Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,727
- 29,970
Amani iwe kwako mkuu wangu wa nchi.
Nimeweka heading hiyo kuweza kukuvutia kusoma usuli wa hoja yangu.
Sote tunafahamu kwa Mujibu wa Katiba kuwa tasisi unayoiongoza imepewa mamlaka ya kuunda, kupangua ama kufuta wizara mbalimbali za serikali hasa kutokana na mahitaji ya nchi kwa wakati husika.
Umeunda wizara mahususi ya kushughulika na hitaji kubwa la ustawi na maendeleo ya kisekta kwa kulenga jamii hususan makundi yaliyo kwenye wskati mgumu kijamii ambayo ni wanawake, watoto na wenye ulemavu. Naongekea wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum. Nimeweka hapa chini screenshot ya banner la wizara lililopo kwenye interface ya tovuti ya wizara
UKAKASI
Nimetafakari jina la Wizara ni kama linaleta ukakasi zaidi kwa muktadha wake.
Je neno JINSIA lilimaanisha nini ama aina gani ya jinsia zilizopo ndani ya neno hilo? Nimeona Jinsia imetajwa kisha mbeleni naona Wanawake wanatajwa nje ya jinsia. Ingesomeka wanaume badala ya jinsia ili kubeba mantiki ya neno wanawake mbeleni hapo.
Neno lingine ni makundi maalumu. Ambapo sisi raia wako tunaamini makundi maalumu ni wanawake, watoto na wenye ulemavu. Najiuliza kama jinsia lipo, wanawake wapo hapo kwenye makundi maalumu tunamaanisha makundi gani?
USHAURI
Nikiulizwa kuwa napendekeza jina lisomekaje nitajibu Jina la Wizara litapendeza likisomeka WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WATOTO NA WENYE ULEMAVU.
Nimetoa hoja