Profesa Kabudi awasha moto Katiba Mpya

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amejibu baadhi ya hoja za watu wanaopendekeza muundo wa serikali mbili na kusema Serikali ya Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka serikali tatu mwaka 1984."

Aidha, amewashangaa wanaolibeza jina la Tanganyika kutumika serikalini kwa madai kuwa jina hilo siyo haramu kwa kuwa limo ndani ya Katiba ya sasa.

Alisema kuwa wakati huo madai ya serikali tatu yalitolewa na Zanzibar na kusimamiwa na Rais aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.

"Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea kwa sauti nzito, kama ulikuwa ukimsikiliza, unasema muungano haupo," alisema Profesa Kabudi na kueleza kuwa Fakhi alisema: "Zanzibar siyo koloni la Tanganyika."

Alikuwa akichangia hotuba katika Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika mjini Zanzibar jana. Alieleza kwamba mjadala wa sasa wa muungano siyo mkali kama uliokuwepo mwaka 1983 na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla mzungumzaji kumaliza hotuba yake.

Katika maelezo yake, Profesa Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei kama mtu baki, bali aliagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

"Lugha ilikuwa ni kali," alisema.

Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
"Unawezekana kuwa muungano unatunyima fursa moja ua mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao, lakini wahakikishe wanawahudumia wananchi," alisema.

Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu ya Katiba Mpya.

Kikwete pamoja na wajumbe hao kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba haionyeshi uhalisia wa matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu muundo wa muungano.

Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.

"Unaweza kuwa muungano unatunyima fursa moja au mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao lakini wanahakikisha wanawahudumia wananchi," alisema.

Akifafanua matumizi ya jina la Tanganyika kwenye Katiba ya sasa, Profesa Kabudi alisema: "Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya nne, 34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya masuala ya muungano na mamlaka ya masuala yasiyo ya muungano katika upande wa Tanzania Bara (Tanganyika)."

Alibainisha: "Nataka niwaambie, leo ukienda kwenye Ibara ya 151 ya Katiba, Tanzania Bara imetajwa kuwa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo Tanganyika siyo jina haramu."

Alisema anaamini kila taifa lina ujinga wake katika kutunga Katiba, lakini ujinga wa kizazi kimoja hauwezi kuwa wa kizazi kingine.
"Ujinga wa kizazi hiki, tusidhani utakuwa ujinga wa kizazi cha kesho, vizazi vijavyo vya Tanzania vitakuwa na ujinga wake."

Alifafanua: "Ni vyema kuwawekea misingi lakini waje kuishi na ujinga wao, kuliko kulazimisha ujinga wako, kwa sababu wewe ujinga wako ndiyo amali yako lakini kwa wengine siyo amali. Ulitegemea Waingereza wangekapigia mizinga kachanga ka siku moja?"

Hati ya Muungano

Akizungumzia hati ya muungano iliyozua sintofahamu hivi karibuni kwa madai kwamba haikuwepo, alisema msingi wa kikatiba na kisheria wa muungano wowote ni hati za muungano.

Alisema miaka ya 1980, suala lililokuwa linajadiliwa ni iwapo hati za muungano ni sehemu ya sheria za kimataifa au la. Baadaye ilibainika kuwa hati hizo ni mkataba wa kimataifa na kwamba unatawaliwa na sheria za kimataifa.

"Hili suala la kwamba hati zipo au hazipo siyo suala kubwa, suala ziliridhiwa? Ushahidi upo upande wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa upande wa Zanzibar kuna utata na hiyo kesi ipo mahakamani," alisema.

Alisema kutokana na utata huo katika Rasimu, wakapendekeza namna ya kutatua tatizo lililodumu kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa hati ya maridhiano ya Tanganyika na Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Unless una akili fupi kama za jk na lukuvi however otherwise lazima tupate nchi yetu ya Tanganyika..
 
Ningekuwa na uwezo wa kumshauri mwalimu wangu, dean wangu, na super visor wangu wa LL.B dissertation yangu, Prof. Palamagamba Kabudi, ningemshauri, aizamishe hii sense ya Tanganyika ndani ya vichwa vya CCM!. Hili ni suala tuu la kuwapatia elimu CCM, waelimike, waachane na ujinga wao wanaotaka kuulazimisha kwenye bunge maalum!.

Asante Prof. Kabudi, kulizungumzia hili.

Thanks.

Pascal.
 
Ningekuwa na uwezo wa kumshauri mwalimu wangu, dean wangu, na super visor wangu wa LL.B dissertation yangu, Prof. Palamagamba Kabudi, ningemshauri, aizamishe hii sense ya Tanganyika ndani ya vichwa vya CCM!. Hili ni suala tuu la kuwapatia elimu CCM, waelimike, waachane na ujinga wao wanaotaka kuulazimisha kwenye bunge maalum!.

Asante Prof. Kabudi, kulizungumzia hili.

Thanks.

Pascal.
Pascal Mayalla, inasikitisha sana kuona hawa watawala wetu wakiikana Tanganyika ambayo pia ipo ndani ya KATIBA, na vilevile ni vigumu kuitamka Zanzibar bila kuitambua Tanganyika. Sijui wamelishana yamini gani kujiaminisha kitu ambacho hakipo na hakiwezekani.
 
Last edited by a moderator:
Wanahitaji ushauli juu ya tanganyika,maana hapo kuna zanzibar + tanganyika =TANZANIA hapo hapo eti wanahitaj serkar 2,zip ss
 
Prof Kabundi yuko vzr, ila angali usije ukawa kama prof shivuji mwazo alikubali muundo wa serikali 3 kwa maandishi
yake ya vitabu leo anasema eti mbili ndio mwarobaini wa muungano huu. kigeugeu
 
Tunawasomi wazuri mnoo tz ila wanashawishika they face conflict of interest simameni wasomi muokoe nchi hii ndo mda huu wakutusaidia wanyonge
 
Nilimsikiliza jana Prof.Kabudi,huyu ni mwalimu wangu ninamuheshimu sana.
Jana ametoa somo kubwa sana...akawajibu wale wanaotaka kueneza propaganda kuwa Tundu Lissu kamtukana Mwalimu Nyerere....lakin Kabudi katuonyesha kuwa,bado Lissu alitumia Lugha laini sana,kumbe huko nyuma kuna watu walioifananisha Tanganyika ya Nyerere na Wakoloni,na wakasema ”hatutaki kuwa koloni la Tanganyika“
Na kwamba ”ujinga” wa kizazi cha Mwalimu Nyerere na Karume hauwezi kuwa wa kwetu...ukiwa na akili timamu atamuelewa Tundu Lissu,lkn kwa kumsikiliza Hamphley Polepole na Prof.Kabuti nimapata picha kwanini CCM walikataa wajumbe wa Tume ya Katiba wasiwe sehemu ya Bunge la Katiba.
Aibu ni pale TBC walipozima matangazo wakati Prof.Kabuti akichanachana hoja ya S2 ya Ma-CCM,
 
Lissu hakumtukana wala kumdharirisha mtu CCM tuache kumtumia Mwalimu kama kinga ya kujihami, yeye alikuwa nani hadi asikosee? Kama alikuwa Mungu sawa kama hata Lucifer alikuwa malaika na akakosea iweje Mwalimu? Acheni kuburuza watu mda huo haupo sasa watu wako macho subirini walale ndo muwaburuze
 
Magamba yakiachiwa huu uundwaji wa katiba mpya utaona Shivj anakuwa waziri au mku wa mkoa, amenweshwa smu tayari na wala hana nguvu ya kupinga uchawi wa CCM
 
This time sujui ccm na usalama wao wa taifa watamng'oa meno na kucha nani kwa maana kila kona ya nchi mambo yamebana ba watu wanataka Tanganyika na Zanzibar yao...
 
Back
Top Bottom