Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,489
- 40,018
Sipendi shindana na wewe kwa vile hata kama nilifanya kitu kidogo sana bado nitakushinda
hujafanya kitu kwa sababu huna uwezo huo; badala ya na wewe kuwa sehemu kweli ya mabadiliko kupigana na ufisadi kiukweli umebakia kudhania watu ni maajenti. Ni uongo huu ambao umepandikizwa na wale ambao wanajua tumeshawashinda na tunaendelea kuwashinda - mafisadi. Katika hili hakuna mswalia mtume; wale ambao wanataka kuja kututawala tutawasimamia na kuwapima kabla hawajaja kututawala. Hatutawapa blank check kama unavyofanya wewe. Tunavyowabana watawala wa sasa walioshindwa ndivyo ambavyo tutawabana watawala wanaokuja. Hatuamini katika haki ya watu kututawala kama unavyoamini wewe.
Kwamba CDM kisihojiwe, kiachwe na kisiulizwe. Unataka watu wakikubalie chama kwa sababu tu kinaonekana kubeba matarajio na matumaini yao. Hili linaweza kuwavutia wengine wenye mtazamo wa kishabiki na wenye fikra zilizo dhaifu kama za kwako. Kwamba, chama cha siasa kinachota kuja kuiondoa CCM madarakani hakitakiwi kuulizwa, hakitiwi kupingwa, hakitakiwi kukosolewa au kuoneshwa udhaifu wake. Sidhani kama huku ni kukitakia mema.
Nadhani, unachofanya ni kuitakia CDM mabaya; hutaki ijipime, ijiangalie na kukosolewa ili ijijenge vizuri kulekea 2015. Unatak iende ikiwa katika udhaifu ambao tumeiona mara kwa mara. Wakati wengine tumekuwa katika vita hii dhidi ya ufisadi na tumeshashinda mara kadhaa na tunaendelea kushinda unakuja kama wewe usiye fanya lolote, usiyesaidia chama kwa lolote zaidi ya kutetea tu ili utetee na badala yake unataka kishindwe ili uwe wa kwanza kutaka kijipange tena 2020.
Sera za watu kama wewe zimeshindwa, mitazamo yenu imeshindwa, mikakati yenu imeumbuliwa na inaendelea kuumbuliwa na kufunuliwa kuwa ni dhaifu. Ni mikakati ya watu wasioona mbali. Mnataka CDM ishinde lakini ishinde kama kwa zawadi badala ya kupambana na kujipanga kweli kupambana. Baada ya kukusoma kwa muda mrefu na kukupima nimejiridhisha tu huna nafasi (kama hutobadilika) ya kuwa katika mwamko wa mabadiliko ambao tumeuasisi na kuutetea kwa gharama kubwa kuliko unavyoweza hata kuota kwenye njozi zako usiku. Wimbo wa kutaka CDM isijipange kabla ya 2015 tena mapema zaidi ni wimbo usio na kibwagizo; ridhim yake inakera.
Yeyote anayeitakia CDM mema; yeyote anayetaka CDM ishinde na siyo kushinda kirahisi tu bali kushika dola 2015 anapaswa na anatakiwa kuisimamia CDM kwa karibu zaidi, kuibana, kuilazimisha na hata kuisukuma itoke katika usingizi wa sifa ili iweze kujipanga upya na kiukweli. Katika kufanya hivyo wewee huwezi; huamini kuwa CDM inahitaji mabadiliko ili ishinde. Na hili ni ni tamanio la wana CCM wote kama wewe. Watu wote ambao hawataki mabadiliko ya kweli 2015 wanataka CDM iwe hivi hivi; ili ijikute kwenye migogoro ya kijinga, ili iweze kudhoofishwa.
Wachache wetu tumedhamiria kabisa kuwa kama CDM inataka kuja kuwa chama tawala basi itapita kwenye tanuru ya moto; itassafishwa, itajipanga na tutafanya yote yaliyo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha kuwa chama hiki ambacho kimechota fikra za Watanzania kinajipa utayari wa kuja kuwaongoza. Natumaini utakuja upande huu na wewe utasimama na wale wanaotaka mabadiliko ya kweli, na utakuwa tayari kukisaidia chama hiki kushinda uchaguzi mkuu ujao na ule wa serikali za mitaa.
The end.