Protokali ya Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu ipoje?

Amiri Jamal alizaliwa na wazazi wa Ki Gujarati au unaweza ukasema Wahindi wa Asili au wahindi mama yake aliitwa Kulsum Thawer na baba yake Habib Jamal, ambaye ndo mwanzilishi wa Asian Association..

Sasa kuhusu Yeye kuwa Waziri Mkuu nimetoa ufafanuzi Rudia kusoma Taratibu hiyo Post nimesema miaka kadhaa alikuwa waziri Mchangia au waziri asiye na wizara maalumu Hicho cheo kilikuwa ni sawa na waziri Mkuu..

Sijui hata unajua Neno Mtanzania ni kina nani?
Amiri Jamal hakuwa Mtanzania alikuwa i Muhindi hata alipofariki hakufanyiwa huduma hapa hana ndugu hata mmoja hapa..
Hadhi ya waziri asiye na wizara maalum haijawahi kuwa sawa na ya Waziri Mkuu...Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwepo kikatiba tangu Tanganyika iwe Jamhuri...Na kwa kipindi chote ambacho Jamal alihudumu kwenye baraza la mawaziri, Waziri Mkuu alikuwa pia ndiye Makamu wa Pili wa Rais..Hivyo, kwa vyovyote usingeweza kusema kwamba Waziri asiye na wizara maalum ni sawa na waziri mkuu....

Kuhusu Jamal kutofanyiwa taratibu za mazishi Tanzania...hiyo peke yake haiondoi fact kwamba alikua ni Mtanzania.......Je tunaweza kusema late Daudi Balali-former BoT Governor-hakuwa Mtanzania kwa sababu tu hakuzikwa TZ?
 
Kwani Balali Alikufa Mkuu?
Unaweza kuonyesha Kabuli lake?

Umesema ofisi ya waziri Mkuu imekuwepo kikatiba Tangu Tanganyika Iwe Jamhuri..
Katiba ipi kati ya hizi hapa chini?
Je unajua majukumu ya Waziri Asiye na wizara maalumu kwa katiba zote?

  1. KATIBA YA UHURU YA MWAKA 1961
  2. KATIBA YA JAMHURI YA MWAKA 1962
  3. KATIBA YA TANZANIA YA 1964 - KATIBA YA MUUNGANO
  4. KATIBA YA MUDA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1965
Au ni ya siku hizi
  • KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977
Je unajua majukumu ya Waziri asiye na wizara maalumu kwa Katiba Zote hizo?

kumbuka cheo hicho kilifutwa na katiba ya Jamhuri ya muungani ya mwana 1977
 
Jiwe alizungushwa majiji yote ndipo akazikwa, walifupisha kwa kuwa aliua watu, alipora mali za watu, aliteka watu na kupiga watu risasi.

Sasa kwa huyu waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa kwa kuwa alikuwa mtu wa watu atazungushwa mikoa yote na wilaya zote ndipo azikwe.

RIP Edo
We kinyezi kabiza
 
Sikuwa na haja ya kumuandika Nyerere kwa sababu kipindi anakuwa Waziri Mkuu Tanganyika haikuwa Jamhuri ilkuwa ni Jimbo la Uingerez
Baada ya siku 45 alijiuzuru ili kuifanya nchi Jamhuri, waziri mkuu akawa Rashid Kawawa, then baada ya Vita 1979 akapewa Edward Sokoine, kisha akapewa Dr. Salim Ahmed Salim, then Cleopa David Msuya, Kisha Joseph Sinde Warioba, John Samuel Malechela, Fredrick Tulway Sumaye, Kisha Edward Lowasa, Mizengo Kayanza Pinda na sasa Majaliwa Khasim Majaliwa
 
Hapana. Wakati wa utawala wa Kikwete Nadhani Mhandisi Mark Mwandosya aliwahi kuwa waziri asiye na wizara maalum kwaiyo tuseme naye alikuwa waziri mkuu?
Tofauti ya Mark mwandosya na Amir ni katiba iliyokuwa Inawaongoza kuhusu Majukumu Yao..
Katiba ya jamhuri ya Tanganyika 1962,Katiba ya Muda ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964 ni tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977..
Imerekebishwa sanaa
 
Baada ya siku 45 alijiuzuru ili kuifanya nchi Jamhuri, waziri mkuu akawa Rashid Kawawa, then baada ya Vita 1979 akapewa Edward Sokoine, kisha akapewa Dr. Salim Ahmed Salim, then Cleopa David Msuya, Kisha Joseph Sinde Warioba, John Samuel Malechela, Fredrick Tulway Sumaye, Kisha Edward Lowasa, Mizengo Kayanza Pinda na sasa Majaliwa Khasim Majaliwa
Kosa ni moja Tu uliposema Kujiuzuru Kujiuzuru kwa waziri Mkuu wa Tanganyika hakukufanya Tanganyika kuwa Jamhuri ila Bunge la Tanganyika lilipitisha katiba ya mwaka 1962 (Katiba ya Jamhuri) iliyofanya Tanganyika kutoka kwenye katika ya mwaka 1961 iliyokuwa inaitwa katiba ya uhuru..
katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962 ndo ilifanya mabiresho kama Mawaziri kuwajibika kwa Rais moja kwa moja hapo awali walikuwa wakiwajibika kwa Bunge la Tanganyika na bunge lilikuwa likiwajibika Chini ya Malkia wa Uingereza..

Katiba ya 1962 iliitwa Katiba ya Jamhuri.
Kwa bahati mbaya utengenezaji wake haukuhusisha wananchi wa kawaida. Ushiriki ulibaki mikononi mwa wabunge 71 wa TANU ambao walijigeuza na kuwa bunge maalum la Katiba lililopitisha Katiba hii.

Katiba ya 1962 ndiyo ilianzisha mfumo wa Urais wa kifalme ambaye pia alikuwa Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa serikali.

Baraza la Mawaziri na waziri mmojammoja sasa waliwajibika kwa Rais badala ya bunge kama ilivyokuwa katiba ya 1961.

Katiba hii iliweka Rais mwenye madaraka na mamlaka makubwa sana..

Waki huo kama utakumbuka Katiba ya 1961..
Au katiba ya uhuru ..

Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1961 ilitokana na azimio la sheria ya uhuru (Order in Council) lililopitishwa katika bunge la Uingereza na kuletwa Tanganyika kama Katiba ya awali.

Katiba hii iliitwa Katiba ya uhuru ambayo ilitengenezwa na waingereza nchini Uingereza na kuletwa kwetu.
Mapungufu yake makuu ni kwamba haikuwa na haki za binadamu. Mambo mengi bado yalitegemea kufanyiwa maamuzi toka Uingereza chini ya Malkia ambaye aliendelea kuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika mpaka mwaka 1962.

Katiba hii pia ilianzisha kanuni ya uwajibikaji wa pamoja wa Baraza la mawaziri na waziri mmojammoja alikuwa anawajibika kwa bunge. Pia, Katiba hii ilianzisha msingi wa uhuru wa mahakama.

Nafikiri kwa kifupi umejua kwanini nakwambia sio tu Nyerere Hakuwahi kujiuzuri Bali hakukuwa na haja ya Kujiuzuru sijui kama unajua maana ya kujiuzuru?
Ila kulikuwa na mabadiliko ya katiba yaliyochange mfumo mzima kutoka nchi iliyo chinu ya Ufalme (Malkia) mpaka Jamhuri..

Ila kwa mpangilio.umetaja vizuri sana
 
1. Miaka zaidi ya 60 toka tupate Uhuru sijawahi kushuhudia Mazishi ya Waziri Mkuu (Mstaafu) Narudia WAZIRI MKUU (Mstaafu) usinitajie Sokoine.

2. Nimeshuhudia mazishi ya Rais, Rais Mstaafu na Makamu wa Rais (Mstaafu). Mwenye kujua taratibu zake zipoje?

3. Je Ile sheria ya Viongozi kuzikwa Dodoma ilipita Bungeni?
Wewe na bunge lako la Buza ndiye utuambie kama mliipitisha, sisi hatuwezi kujua
 
Si kweli. Yeye hutumwa na raisi kwa utashi wa huyo raisi. Hivi karibuni nafikiri mzee mkuchika ana cheo kama hiko. Check
Tofautisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu ) na waziri Asiye kuwa na Wizara maalumu..
ni Viwili tofauti tena mbali sana..

Kidogo ungemtaja Labda Mark mwandosya anaweza kulingana wizara japo Amir wizara yake Haikuwa Chini ya Ofisi ya Rais au waziri wa Nchi ofisi ya Rais..
lakini kingine katiba iliyokuwa Inawaongoza kuhusu Majukumu Yao Ziko tofauti pia..

Katiba ya jamhuri ya Tanganyika 1962,Katiba ya Muda ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964 ni tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977..

Imerekebishwa sanaa
 
Tofautisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu ) na waziri Asiye kuwa na Wizara maalumu..
ni Viwili tofauti tena mbali sana..

Kidogo ungemtaja Labda Mark mwandosya anaweza kulingana wizara japo Amir wizara yake Haikuwa Chini ya Ofisi ya Rais au waziri wa Nchi ofisi ya Rais..
lakini kingine katiba iliyokuwa Inawaongoza kuhusu Majukumu Yao Ziko tofauti pia..

Katiba ya jamhuri ya Tanganyika 1962,Katiba ya Muda ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964 ni tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977..

Imerekebishwa sanaa
Kazi maalum na asiyekuwa na wizara maalum ni sawa tu. Waziri una wizara au huna mengine ni mbwembwe tu. Kaka yangu mkuchika hana wizara.
 
Kazi maalum na asiyekuwa na wizara maalum ni sawa tu. Waziri una wizara au huna mengine ni mbwembwe tu. Kaka yangu mkuchika hana wizara.
Hana wizara Ila mema ya nchi anakula eg posho, usafir, nyumba, matibabu, connection/deals.
 
1. Miaka zaidi ya 60 toka tupate Uhuru sijawahi kushuhudia Mazishi ya Waziri Mkuu (Mstaafu) Narudia WAZIRI MKUU (Mstaafu) usinitajie Sokoine.

2. Nimeshuhudia mazishi ya Rais, Rais Mstaafu na Makamu wa Rais (Mstaafu). Mwenye kujua taratibu zake zipoje?

3. Je Ile sheria ya Viongozi kuzikwa Dodoma ilipita Bungeni?
Huna kumbukumbu Kama panzi. Tulipomzika Kawawa ulikua umelewa?
 
Back
Top Bottom