Petition ya "BUNGE LIVE NOW"

Status
Not open for further replies.

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Ndugu Wananchi,

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-1, inatamka ifuatavyo:

Uhuru wa Mawazo

18.- (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.​

Kwa mtazamo huu, tunavyoadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari duniani, kwamba uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta matangazo ya moja-kwa-moja ya vikao rasmi vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na, badala yake, kutayarisha kipindi ambacho kimehaririwa, ambacho kinahaririwa na kurushwa baadae kwenye kituo cha luninga cha TBC1, ni dhahiri kwamba Serikali IMEVUNJA KATIBA!

Kwa mujibu wa Katiba, Serikali inapata mamlaka ya kutawala nchi kama ifuatavyo:

8.- (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.​

Bila KUMUNG’UNYA MANENO, ni dhahiri kwamba Serikali imekiuka Katiba kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 9 na Ibara ya 18. SISI RAIA WA TANZANIA hatukuingia mkataba na Serikali ili ivunje haki zetu. Serikali inatudhulumu kwa kufanya maamuzi ambayo yake nje ya mamlaka yake; haina mamlaka ya kufanya uamuzi unaoingilia haki zetu za Kikatiba BILA KUTUSHIRIKISHA. Inaminya haki zetu, hususan haki ya “kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii” kama ilivyoainishwa na Ibara ya 18.

Sasa umefika wakati – ambapo tumechelewa sana – wa sisi raia ambao ndio MSINGI WA MAMLAKA YOTE kuiwajibisha Serikali, kwa kuwa Serikali inawajibika kwetu sisi; SISI hatuwajibiki kwa Serikali.

Kwa kuwa Serikali – ambayo inawajibika kwetu – imeamua kukiuka mkataba uliopo kati yetu, ninapendekeza tufanye yafuatayo, baada ya muda wa saa 72 kukamilika, muda ambao ninapendekeza Serikali irudishe matangazo ya luninga ya moja-kwa-moja kupitia TBC 1, chombo cha habari kinachoendeshwa kwa kodi zetu. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo:

1. Kusitisha kununua magazeti yanayomilikiwa na Serikali, yaani “Habari Leo” na “Daily News”
2. Kusitisha kutazama na kusikiliza vituo vyote vya redio na luninga vya TBC 1, ambayo inasimamiwa KIMABAVU na Serikali; vituo hivyo ni TBC 1 na TBC 2; TBC Taifa, TBC FM na TBC International
3. Zoezi hili lifanyike kwa siku zisizopungua 30 (mwezi mmoja) hadi hapo Serikali itakaporejesha matangazo hayo ya Bunge ya moja-kwa-moja​

Ndugu Wananchi, tambueni kwamba TUNAYO HAKI ya kufanya hivi bila kuvunja sheria, kwa kuwa SISI NDIO WAMILIKI WA SERIKALi! Serikali imeingia kwenye mkataba na raia wa Tanzania kupitia mkataba, na jambo hili limedhihirishwa kwenye Katiba kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii” (Ibara ya 8-(1) (a). Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba SISI WANANCHI ndio wamiliki wa MAMLAKA YOTE, na wanachofanya watendaji wa Serikali ni UASI; hawana mamlaka ya kufanya maamuzi makubwa yanayokiuka Katiba BILA KUTUSHIRIKISHA, kwa kuwa “Serikali itawajibika kwa wananchi.”

Tumekuwa wakimya KWA MUDA MREFU MNO! Sasa umefika wakati wa KUCHUKUA HATUA!

Tuna wajibu wa kudai haki zetu kwa kuwa, kama alivyosema William Hague, “Serikali zinazozuia azma za wananchi wake, zinazoiba na za kifisadi, zinazowanyanyasa na kuwatesa au kuwanyima uhuru wa mawazo na haki za kibinadamu, zinapaswa kuzingatia ukweli kwamba zitakuwa na wakati mgumu wa kukwepa hukumu itakayotolewa na wananchi enyewe, au, panapostahili, mikono ya sheria za kimataifa.”

#BungeLive
#UhuruWaHabari
#UhuruWaMawazo

Tushiriki zoezi hili la kudai haki zetu kwa kuweka sahihi zetu hapa

www.ipetitions.com/petition/bunge-live-now

================

bunge.png

TAMKO:
Sisi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatumia haki yetu ya Kikatiba kutoa maoni yetu, kuhusu kitendo kiovu cha Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ifuatavyo:

1.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-2, inayosema "Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii",

2.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 8(1)-a "wananchi ndio msingi wa MAMLAKA YOTE na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujubu wa Katiba hii",

3.Na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba hii, "Ibara ya 8(1)-c, Serikali itawajibika kwa wananchi", na "(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii",

Tunatoa tamko lifuatalo:

1.Serikali imekiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwanyima wananchi haki yao ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali mchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia, juu ya masuala muhimu kwa jamii, HUSUSAN matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.Serikali imetoa kisingizio kwamba gharama za matangazo hayo ni Shilingi za Tanzania Bilioni 4 kwa mwaka, lakini imekataa kupokea michango ya gharama hizo kutoka kwa wananchi, bila kutoa sababu za kuridhisha, hata pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari nchini vilipojitolea kubeba gharama hizo moja kwa moja na kutangaza matangazo hayo

Sisi Wananchi, raia wa Tanzania, tumeamua kufanya yafuatayo:

1.Tutaaacha kununua magazeti yanayochapishwa na vyombo vya habari vinavyosimamiwa na Serikali

2.Tutaacha kusikiliza vituo vya redio na luninga vinavyoendeshwa na Serikali

3.Tutafanya hivi kwa kipindi kisichopungua siku 30, baada ya muda usiopungua saa 72, ambazo tunaitaka Serikali iwe imerejesha mfumo wa matangazo ya moja kwa moja kupitia kituo cha luninga cha TBC1, ambacho kinaendeshwa kwa kodi za wananchi, yaani SISI, ambao kwa mujibu wa Katiba "ndio msingi wa MAMLAKA YOTE"!

Serikali yet IMEASI. Imetunyanyasa vya kutosha, imetupuuza vya kutosha, sasa tunasema, hatutanyanyaswa tena na hatutapuuzwa vya kutosha.

HITIMISHO:
Iwapo maendeleo ya kweli yanapaswa kufanyika, ni lazima wananchi wahusishwe! - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 
bunge kuwa live na wananchi kuona kinachofanyika bungeni ni haki ya wananchi kimsingi anayepora haki hii hawatendei haki wananchi.

wasiwasi wangu ni pale bunge linapotumika kama chombo cha propaganda za kisiasa,
wabunge badala ya kuweka maslahi ya nchi wameweka maslahi ya vyama vyao.

ccm kazi yao kusifia tu serikali hata. pale inapokosea.

wapinzani wao kukosoa tu hata pale serikali inapofanya vizuri hii sio sawa.

tukiacha kuligeuza bunge kama jukwaa la kisiasa ndipo umuhimu wake wa kuwa live utaonekana.
 
Umeliona hilo tu ndani ya KATIBA? Nini haki nyingine ulizoziona.Hili la BUNGE LIVE haliwezekani tulete JF hoja nyinginezo za kuijenga TANZANIA YETU.Kila Mtanzania anaelewa dhiki zake Nakuona Serikali ya Awamu ya Tano inawafanyia nini hilo ndiyo la Msingi.Mbona hampigii kelele za ufisadi Rushwa Ukiukwaji wa Maadili ya Viongozi n.k. badala yake kushikiwa Bango la BUNGE LIVE.?Kulikoni Kipindi cha PROMO kiimeisha Badala yake Mbunge /Mwakilishi anawafanyia nini WAPIGA KURA wake.Kihistoria wabunge watambue wananchi wanauelewa mkubwa na sio kulishwa Maneno eti Viongozi fulani wamesema.Mbona hawayasemi yale waliyokuwa wakituaminisha na kuyapigia kelele Tukiwaona LIVE katika RUNINGA ni Hoja ya Mshiko warejee katika Matamko yao.Na si kuja na Hoja ya BUNGE LIVE!!!!
 
Ndugu Wananchi,

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-1, inatamka ifuatavyo:

Uhuru wa Mawazo

18.- (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha n, shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.​

Kwa mtazamo huu, tunavyoadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari duniani, kwamba uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta matangazo ya moja-kwa-moja ya vikao rasmi vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na, badala yake, kutayarisha kipindi ambacho kimehaririwa, ambacho kinahaririwa na kurushwa baadae kwenye kituo cha luninga cha TBC1, ni dhahiri kwamba Serikali IMEVUNJA KATIBA!

Kwa mujibu wa Katiba, Serikali inapata mamlaka ya kutawala nchi kama ifuatavyo:

8.- (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.​

Bila KUMUNG’UNYA MANENO, ni dhahiri kwamba Serikali imekiuka Katiba kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 9 na Ibara ya 18. SISI RAIA WA TANZANIA hatukuingia mkataba na Serikali ili ivunje haki zetu. Serikali inatudhulumu kwa kufanya maamuzi ambayo yake nje ya mamlaka yake; haina mamlaka ya kufanya uamuzi unaoingilia haki zetu za Kikatiba BILA KUTUSHIRIKISHA. Inaminya haki zetu, hususan haki ya “kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii” kama ilivyoainishwa na Ibara ya 18.

Sasa umefika wakati – ambapo tumechelewa sana – wa sisi raia ambao ndio MSINGI WA MAMLAKA YOTE kuiwajibisha Serikali, kwa kuwa Serikali inawajibika kwetu sisi; SISI hatuwajibiki kwa Serikali.

Kwa kuwa Serikali – ambayo inawajibika kwetu – imeamua kukiuka mkataba uliopo kati yetu, ninapendekeza tufanye yafuatayo, baada ya muda wa saa 72 kukamilika, muda ambao ninapendekeza Serikali irudishe matangazo ya luninga ya moja-kwa-moja kupitia TBC 1, chombo cha habari kinachoendeshwa kwa kodi zetu. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo:

1. Kusitisha kununua magazeti yanayomilikiwa na Serikali, yaani “Habari Leo” na “Daily News”
2. Kusitisha kutazama na kusikiliza vituo vyote vya redio na luninga vya TBC 1, ambayo inasimamiwa KIMABAVU na Serikali; vituo hivyo ni TBC 1 na TBC 2; TBC Taifa, TBC FM na TBC International
3. Zoezi hili lifanyike kwa siku zisizopungua 30 (mwezi mmoja) hadi hapo Serikali itakaporejesha matangazo hayo ya Bunge ya moja-kwa-moja​

Ndugu Wananchi, tambueni kwamba TUNAYO HAKI ya kufanya hivi bila kuvunja sheria, kwa kuwa SISI NDIO WAMILIKI WA SERIKALi! Serikali imeingia kwenye mkataba na raia wa Tanzania kupitia mkataba, na jambo hili limedhihirishwa kwenye Katiba kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii” (Ibara ya 8-(1) (a). Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba SISI WANANCHI ndio wamiliki wa MAMLAKA YOTE, na wanachofanya watendaji wa Serikali ni UASI; hawana mamlaka ya kufanya maamuzi makubwa yanayokiuka Katiba BILA KUTUSHIRIKISHA, kwa kuwa “Serikali itawajibika kwa wananchi.”

Tumekuwa wakimya KWA MUDA MREFU MNO! Sasa umefika wakati wa KUCHUKUA HATUA!

Tuna wajibu wa kudai haki zetu kwa kuwa, kama alivyosema William Hague, “Serikali zinazozuia azma za wananchi wake, zinazoiba na za kifisadi, zinazowanyanyasa na kuwatesa au kuwanyima uhuru wa mawazo na haki za kibinadamu, zinapaswa kuzingatia ukweli kwamba zitakuwa na wakati mgumu wa kukwepa hukumu itakayotolewa na wananchi enyewe, au, panapostahili, mikono ya sheria za kimataifa.”

#BungeLive
#UhuruWaHabari
#UhuruWaMawazo

Tushiriki zoezi hili la kudai haki zetu kwa kuweka sahihi zetu hapa

================

View attachment 344518

TAMKO:
Sisi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatumia haki yetu ya Kikatiba kutoa maoni yetu, kuhusu kitendo kiovu cha Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ifuatavyo:

1.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-2, inayosema "Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii",

2.Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 8(1)-a "wananchi ndio msingi wa MAMLAKA YOTE na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujubu wa Katiba hii",

3.Na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba hii, "Ibara ya 8(1)-c, Serikali itawajibika kwa wananchi", na "(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii",

Tunatoa tamko lifuatalo:

1.Serikali imekiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwanyima wananchi haki yao ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali mchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia, juu ya masuala muhimu kwa jamii, HUSUSAN matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.Serikali imetoa kisingizio kwamba gharama za matangazo hayo ni Shilingi za Tanzania Bilioni 4 kwa mwaka, lakini imekataa kupokea michango ya gharama hizo kutoka kwa wananchi, bila kutoa sababu za kuridhisha, hata pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari nchini vilipojitolea kubeba gharama hizo moja kwa moja na kutangaza matangazo hayo

Sisi Wananchi, raia wa Tanzania, tumeamua kufanya yafuatayo:

1.Tutaaacha kununua magazeti yanayochapishwa na vyombo vya habari vinavyosimamiwa na Serikali

2.Tutaacha kusikiliza vituo vya redio na luninga vinavyoendeshwa na Serikali

3.Tutafanya hivi kwa kipindi kisichopungua siku 30, baada ya muda usiopungua saa 72, ambazo tunaitaka Serikali iwe imerejesha mfumo wa matangazo ya moja kwa moja kupitia kituo cha luninga cha TBC1, ambacho kinaendeshwa kwa kodi za wananchi, yaani SISI, ambao kwa mujibu wa Katiba "ndio msingi wa MAMLAKA YOTE"!

Serikali yet IMEASI. Imetunyanyasa vya kutosha, imetupuuza vya kutosha, sasa tunasema, hatutanyanyaswa tena na hatutapuuzwa vya kutosha.

HITIMISHO:
Iwapo maendeleo ya kweli yanapaswa kufanyika, ni lazima wananchi wahusishwe! - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
kamanda hatutaki ushenzi ondoa takataka yako hapa. hatuna muda wa kuangalia bungelive muda huo tutaupata wapi. unataka kutuongopea tusifanye shughuli zetu za kiuchumi wakati nyinyi mnaendelea kula bata. bunge live inatisaidia nini katika kutuongezea uchumi wetu. hiyo ni kazi ya wabunge wanalipwa kwa kazi hiyo, tunachowataka majimboni kwetu waje watimize ahadi zao walizotoa wakati wa kampeni. fullstop. eti bunge live. ! kwani mbona linaonyeshwa usiku na habari zote tunazipata kuputia vyombo vya habari. nini kipya. mnataka kutuonyesha jinsi wanavyotoa hoja za shanga ,au jinsi wataalam wa matusi wanavyoyabubujisha mjengoni. hatuna muda na ujinga huo.
mlipewa time ya kujitokeza mwwnye pesa za kulipia airtime ambazo ni 4bilioni. hakuna hata bepari mmoja aliyejitokeza. kwa nini mnataka kupata umaarufu kutumia fedha za walipa kodi kwa faida yenu wenyewe. whyyyy.
tunasema na tunatoa tahadhari kwa niamba ya wananchi wazalendo wa nchi hii ambao wameamua kuweka kando siasa zenu za uongo na kweli na kuamua kujenga uchumi kwa nguvu zote. usanii wa kisiasa umetuchosha . tafuteni issue nyingine.
pesa hizi za kugharamia bunge live ziende zikagharamie madawa na matibabu mahospitalini.shule bure, kununua madawati, mabarabara, maabara za shule. pembejeo na mengineyo.tuacheni tuchape kazi kwa uhuru na amani iki tujenge uchumi wetu binafsi. biashara ya siasa mtuletee wakati wa uchaguzi ukikaribia. ni aibu watu wazima kulilia eti bunge live bila kujua kwamba wanatumia muda wao vibaya kujenga uchumi wao kwa kushinda mbele ya luninga kutwa nzima. ushabiki wa style hiyo wajameni umepitwa na wakati
 
Bunge kuwa live linawafanya wananchi kushiriki moja kwa moja katika mijadala inayoendelea bungeni. Hasa mijadals ya budget. Cha ajabu hadi sasa habari za bunge ni chache sana kwenye vyombo vya habari. Serikali ijue wananchi hawajafurahia hili jambo!
 
Kwa hoja hizo ulivyozipangilia, ukikosa ukuu wowote katika awamu hii basi tena rudi Tabora tuline Asali.
 
CCM wanawafanya wajinga waendelee kumshangilia Magu kwa kutumbua majipu.TBC kila akiongea rais lazima awe LIVE, yaani kwa upande wa rais hakuna gharama. Spika wa awamu hii atakuwa mbovu kuliko yeyote waliopita
 
Bunge kuwa live linawafanya wananchi kushiriki moja kwa moja katika mijadala inayoendelea bungeni. Hasa mijadals ya budget. Cha ajabu hadi sasa habari za bunge ni chache sana kwenye vyombo vya habari. Serikali ijue wananchi hawajafurahia hili jambo!
How mwananchi ashiriki mijadala moja kwa moja? So mbunge kule bungeni atakuwa anafanya kazi gani wakati na mimi huku nashiriki mjadala?, uwakilishi wake utakuwa wa kazi gani tena? Je haki ya kikatiba ni kupata habari au ni bunge kuonekana live?
 
Hii sawa, lakini kitatokea nini kama tukifanya hayo yote halafu walevi wa madaraka wasisikilize maoni ya wenye Mali?
 
Nimemuona Nape Nnauye ameanza kutaga.
Anasema eti yeye kama serikali yuko tayari kukaa katikati ya Bunge na Wadau kujadili mwenendo wa urushwaji wa matangazo ya bunge.
Naamini soon serikali itachutama.
Hata mimi nimemona aisee... Inawezekana huyo jamaa ana akili fupi sana!!! Hata sijui nifananishe na nini ili nieleweke.
Amesahau 'aliporopoka' ya kuwa kurusha matangazo moja kwa moja ni gharama, walivyojitokeza wadau, naona anadai eti ni kanuni..
CCM inajidhalilisha yenyewe.
Leo Nape ameongeza ushahidi usiotia shaka juu ya unafiki wake.
N.B. Hata kuperuzi tovuti za hivyo vyombo vya habari inapaswa kuwa 'dhambi'.
Aliwahi kusema kuwa atakaa na wanahabari ili kuangalia namna ya kupunguza adha wanazokutana nazo ktk kupata habari za Bunge pale Dodoma, je amewahi kufanya hivyo?
JE ATAHUDUMIA MABWANA WANGAPI??
 
Aliyewaita akina Jumanne Maghembe n.k "mawaziri mizigo", anaelekea kuitwa 'Absent minded' na jamii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom