UZUSHI Pen (kalamu) zinazolipuka kama Bunduki zinagawiwa na kuuzwa kwenye Shule za Tanzania

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa.

1000032648.jpg


Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo.

Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.


 
Tunachokijua
Bunduki ya kalamu ni bunduki inayofanana na kalamu ya wino. Kwa ujumla ni za kiwango kidogo (k.m., .22 LR, .25 ACP, .32 ACP, .38-caliber, n.k.) Na huwa na uwezo wa kubeba risasi moja pekee.

images
Siku za hivi karibuni imesambaa video ikionesha mikono na kusikika sauti ya ya mtu mmoja anayeongea lugha ya kigeni huku akionesha Kitu kama kalamu ambacho aliweka risasi na kisha kukifyatua na kikalipuka mithiri ya bunduki. Hali hiyo ya kulipuka inafanya tuamini bila shaka hiyo ni bunduki ndogo iliyotengenezwa katika umbo la kalamu.

Katika video hiyo ambayo ilianza kusambaa wiki mbili zilizopita Kuanzia tarehe 8 April 2024 ambapo kulingana na video iliyopo mtandao wa Youtube inaonesha video hiyo ilianza kusambaa kutokea South Africa katika mtandao wa Youtube kisha kuenea mitandao mingine japo video hiyo imekuwepo mtandaoni muda mrefu.

Baadaye tena ilisambaa video hiyohiyo kwene mitandao ya kijamii Nchini Tanzania ikiwa imewekwa sauti ya mwanamke anayeongea lugha ya kiswahili ambaye alidai wametumiwa video hiyo kwenye kundi sogozi (group) la Shule ya ThemiHill ambapo wameambiwa kalamu hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa, huku akiongea kuonesha wasiwasi juu ya watoto kuuana au kujeruhiana kwa kutumia kalamu hizo.

Je, ukweli ni upi juu ya uwepo wa kalamu hizo nchini?

Jamiicheck
ilichukua hatua ya kuifatilia taarifa hiyo ili kubaini ukweli wake, ambapo tulimtafuta Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo ambaye alieleza kuwa:

Clip hiyo ameiona na kuisikiliza, Mkuu wa shule amesema clip ya kwanza aliwahi kuiona muda mrefu siyo leo wala mwaka jana, ambayo inaongea lugha ngeni.

"Clip kwenye mitandao zipo 3, clip ya kwanza inaongea lugha ngeni na inatembea yenyewe na ipo mtandaoni sio leo wala mwaka jana
".
Alisema Mkurugenzi wa shule ya Themi hill

Aliendelea kusema kuwa clip hiyo hiyo kuna mama mmoja anayeongea kiswahili ambaye hamfahamu wala hafamu lengo lake, ameiwekea sauti video hiyo huku akiituhumu Themihill kugawa kalamu za bunduki kwa wanafunzi.

"Clip hiyo hiyo kuna Mama mmoja ameiwekea voice clip akitutuhumu Themihill kwamba sisi tunagawa kalamu bunduki kwa wanafunzi. Sasa mimi ninachojua bunduki zote pamoja na risasi kwa Tanzania ni mali ya Serikali, ukitaka kumiliki lazima bastola au risasi lazima uwe na kibali maalum cha kumiliki".


Mkurugenzi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo amesema kuwa suala hilo si la kweli na kwamba mama huyo amezusha kwa lengo la aidha kuichafua taasisi yao au kumchafua yeye binafsi, na kwamba hajui anaongea Themihill ipi, ni hiyo ya Tabora au Arusha ukizingatia Arusha kuna Themihill.

Katika kupambana na jambo hili amesema alilitolea taarifa kwenye vyombo ya usalama na Vyombo vya usalama walimhakikishia kuwa clip hiyo haina mantiki yoyote na yeye aipuuze na kuachana nayo, nao Vyombo vya usalama walimuahidi kuendelea kuifatilia kubaini muhusika aliyeweka sauti hiyo ya kiswahili.

"Nilipowaambia vyombo vya usalama waliniambia Mambo, clip hiyo haina mantiki yoyote wewe ignore tu maana ukisikiliza kwa makini huyo mtu ni kama anataka kukuchafua tu kwa Tanzania hakuna kitu kama hicho hivyo nisiwe na wasiwasi".

Mambo amesema hafahamu kwa nini mtu huyo kaamua kurekodi clip hiyo, kwa nini kaisambaza na alikuwa na lengo gani, pia amesema yeye hana hakika hata kama kwa Tanzania kuna weza kuwa na bunduki ya aina hiyo, Piaamesema yeye hela ya kununua Bunduki za kuwagawia wanafunzi anazipata wapi iwa hata kalamu wala daftari hajawahi kutoa.

Ameeleza kuwa hata mwananfunzi afaulu kwa kiwango kikubwa sana hajawahi kutoa zawadi ya aina yoyote zaidi ya kumpa punguzo la ada, sasa iweje aanze kugawa bunduki, hivyo amekanusha kuwa taarifa hizo za kwenye clip si za kweli na wala hazihusiani naye wala shuleya Themihill.

Pia ili kujiridhisha zaidi Jamiicheck ilimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao ambaye alithibisha kutokuwepo kwa kalamu hizo za bunduki.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, Kasema kwenye Mkoa wake hakuna tukio Kama hilo la kugawa Bunduki au Silaha.

"Kwenye akili ya Kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani. Kama kutakuwepo kalamu yenye Silaha itakuwa na thamani kubwa sana, uwezekano wa kusema inaweza ikasambazwa kwa wanafunzi bure ni Kitu ambacho hakiwezekani". Amesema ACP Abwao

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi w wa Shule ya Themihill na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tabora na uwepo wa video clip hiyo mtandaoni kwa muda mrefu Jamiicheck inathibitisha kuwa clip hiyo iliyowekwa sauti ya kiswahili ni ya uzushi.
M nikiona mtu anaamin vitu kama hiv naonaga ni ana mental problem, yan kitu cha kureason dakika 2 nakujua ni impossible yeye anashupalia, kama huyo mdada anaeweka hadi sauti, ni wakukamata na kufunga
Hao ndiyo wafuasi wa manabii. Wanaamini hata visivyo na mantiki.
 
Wewe ulieleta hii habari hapa tuwekee namba ya huyo mwalimu tumhoji maana ninayomaswali mengi.
Ila swali kama ifuatavyo.

Unadhani kama hiyo shule kweli ingekuepo siingebidi uongozi uwekwe nyuma ya geti ili usaidie polisi?
Au tunajuaje kama ni ajenda ya kuchafua shule tajwa?
Kwani huyo anaesambaza hizo toi anapata maslahi gani?
Je wameshapigwa wanafunzi wangapi na waliofariki ni wangapi?
 
Wewe ulieleta hii habari hapa tuwekee namba ya huyo mwalimu tumhoji maana ninayomaswali mengi.
Ila swali kama ifuatavyo.

Unadhani kama hiyo shule kweli ingekuepo siingebidi uongozi uwekwe nyuma ya geti ili usaidie polisi?
Au tunajuaje kama ni ajenda ya kuchafua shule tajwa?
Kwani huyo anaesambaza hizo toi anapata maslahi gani?
Je wameshapigwa wanafunzi wangapi na waliofariki ni wangapi?
Sasa nikupe namba ili iweje mkuu wkt hapo hapo unasema jina la shule limetajwa inaweza kuharibu biashara ya mtu?.

Why usijiongeze kuitafuta hiyo shuke ilihali imetwajwa na huyo mzazi?.
 
Kila kitu kinawezekana Wazungu wanatulazimisha tuwe mashoga SisiWafrika ili tusipate kuzaliana Wazungu wameleta ugonjwa wa korona wakapeleka nchini china ili kupunguza watu duniani itakuwa kutengeneza silaha ya peni kuwa maliza watoto wetu? Kwa Akili yako wewe unafikiri Wazungu wanawapenda Watu weusi?
Yaani unagawa ndogo halafu Lawama Zote Kwa John?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom