Rais Samia kumtoa Makonda kwenye Uenezi hasa kipindi hiki umefanya makosa makubwa

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
483
969
Wasalam mabibi na mababu..

Nikiwa katika Tafakari kubwa sana ni kipi kimemfanya Rais Samia kumtoa Makonda kwenye Uenezi na kumpeleka kama mkuu wa Mkoa wa Arusha! Japokuwa mitaa haiishii soga kuna wanaosema bwana mdogo anavimba, kuna wanaosema bwana mdogo ana bifu na GSM na maougomvi, kuna wanaosema kapelekwa kimkakati jimbo lisiende upinzani n.k.

Kimsingi bwana makonda ile nafasi alitosha na aliitendea haki sana, yaani alitengeneza attention nchi nzima na watu wakaitika, dogo alikuwa na ubunifu wake kila mkoa kuingia na mbwembwe zake, alijua kukiweka chama cha Mapinduzi Katika mamlaka yaani hadi anaweza mpigia Waziri atoe majibu fulani ile ni kuonyesha chama ni kikubwa kuliko mtu au nyadhifa.

Kiuhalisia nafasi ya uenezi haitaki mtu alie serious, inataka mtu ambae hana madhara, mtu wa kutoa pumba muda wote, mtu wa kuweka attention, mtu mwenye kukera wapinzani, mtu wa kujibizana na Mwenye mbwembwe za kuongea.

Katika kuelekea Uchaguzi serikali za mitaa mwaka huu na ule mkuu wa Mwakani 2025, Kumtoa huyu bwana mdogo naona Rais na CCM kwa ujumla wakiwa wamechanga vibaya karata zao, huyu dogo alikuwa ni asset kwa kipindi hiki,.

Ninachelea kusema kuwa Kampeni na mkutano ya kisiasa ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2025 haitakuwa na mvuto mana Chama hakina watu wenye mahoka wa kuleta attention, ukimuangalia katibu mkuu kapooza kama hayupo vile hana maajabu wala attention yoyote, na nikiwaza wa kucover hiyo nafas ambae atakuwa amejichetua simuoni kabisaa huko Chamani...

Chama kinahitaji mtu mwenye uongeaji kama mzee Makamba na sio pooza, Mapema sn tutakwenda kuwa kumbuka kina nape, pole pole...
 
The road to hell is paved with good intentions, he is satan trying to prove to us that he is an angel
 
Ninafikiri Mama amemstahi tu, lakini Makonda haendani na siasa za kistaarabu. Yaani yeye na Sabaya hawawezi kucheza beat za USTAARABU. Wao hutamani ubabe na kauli kali.
 
Back
Top Bottom