UZUSHI Pen (kalamu) zinazolipuka kama Bunduki zinagawiwa na kuuzwa kwenye Shule za Tanzania

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa.

1000032648.jpg


Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo.

Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.


 
Tunachokijua
Bunduki ya kalamu ni bunduki inayofanana na kalamu ya wino. Kwa ujumla ni za kiwango kidogo (k.m., .22 LR, .25 ACP, .32 ACP, .38-caliber, n.k.) Na huwa na uwezo wa kubeba risasi moja pekee.

images
Siku za hivi karibuni imesambaa video ikionesha mikono na kusikika sauti ya ya mtu mmoja anayeongea lugha ya kigeni huku akionesha Kitu kama kalamu ambacho aliweka risasi na kisha kukifyatua na kikalipuka mithiri ya bunduki. Hali hiyo ya kulipuka inafanya tuamini bila shaka hiyo ni bunduki ndogo iliyotengenezwa katika umbo la kalamu.

Katika video hiyo ambayo ilianza kusambaa wiki mbili zilizopita Kuanzia tarehe 8 April 2024 ambapo kulingana na video iliyopo mtandao wa Youtube inaonesha video hiyo ilianza kusambaa kutokea South Africa katika mtandao wa Youtube kisha kuenea mitandao mingine japo video hiyo imekuwepo mtandaoni muda mrefu.

Baadaye tena ilisambaa video hiyohiyo kwene mitandao ya kijamii Nchini Tanzania ikiwa imewekwa sauti ya mwanamke anayeongea lugha ya kiswahili ambaye alidai wametumiwa video hiyo kwenye kundi sogozi (group) la Shule ya ThemiHill ambapo wameambiwa kalamu hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa, huku akiongea kuonesha wasiwasi juu ya watoto kuuana au kujeruhiana kwa kutumia kalamu hizo.

Je, ukweli ni upi juu ya uwepo wa kalamu hizo nchini?

Jamiicheck
ilichukua hatua ya kuifatilia taarifa hiyo ili kubaini ukweli wake, ambapo tulimtafuta Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo ambaye alieleza kuwa:

Clip hiyo ameiona na kuisikiliza, Mkuu wa shule amesema clip ya kwanza aliwahi kuiona muda mrefu siyo leo wala mwaka jana, ambayo inaongea lugha ngeni.

"Clip kwenye mitandao zipo 3, clip ya kwanza inaongea lugha ngeni na inatembea yenyewe na ipo mtandaoni sio leo wala mwaka jana
".
Alisema Mkurugenzi wa shule ya Themi hill

Aliendelea kusema kuwa clip hiyo hiyo kuna mama mmoja anayeongea kiswahili ambaye hamfahamu wala hafamu lengo lake, ameiwekea sauti video hiyo huku akiituhumu Themihill kugawa kalamu za bunduki kwa wanafunzi.

"Clip hiyo hiyo kuna Mama mmoja ameiwekea voice clip akitutuhumu Themihill kwamba sisi tunagawa kalamu bunduki kwa wanafunzi. Sasa mimi ninachojua bunduki zote pamoja na risasi kwa Tanzania ni mali ya Serikali, ukitaka kumiliki lazima bastola au risasi lazima uwe na kibali maalum cha kumiliki".


Mkurugenzi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo amesema kuwa suala hilo si la kweli na kwamba mama huyo amezusha kwa lengo la aidha kuichafua taasisi yao au kumchafua yeye binafsi, na kwamba hajui anaongea Themihill ipi, ni hiyo ya Tabora au Arusha ukizingatia Arusha kuna Themihill.

Katika kupambana na jambo hili amesema alilitolea taarifa kwenye vyombo ya usalama na Vyombo vya usalama walimhakikishia kuwa clip hiyo haina mantiki yoyote na yeye aipuuze na kuachana nayo, nao Vyombo vya usalama walimuahidi kuendelea kuifatilia kubaini muhusika aliyeweka sauti hiyo ya kiswahili.

"Nilipowaambia vyombo vya usalama waliniambia Mambo, clip hiyo haina mantiki yoyote wewe ignore tu maana ukisikiliza kwa makini huyo mtu ni kama anataka kukuchafua tu kwa Tanzania hakuna kitu kama hicho hivyo nisiwe na wasiwasi".

Mambo amesema hafahamu kwa nini mtu huyo kaamua kurekodi clip hiyo, kwa nini kaisambaza na alikuwa na lengo gani, pia amesema yeye hana hakika hata kama kwa Tanzania kuna weza kuwa na bunduki ya aina hiyo, Piaamesema yeye hela ya kununua Bunduki za kuwagawia wanafunzi anazipata wapi iwa hata kalamu wala daftari hajawahi kutoa.

Ameeleza kuwa hata mwananfunzi afaulu kwa kiwango kikubwa sana hajawahi kutoa zawadi ya aina yoyote zaidi ya kumpa punguzo la ada, sasa iweje aanze kugawa bunduki, hivyo amekanusha kuwa taarifa hizo za kwenye clip si za kweli na wala hazihusiani naye wala shuleya Themihill.

Pia ili kujiridhisha zaidi Jamiicheck ilimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao ambaye alithibisha kutokuwepo kwa kalamu hizo za bunduki.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, Kasema kwenye Mkoa wake hakuna tukio Kama hilo la kugawa Bunduki au Silaha.

"Kwenye akili ya Kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani. Kama kutakuwepo kalamu yenye Silaha itakuwa na thamani kubwa sana, uwezekano wa kusema inaweza ikasambazwa kwa wanafunzi bure ni Kitu ambacho hakiwezekani". Amesema ACP Abwao

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi w wa Shule ya Themihill na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tabora na uwepo wa video clip hiyo mtandaoni kwa muda mrefu Jamiicheck inathibitisha kuwa clip hiyo iliyowekwa sauti ya kiswahili ni ya uzushi.
Hapa wazungu wanahusikaje? Ni malalamiko yale yale ya kipumbavu siku zote. Asilimia 80 ya vitu ulivyo navyo asili yake au vimetengenezwa na wazungu. We unataka wakupende we mwanamke? Usitake kupendwa na wazungu pambana na maisha yako yakae sawa.
Huyu jmaa mleta thread ni tapeli mmoja anayejifanya anajua mizizi ya dawa. Kila ugonjwa kwake unatibika. Yuko obsessed na wazungu kwa sababu anataka watu waingie kwenye anga za utapeli wake.
 
We jamaa ni MTU ambaye huwa unaendeshwa na Emotions jambo ambalo linakufanya Una-decline responsibility na kutokuwa logically.

Jitahidi ubadilike .

Mzungu hajakufanya usifanikiwe au ufanikiwe ni swala la kuwa na ufahamu.

Biashara ya kusema unatibu magonjwa yote kwa mizizi ni uongo tu ambao hauna msingi wowote .

Post zako 99% ni uongo tu
 
Huyu jmaa mleta thread ni tapeli mmoja anayejifanya anajua mizizi ya dawa. Kila ugonjwa kwake unatibika. Yuko obsessed na wazungu kwa sababu anataka watu waingie kwenye anga za utapeli wake.
Yupo self-obsessed

Namjua muongo muongo sana
 
Hiyo video siyo halisi, imeingiziwa sauti tu. Kwa mbaali kuna sauti ingine ambayo inaelezea matumizi ya hiyo kalamu.
 
Kila kitu kinawezekana Wazungu wanatulazimisha tuwe mashoga SisiWafrika ili tusipate kuzaliana Wazungu wameleta ugonjwa wa korona wakapeleka nchini china ili kupunguza watu duniani itakuwa kutengeneza silaha ya peni kuwa maliza watoto wetu? Kwa Akili yako wewe unafikiri Wazungu wanawapenda Watu weusi?
Mkuu, umeamka vipi leo? Mbona hii habari ambayo ni pure uzushi imekuwepo mitandaoni muda mrefu na majibu yamekuwa yakitolewa kuhusu uhalisia (Ukweli) wa habari hii?

Kwanza nakushauri ww kama msomi(Dr) uache chuki binafsi dhidi ya Wazungu eti wanatulazimisha tuwe mashoga. Kuwa shoga hakumhitaji mzungu aje kukulazimisha. Ushoga umekuwapo enzi na enzi hapa Afrika sema tu ww ulikuwa hujui na wala hujafuatilia. Tena ww kama Dr. inafaa ujue kwamba kuwa shoga hakumzuii mtu kuzaliana. Halafu unasema Wazungu eti wameleta korona. Je, unaweza kuthibitisha hilo?

Mwisho unadai utengenezwaji wa silaha ya peni ni kwa ajili ya kuwamaliza watoto wetu. Inakuwaje mkuu unajitoa ufahamu kuhusu umiliki wa silaha za moto halafu eti mtu atengeneze kitu cha gharama kubwa hivyo halafu eti aje kuwagawia wanafunzi mashuleni BURE.

Ni kweli hizo silaha za peni zipo na zimekuwepo muda mrefu ni pamoja na silaha zingine size ndogo na hutumika kujihami hususan na majasusi e.g. CIA, Mossad, n.k. Fuatilia tu mkuu utajua.
Nakuomba tuache kutoa Taarifa zitakazoweza kuzua taharuki miongoni mwa Jamii bila sababu yeyote. Vyombo vya Usalama vya nchi yetu vipo makini 24 hrs. na sio rahisi kitu kama hicho kiwepo hapa nchini bila wao kujua.

NB: Hii ni mada nzuri kwa majadiliano, kubishana kistaarabu na kwa hoja ila haina ukweli wowote.
 
ILa ni mkongwe sana humu ndani tumsamehe na tumpe heshima yake kidogo maana wakati mwingine ana post Madini ila Leo Kwa Mara ya kwanza kapost thread mandazi kabisa labda angeiweka jukwaa la jokes

Muhuni huyo mkuu
Ansema anatibu magonjwa yote kupitia mizizi
 
Hiyo shule ipo Tabora, huyo mama ni mzushi ameamua kuzua taharuki tu.
Huyo aliyeshika pen ukimsikiliza uongeaji wake, wala hayupo Tanzania.
Kwa akili za kawaida hiyo silaha wewe unaina inaweza ikauzwa kwa bei ya Pen hata zisambazwe mashuleni?
Huo mlio umeisikia?
Kama hiyo shule kweli ipo Tabora Polisi Watafuatilia zaidi ili tupate kujuwa kama kuna ukweli wowote hakuna cha taharuki hapo tunachotaka sisi usalama wa watoto wetu walioko Mashuleni sio tena mpaka wafe watoto ndipo tupate kujuwa hicho kitu hatukitaki . Nchi yetu ni nchi ya amani hatutaki maafa yatokee mahali popote pale nchini mwetu.Ninaipenda nchi yangu.
 
Tumia akili zako vizuri basi hata kidogo. yaani mtu agawe hizi bunduki shuleni kwa lengo gani? Manake kumbuka hii sio kalamu ni bunduki, hizi hutumika zaidi na mashushu. Unafikiri hii thamani yake ni sh 1,000 ? au buku 5 ? Hata mtu anunue aende kuzigawa shuleni? Yaani waalimu wapo alafu waruhusu na hii kitu kabisa??? We unaona inawezekana??? Habari za kipuuzi hizi
 
Ni kweli hizo silaha za peni zipo na zimekuwepo muda mrefu ni pamoja na silaha zingine size ndogo na hutumika kujihami hususan na majasusi e.g. CIA, Mossad, n.k. Fuatilia tu mkuu utajua.
. Vyombo vya Usalama vya nchi yetu vipo makini 24 hrs. na sio rahisi kitu kama hicho kiwepo hapa nchini bila wao kujua.
Mipaka ya nchi yetu ipo wazi sana, uwezekano wa kuingia vifaa vya namna hii upo mkubwa sana tofauti na unavyofikiri mkuu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom