Hebu fafanua zaidi mkuu.
 
Katiba nikurasmisha na kuapprove ya jaji warioba

Rasim ya jaji warioba ndio maoni stahiki na halisi ya wananchi.

Kuanza kupata vigugumizi nikupoteza muda nakuchelewesha mambo muhimu ya msingi kiutekelezaji
Inavyoonekana ni kwamba, watu wengi wanakubaliana na rasimu ya Jaji Warioba na inatosha kumfanya Mama aendelee kutokea pale.

Kama hivyo ndivyo basi ni kuunda tu bunge la katiba.

Unaweza ukatuambia chochote juu ya namna ambavyo ungependa muundo wa bunge hilo uwe??
 
Back
Top Bottom