Rais Samia na Familia yake Wachangia Milioni 100 Ujenzi wa kanisa la Mtakatifu Karoli jimbo kuu la katoliki Arusha

Huyu Mama uongozi wake umetoka kwa Mungu, haya ni maajabu katika nchi hii. Mungu ambariki sana
 
Wazanzibar unawajua au unawasikia? umewahi kuishi Zanzibar mkuu? mi naona anajitahidi sn maana wenzake ni balaa tupu na hovyo kabisa
Hili si suala la Wazanzibari tu.

Hiki ni suala la kuchanganya dini na siasa. Kuchanganya dini na siasa ni kitu kibaya sana.

Kwa nini rais anaona ulazima wa kuchangia ujenzi wa makanisa, jambo linaloleta sura ya kuingiza dini kwenye siasa, wakati kuna shule, hospitali na miradi kibao ya serikali ambayo anaweza kuchangia?

Hivi hamuoni kuwa hizi ni siasa za kujipendekeza kwa watu wa dini kabla ya uchaguzi?

Hamuoni kuwa hizi ni jitihada za kununua kura za watu ambao vinginevyo watamuona Samia hajawafanyia kitu?
 
Ifike mahali tutenganishe dini na siasa! Hii itafika siku Tanzania tukichagua rais asiye na dini. Sababu walio na dini hasa hizi mainstream hili la kutenganisha limewashinda. Ni rasilimali nyingi sana za nchi zinatumika kuwanufaisha wachache hasa wanaojifanya kufuata hizi dini 2 Tanzania
 
Yaani umeandika kwa mbwembwe na Madaha makubwa huku ukimsifia Bashite na raia namba moja kama vile wameumba dunia??
Acha hizo aiseee))

Kweli 100ml ni parefu ila punguza sifa ili Mungu awabariki waliotoa.
Mimi sijawasifia bali nimeongea ukweli
 
Ifike mahali tutenganishe dini na siasa! Hii itafika siku Tanzania tukichagua rais asiye na dini. Sababu walio na dini hasa hizi mainstream hili la kutenganisha limewashinda. Ni rasilimali nyingi sana za nchi zinatumika kuwanufaisha wachache hasa wanaojifanya kufuata hizi dini 2 Tanzania
Tuacheni chuki binafsi ndugu yangu.
 
Hatari sana, kwa nini watu wanajitia ujinga wa kutoelewa hili?
Watu wana washadadia wana siasa kwenye mambo yasiyo ya msingi sana pasipo kujali ustawi wa taifa. Bado tuna miundo mbinu mingi mibovu ambapo ingepelekwa hiyo hela ingeleta ahuweni kwenye jamii
 
Huna adabu kabisa wewe na makuzi na malezi yako inaonyesha ulikosa walau hata kupata maelezo ya mama yako mzazi. Hivi unaanzia wapi kumtukana Rais wetu kuwa ni mjinga? Huna akili kabisa na umekosa kabisa adabu wewe.
Kuwa mjinga siyo tusi, “ignorant” yaani “hajui”, kwa hiyo ni mjinga.

Twende nyuma. Rais mshahara Tshs: 35 million kwa mwezi. Anatoa msaada mmjoja 100 millioni! Yaani Tanzania ni nchi among 20 poorest in the world!!! Haaaaaaaa.
Hata Biden hana uwezo huo. Familia ya Biden juzi juzi tu last week wamedeclare mapato ya mwaka laki sita dollar na kulipa kodi. Huyu Rais wa nchi masikini kama hii anatoa wapi pesa zote hizi ?
 
Watu wana washadadia wana siasa kwenye mambo yasiyo ya msingi sana pasipo kujali ustawi wa taifa. Bado tuna miundo mbinu mingi mibovu ambapo ingepelekwa hiyo hela ingeleta ahuweni kwenye jamii
Mkuu,

Unafikiri watu wanashadadia hivyo kwa ujinga, kwamba genuinely hawaelewi ubaya wa kuchanganya dini na siasa, na ukielezea hilo wanakushangaa wewe kwa kutoelewa na kuuliza "wewe viipi?".

Au, wanashadadia hivyo kwa kuelewa fika, ila wanaendekeza uchawa tu kwa kusema wanataka wanasiasa wanaowapenda washinde chaguzi "by any means necessary", ikiwamo hata kutumia siasa makanisani?
 
Nilichojifunza uchawa ni mbaya sana. Miaka ya mbeleni hali ikiendelea hivi tutapata nchi ya hovyo sana mkuu
 
Akitoa milioni 100 mshahara tunaomlipa wa miezi 10 baada ya hapo anaishije . Huu udwanzi uko africa tuuu bara la giza tororo pfuuuu
 
Akitoa milioni 100 mshahara tunaomlipa wa miezi 10 baada ya hapo anaishije . Huu udwanzi uko africa tuuu bara la giza tororo pfuuuu
Kibaya zaidi, bajeti ya Ikulu haiko wazi, haifanyiwi auditing, haijulikani.

Kwa hivyo, hata akikwambia hizi ni pesa zake binafsi, utahakikishaje hilo ni kweli?
 
Akitoa milioni 100 mshahara tunaomlipa wa miezi 10 baada ya hapo anaishije . Huu udwanzi uko africa tuuu bara la giza tororo pfuuuu
Kutoa ni moyo na si utajiri.Mheshimiwa Rais wetu kipenzi anastahili pongezi sana kwa moyo wake wa kujitoa na kujitolea na kujali maisha ya watanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom