Rais ajaye baada ya Putin atalazimishwa kulipa hasara iliyosababishwa Ukraine

Conwel Ngani

Senior Member
Sep 16, 2018
134
149
Lengo la Mmarekani na washirika wake Nato ni kuhakikisha Urusi inafilisika kiuchumi. Na ili hilo lifanikiwe wanataka vita iendelee kwa muda mrefu ili Urusi idhoofike ndio maana tunaona hayo yanayoendelea.

Wengi tulidhani Ulaya ingeufyata kutokana na vikwazo wanavyowekewa na Urusi ila badala yake imewachochoea zaidi kuendelea kuisaida Ukraine.

Hawa jamaa sio wajinga, hii inaitwa calculated risk, wanaona bora waumie sasa ila kwa manufaa ya kudumu ya badae. Na mwisho wa siku hata rais ajaye wa Urusi si ajabu akalazimishwa kulipa hii hasara ya uvamizi ili kuondolewa vikwazo.
 
Hela ya Russia imejaa kwenye mataifa ya magharibi na bunge la Marekani tayari limeshaidhinisha kwamba itumiwe ktk kuijenga upya Ukraine ni zaidi ya US$ bilioni 400.

Hata hizi fedha ambazo Marekani wanapitisha mara kwa mara kuisaidia Ukraine utakuta ni zile zile ya Russia.
 
Mimi nilesema hicho kitu wapenzi wa Putin walinishambulia sana.Kitakochotokea ni kuwa Urusi ili irudi kwenye system ya dunia (SWIFT) na vikwazo vingine vingi walivyowekewa ikiwemo ndege zao kutokutua US ,EU countries na baadhi ya nchi za Asia na Latin America amabako ni Hasara kubwa kwa mrusi kwani uchumi wa urusi umeshuka kwa asilimia 4 na kwa taifa kubwa kama Urusi sio jambo la kitoto.

So Fedha zao zilizopo kwenye mabenki washirika wa marekani na ulaya hawatapewa badala yake wataambiwa wakubali hizo fedha ziende Ukraine. Kama unafuatilia waziri wa fedha wa Ukraine kila wiki anatoa figure ya hasara ya vita hii.ni mahususi kuanza kuangalia account nono za Urusi zolizopo nje
 
Mimi nilesema hicho kitu wapenzi wa Putin walinishambulia sana.Kitakochotokea ni kuwa Urusi ili irudi kwenye system ya dunia (SWIFT) na vikwazo vingine vingi walivyowekewa ikiwemo ndege zao kutokutua US ,EU countries na baadhi ya nchi za Asia na Latin America amabako ni Hasara kubwa kwa mrusi kwani uchumi wa urusi umeshuka kwa asilimia 4 na kwa taifa kubwa kama Urusi sio jambo la kitoto.So Fedha zao zilizopo kwenye mabenki washirika wa marekani na ulaya hawatapewa badala yake wataambiwa wakubali hizo fedha ziende Ukraine. Kama unafuatilia waziri wa fedha wa Ukraine kila wiki anatoa figure ya hasara ya vita hii.ni mahususi kuanza kuangalia account nono za Urusi zolizopo nje
Good
 
Back
Top Bottom