ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,991
- 51,833
Rais Samia ameagiza kuanza kuondolewa Kwa Matrafiki ambao walijigeuza Wala Rushwa Barabarani badala yake ametaka zifungwe Kamera na Taa Ili Kuongoza magari.
---
Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kukabiliana na rushwa nchini, trafiki barabarani wanapaswa kuondolewa badala yake taa na kamera zitatumika kuongoza barabarani.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapisha viongozi wateule wa ngazi mbalimbali za uongozi nchini
“Usalama barabarani, tunataka kuondoa trafiki barabarani kukomesha rushwa. Tuyaache mambo ya pita wewe nenda wewe”
My Take
Naunga mkono hoja ya Mh.Rais.
Trafiki waligeuza usalama Barabarani kuwa mradi wa kuvuna pesa za Rushwa Kwa maderva huku ajali na makosa mengine yakizidi kuongezeka.
Kenya wameweza na sisi tuanze maana tulichepewa sana.
Tukitoka hapo tufungue kamela kwenye Mahospitali na kuwavalisha kamela maafisa wa TRA.