UZUSHI Polisi nchini Kenya yapiga marufuku Maandano ya kupinga kuondolewa kwa wamasai wa Loliondo

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
20221027_174150.png
 
Tunachokijua
Taarifa iliyoonekana kama ni taarifa ya polisi wa Kenya kuhusu kuzuia maandamano yaliyopanga kupinga maandamano ya Wakenya dhidi ya yaliyokuwa yanafanyika Ngorongoro Tanzania, haina uthibitisho kuwa imetoka kwa polisi.

Wamasai waliokuwa wanaishi ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro walikuwa wanahamisha ili hifadhi hiyo isiingiliane na watu Wakenya walisemekana kutaka kuandamana kwenda ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kupinga nguvu inayotumika kuwahamisha wamaasai waliokuwa katika hifadhi hiyo.

Taarifa inayoonekana kuwa ni ya polisi inaonekana kuwa imetengenezwa na polisi wa Kenya hawajathibitisha kuzuia maandamano hayo.

Pamoja na JamiiCheck ya JamiiForums, sehemu zingine zilizowahi kuthibitisha kuwa barua hiyo haikuwa sahihi ni gazeti la The Star na PesaCheck.

Pia, Jamii Check imebaini kuwa Augustine Nthumbi aliyetia saini barua hii sio Kamanda wa Polisi wa Nairobi kama inavyodaiwa. Kwa mujibi wa tovuti ya Kenyans.co.ke, Nthumbi aliondolewa kwenye wadhifa huo Januari 30, 2022.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom