Rais Samia Katiba ya Tanzania sio ya Rais, wala CCM, wala Upinzani, ni ya Watanzania wote na huna mamlaka nayo. Kuapa kuilinda sivyo unavyofikiria

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,275
19,112
Nimeshangazwa sana na habari iliyopo kwamba Rais Samia alimuagiza Mkuu wa Polisi Mwanza kuzuia watu kufanya kongamano juu ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania; kwa malaka gani aliyo nayo Samia juu ya Katiba? Je Rais Samia haelewi kwamba japo ana mamlaka ya Uraisi wa Tanzania, uraisi wa Tanzania haumpi mamlaka au umiliki juu ya Katiba kwa kuwa Katiba ya ni ya kila mtanzania?

Na kama Katiba haina mmiliki anaewazidi umiliki Watanzania wengine, suala la Raisi Samia kuzuia watu kukutana na kujadili katiba yao, linatoka wapi? Je, Rais Samia inawezekana kwamba kutoa kiapo cha kuisimamia na kuilinda Katiba ya Tanzania anafikirri maana yake atailinda watu wasiijadili? Ikiwa ndivyo, basi kuna uhitaji wa haraka sana wa kumwelimisha Raisi Samia nini maana ya kuisimamia na kuilinda katiba ya Tanzania. Rais anapaswa kuelimishwa kwamba kuilinda Katiba ya Tanzania maana yake ni kuhakikisha Tanzania kama nchi inaendeshwa kulingana na misingi iliyo ndani ya Katiba, na pale inapoonekana kuna watu wanakiuka hiyo msingi basi anapaswa kuchuka hatua.

Kitendo cha Raisi Samia kuzuia watu kujadili katiba ambayo wana haki na umiliki nayo huko si kuilinda Katiba hata kidogo, na asije akadhani anailinda. Kwa kuwa kila mtu ana haki ya Katiba ya Tanzania, kila mtu ana haki ya kuijadili na mtu mwingine aliye tayari kuijadili pamoja nae, iwe ni watu wawili au maelfu, ili mradi katika kufanya hivyo hawavunji sheraia na wanafanya kwa amani na utulivu. Kitu ambacho hakitaruhusiwa ni mtu yeyote kulazimisha watu wengine waibadili Katiba kulingana na anavyotaka yeye. Lakini ikiwa atataka kuijadili Katiba akiwa na watu wengine kwa lengo la kupendekeza mabdailiko kupitia utaratibu unaokubalika wa kubadili Katiba, si Raisi wala Mkuu wa Polisi wa Mkoa, au hata waziri wa Katiba na Sheria ana mamlaka ya kumzuia huyo mtu.

Kwa hiyo basi, wito kwa Raisi Samia, usijmilikishe Katiba ya Tanzania, na usidhani kwamba kiapo ulichofanya cha kuilinda Katiba maana yake uwazuie wale wanaotaka kuiongelea wasiiongelee. Na pia unapaswa kuelewa wazi sana kwamba kuwa kwako Raisi wa Tanzania kupitia CCM hakuipi CCM mamalaka juu ya Katiba ya Tanzania kuzidi Chadema, au TLP au chama kingine chochote cha siasa. Vyama vyote vya siasa vina haki sawa juu ya Katiba kama vile tu ilivyo kwa Mtanzania moja mmoja.

Umiliki wako Raisi Samia wa Katiba ya Tanzania hauongezewi nguvu na wewe kuwa Raisi wa Tanzania, kwa kuwa una haki sawa juu ya umiliki wa Katiba na mtanzania mwingine yeyote. Tofauti ni kwamba wewe una mamlaka ya kuhakikisha mambo yanafanyika nchini kwa kufuata misingi ya Katiba. Kwa hiyo kama ambavyo mimi sina mamlaka ya kumzuia mtu kujadili Katiba na mtu mwingine, ndivyo na wewe hupaswi kuwa na mamlaka hayo, kwa kuwa mimi na wewe sio wamiliki wa hii Katiba kuliko Watanzania wenzetu.

Kwa hiyo Raisi Samia tafadhali usilete matatizo pale ambapo matatizo hayapo. Kama watu wameamua kujadili katiba ambayo kimsingi ni ya kwao waache wajadili kwa uhuru. Na kama watakuwa na jambo la kuwaambia Watanzania wengine ni kitu gani wamejadili na wanapendekeza nini, tutawasikiliza, na tunaweza kukubaliana na mawazo yao au kutokubaliana, kwa sababu wao hawana umiliki wa Katiba tofauti na sisi wengine ambao hatukuwapo kwenye mjadala wao, na wala haitulazimu kuwapo kwenye mjadala wao.
 
Katiba yenyewe inasemaje juu ya kubadilishwa kwake?

Katiba yenyewe inasemaje?

Isije kuwa kudai katiba sio takwa la kikatiba ?
 
Umiliki wa Katiba ya Tanzania ichukuliwe sawa na umiliki wa pamoja wa mali fulani kama nyumba katika mamlaka yaliyo sawa, bila kujali wewe ni mwenyekiti wa Mtaa au meneja wa kampuni mahali fulani.

Sasa tunapokuwa nyumbani ukaanza kusema sitaki watu humu ndani mjadiliane kuhusu labda kuipaka rangi nyumba ipendeze zaidi, sisi wamiliki wenzako wa nyumba tutaona kama unaingiliwa na wazimu fulani hivi.

Nani au kitu gani kinakupa mamlaka zaidi ya umiliki wa nyumba yetu zaidi ya sisi wengine hadi utuzuie kuongelea juu ya nyumba yetu ambayo tuna umiliki sawa, japo wewe ni mwenyekiti wa mtaa wetu?
 
Kama katiba ni ya Watanzania wote bc mimi kama mtanzania SITAKI KATIBA MPYA.
 
Nimeshangazwa sana na habari iliyopo kwamba Raisi Samia alimuagiza Mkuu wa Polisi Mwanza kuzuia watu kufanya kongamano juu ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania; kwa malaka gani aliyo nayo Samia juu ya Katiba? ...
The irony lady Mama Samia Suluhu Hasan.

aendelee kuupiga mwingi.
 
Katiba yenyewe inasemaje juu ya kubadilishwa kwake ?

Katiba yenyewe inasemaje ?

Isije kuwa kudai katiba sio takwa la kikatiba ?
Unajua hata kudaai Katiba sio suala la Kikatiba. Unadai Katiba kwa nani? Nani amejipa mamlaka ya kwamba yeye watu wanapotaka Katiba mpya basi waidai kwakwe? Soma Katiba, kuna mtu kapewa mamlaka ya kupokea madai ya Katiba mpya?

Kimsingi, Rais Samia anachoweza kufanya ni kusema, jamani eeh, kama suala la katiba mpya ni jambo la wengi, basi tufanye referandum tuone kama ni kweli watu wanataka Katiba mpya. Basi referandamu itafanywa, na ikionekana ni wachache wanaodai Katiba mpya, basi Raisi Samia atakuwa na haki na mamlaka ya kusema hili suala sasa tumelimaliza limekwisha. Na ikionekana ni wengi wanataka Katiba mpya, si uraisi wake wala u CCM wake unapaswa kuzuia hilo.

Lakini Raisi Samia hana kabisa mamlaka ya kusema mie Katiba mpya sio ajenda yangu. Who are you kusema sio ajenda yako, kwani hii ni Katiba yako au ya Chama chako? Ikiwa watu wanasema tunataka Katiba mpya ni wajibu wako kama msimamizi wa uongozi nchi ku-facilitate hilo au kufanya uhakiki kama ni dai la wengi kupitia referendum. Sio kujipa umiliki na mamlaka juu Katiba vitu ambavyo huna na hupaswi kudhani unavyo.
 
Unajua hata kudaai Katiba sio suala la Kikatiba. Unadai Katiba kwa nani? Nani amejipa mamlaka ya kwamba yeye watu wanapotaka Katiba mpya basi waidai kwakwe? Soma Katiba, kuna mtu kapewa mamlaka ya kupokea madai ya Katiba mpya?...
Katiba ya sasa inasemaje juu ya kudai katiba mpya?
 
Watanzania wanataka maendeleo ili waishi vizuri.

Wana siasa hasa upinzani wanataka katiba mpya ili washike dola.
Ikiwa Katiba iliyoo ndio inawazuia Watanzania kupata maendeleo, na wapinzani kushika dola, basi tuna Katiba yenye matatizo makubwa sana, na tutakuwa wapumbavu sana kuendelea kuikumbatia na kuitumia Katiba ya namna hiyo.

Sio dhambi Watanzania kupata maendeleo, na sio dhambi wapinzani kushika dola. Sasa je, tuna Katiba inayofanya Watanzania kupata maendeleo na wapinzani kushika dola kuwa dhambi?
 
Kama katiba ni ya Watanzania wote bc mimi kama mtanzania SITAKI KATIBA MPYA.
Sawa kabisa, una haki hiyo. Sasa vipi yule Mtanzania ambaye anataka katiba mpya, tunafikiaje suluhu kati ya nyie wawili kwa amani na utulivu? Hatuwezi kumpuuza yeye kwa ajili yako wewe, na hatupaswi kukupuuza wewe kwa ajili yake.
 
Umiliki wa Katiba ya Tanzania ichukuliwe sawa na umiliki wa pamoja wa mali fulani kama nyumba katika mamlaka yaliyo sawa, bila kujali wewe ni mwenyekiti wa Mtaa au meneja wa kampuni mahali fulani. Sasa tunapokuwa nyumbani ukaazna kusema sitaki watu humu ndani mjadiliane kuhusu labda kuipaka rangi nyumba iendeze zaidi, sisi wamiliki wenzako wa nyumba tutaona kama unaingiliwa na wazimu fulani hivi. Nani au kitu gani kinakupa mamlaka zaidi ya umiliki wa nyumba yetu zaidi ya sisi wengine hadi utuzuie kuongelea juu ya nyumba yetu ambayo tuna umiliki sawa, japo wewe ni mwenyekiti wa mtaa wetu?
Umeandika kitu kizuri sana ila watu wameleta masihara.
 
Sasa je, tuna Katiba inayofanya Watanzania kupata maendeleo na wapinzani kushika dola kuwa dhambi?
Kama lengo ni wao kushika dola hatukatai lakini wasiwalishe sumu raia waingie mtaani.

Waingie waandamane wenyewe kwa sababu wakipata dola watakula bata wao huku wananchi wakibaki vile vile.

Hilo ndio lengo,hakuna siku utaskia wanasema wananchi waandamane kwa sababu kijiji fulani hakuna maji n.k

Wao wanataka wananchi wawatume katika mambo yatakayowanufaisha wao.

Sijakataa wao kudai katiba,lakini waidai katiba wao kwa wao ambao wana maslahi nayo.

Kuhusu maendeleo tatizo sio katiba,tatizo ni watu.

Katiba hii iliyopo imezuia jambo gani la maendeleo kufanyika ambalo watu wakiamua wavunje kifungu hiko basi wakashindwa ?
 
Nadhani tumeanza kuelewana. Nasikia watu wote waliokamatwa Mwanza wameachiwa huru. Lakini pia huyu RPC afunguliwe mashitaka. Atajitetea huko Mahakamani kwamba alipewa maagizo.
 
Back
Top Bottom