SI KWELI Pen zinazotoa risasi kama Bunduki zinagawiwa na kuuzwa kwenye Shule za Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa.

1000032648.jpg


Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo.

Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.


 
Tunachokijua
Bunduki ya kalamu ni bunduki inayofanana na kalamu ya wino. Kwa ujumla ni za kiwango kidogo (k.m., .22 LR, .25 ACP, .32 ACP, .38-caliber, n.k.) Na huwa na uwezo wa kubeba risasi moja pekee.

images
Siku za hivi karibuni imesambaa video ikionesha mikono na kusikika sauti ya ya mtu mmoja anayeongea lugha ya kigeni huku akionesha Kitu kama kalamu ambacho aliweka risasi na kisha kukifyatua na kikalipuka mithiri ya bunduki. Hali hiyo ya kulipuka inafanya tuamini bila shaka hiyo ni bunduki ndogo iliyotengenezwa katika umbo la kalamu.

Katika video hiyo ambayo ilianza kusambaa wiki mbili zilizopita Kuanzia tarehe 8 April 2024 ambapo kulingana na video iliyopo mtandao wa Youtube inaonesha video hiyo ilianza kusambaa kutokea South Africa katika mtandao wa Youtube kisha kuenea mitandao mingine japo video hiyo imekuwepo mtandaoni muda mrefu.

Baadaye tena ilisambaa video hiyohiyo kwene mitandao ya kijamii Nchini Tanzania ikiwa imewekwa sauti ya mwanamke anayeongea lugha ya kiswahili ambaye alidai wametumiwa video hiyo kwenye kundi sogozi (group) la Shule ya ThemiHill ambapo wameambiwa kalamu hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa, huku akiongea kuonesha wasiwasi juu ya watoto kuuana au kujeruhiana kwa kutumia kalamu hizo.

Je, ukweli ni upi juu ya uwepo wa kalamu hizo nchini?

Jamiicheck
ilichukua hatua ya kuifatilia taarifa hiyo ili kubaini ukweli wake, ambapo tulimtafuta Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo ambaye alieleza kuwa:

Clip hiyo ameiona na kuisikiliza, Mkuu wa shule amesema clip ya kwanza aliwahi kuiona muda mrefu siyo leo wala mwaka jana, ambayo inaongea lugha ngeni.

"Clip kwenye mitandao zipo 3, clip ya kwanza inaongea lugha ngeni na inatembea yenyewe na ipo mtandaoni sio leo wala mwaka jana
".
Alisema Mkurugenzi wa shule ya Themi hill

Aliendelea kusema kuwa clip hiyo hiyo kuna mama mmoja anayeongea kiswahili ambaye hamfahamu wala hafamu lengo lake, ameiwekea sauti video hiyo huku akiituhumu Themihill kugawa kalamu za bunduki kwa wanafunzi.

"Clip hiyo hiyo kuna Mama mmoja ameiwekea voice clip akitutuhumu Themihill kwamba sisi tunagawa kalamu bunduki kwa wanafunzi. Sasa mimi ninachojua bunduki zote pamoja na risasi kwa Tanzania ni mali ya Serikali, ukitaka kumiliki lazima bastola au risasi lazima uwe na kibali maalum cha kumiliki".


Mkurugenzi wa Shule ya Themihill, Michael Stien Mambo amesema kuwa suala hilo si la kweli na kwamba mama huyo amezusha kwa lengo la aidha kuichafua taasisi yao au kumchafua yeye binafsi, na kwamba hajui anaongea Themihill ipi, ni hiyo ya Tabora au Arusha ukizingatia Arusha kuna Themihill.

Katika kupambana na jambo hili amesema alilitolea taarifa kwenye vyombo ya usalama na Vyombo vya usalama walimhakikishia kuwa clip hiyo haina mantiki yoyote na yeye aipuuze na kuachana nayo, nao Vyombo vya usalama walimuahidi kuendelea kuifatilia kubaini muhusika aliyeweka sauti hiyo ya kiswahili.

"Nilipowaambia vyombo vya usalama waliniambia Mambo, clip hiyo haina mantiki yoyote wewe ignore tu maana ukisikiliza kwa makini huyo mtu ni kama anataka kukuchafua tu kwa Tanzania hakuna kitu kama hicho hivyo nisiwe na wasiwasi".

Mambo amesema hafahamu kwa nini mtu huyo kaamua kurekodi clip hiyo, kwa nini kaisambaza na alikuwa na lengo gani, pia amesema yeye hana hakika hata kama kwa Tanzania kuna weza kuwa na bunduki ya aina hiyo, Piaamesema yeye hela ya kununua Bunduki za kuwagawia wanafunzi anazipata wapi iwa hata kalamu wala daftari hajawahi kutoa.

Ameeleza kuwa hata mwananfunzi afaulu kwa kiwango kikubwa sana hajawahi kutoa zawadi ya aina yoyote zaidi ya kumpa punguzo la ada, sasa iweje aanze kugawa bunduki, hivyo amekanusha kuwa taarifa hizo za kwenye clip si za kweli na wala hazihusiani naye wala shuleya Themihill.

Pia ili kujiridhisha zaidi Jamiicheck ilimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao ambaye alithibisha kutokuwepo kwa kalamu hizo za bunduki.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, Kasema kwenye Mkoa wake hakuna tukio Kama hilo la kugawa Bunduki au Silaha.

"Kwenye akili ya Kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani. Kama kutakuwepo kalamu yenye Silaha itakuwa na thamani kubwa sana, uwezekano wa kusema inaweza ikasambazwa kwa wanafunzi bure ni Kitu ambacho hakiwezekani". Amesema ACP Abwao

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi w wa Shule ya Themihill na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tabora na uwepo wa video clip hiyo mtandaoni kwa muda mrefu Jamiicheck inathibitisha kuwa clip hiyo iliyowekwa sauti ya kiswahili ni ya uzushi.
Sound inayosikika na video ukiiangalia kwa umakini unaona kabisa hapa tunapangwa.
Halafu haijatajwa ni wapi huo mgawo umeshafanyika ili walau wale wenye kazi zao waende huko kufanya uchunguzi kwani hilo sio jambo dogo.
 
Halafu haijatajwa ni wapi huo mgawo umeshafanyika ili walau wale wenye kazi zao waende huko kufanya uchunguzi kwani hilo sio jambo dogo.
Si huyo mama anasema zimeonekana kugaiwa bure na kupelekwa themi Sekondary school. Sijajua hiyo, Themi secondary ipo mkoa gani.
 
Huenda watanzania ujinga hautakwisha vichwani mwetu milele. Hiyo video inayosambaa ni ya wajinga tu, hakuna kitu kipya cha ajabu. Ni uzushi mtupu.

Ngoja niweke sawa.
1. Video halisi haijachukuliwa hapa nchini, na mzungumzaji halisi haongei kiswahili, na alikuwa akionyesha na kueleza bunduki ndogo (pistol) yenye muonekano wa umbile la kalamu. Hizo silaha zimekuwepo duniani kitambo sana (na story zake nilishazisikia miaka mingi mnoo tangu movie za James bond zikilindima), na maduka kibao ya silaha za moto USA zimejaa.

2. Mzungumzaji (mzushi) akaipa maneno yake kulingana na uelewa na wasiwasi wake na kisha kuisambaza mitandaoni ili kuleta hamaki.

Hitimisho.
-Hiyo siyo kalamu, haiandiki, haiwezi kuandika, na huwezi kumpa mtu kama kalamu akaindikie. Hata kuitumia kama silaha ya moto (kuitega risasi na kuifyatua) ni mpaka ujifunze kidogo au kuelewa.

-Hiyo ni silaha ya kuuzwa kwa gharama kule USA (huuzwa milioni+), hakuna mtu mjinga atakuja kuzigawa bure kwa watoto ili wakachezee ili zifyatuke na kuwadhuru).
-Jamii inapoona kitu chenye kuhatarisha usalama wanapaswa kuzitaarifu mamlaka husika za kiusalama tena kutoa taarifa iliyokamilika (wapi? Lini? Nani?) badala ya kuzisambaza mitandaoni ili kutia watu hofu na hamaki.
 
Si huyo mama anasema zimeonekana kugaiwa bure na kupelekwa themi Sekondary school. Sijajua hiyo, Themi secondary ipo mkoa gani.
Arusha. Shule ya Themihill (as a one word) ni Sekondari au Shule ya msingi?Inatuchanganya. Nijuavyo mm Themi hill ni eneo lililopo katika viunga vya Arusha mjini. Hiyo shule Uki-google utaipata kama Themi Sec.School na sio Themihill -Labda kama inajulikana kihivyo kwa wenyeji.
 
Hizo vitu zingekuwa kweli zinagawiwa bure kwa watoto au kuuzwa kama njugu huko Arusha, mpaka muda huu huenda kila 'Mdudu' pale Arusha angekuwa nazo mfukoni kama 10 hivi, na mpaka muda kituo cha Polisi mjini kati (Ngarenaro) pale Arusha kungekuwa na mafuriko ya watu waliotandikwa risasi.
 
Huenda watanzania ujinga hautakwisha vichwani mwetu milele. Hiyo video inayosambaa ni ya wajinga tu, hakuna kitu kipya cha ajabu. Ni uzushi mtupu.
Asante sana mkuu kwa Kutuondolea hofu. Je huyo mzushi haiwezekani Sheria za Jamhuri zikamhusu? Ni hayo tu.
 
Hizo vitu zingekuwa kweli zinagawiwa bure kwa watoto au kuuzwa kama njugu huko Arusha, mpaka muda huu huenda kila 'Mdudu' pale Arusha angekuwa nazo mfukoni kama 10 hivi, na mpaka muda kituo cha Polisi mjini kati (Ngarenaro) pale Arusha kungekuwa na mafuriko ya watu waliotandikwa risasi.
Na baadhi ya waalimu esp. walimu wa Maths, Physics wangekuwa wahanga sana.☕
 
Tactical pen.
Mbona kama mama anayeongea na hao jamaa kwenye clip ni vitu visivyohusiana. Hao wanaonekana sio wabongo. Alafu pia kwa nini peni watoto wauane na kwa maslahi ya nani. Pia hiyo pen inaonekana haina sehemimu ya kuandikia huyo mtoto atainunua ili iweje.

Hapo naona uongo mwingi kuliko ukweli. Pen inaweza kuwa sahihi ila hiyo voiceover ni kama ujanja wa kupata viewers tu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom