KWELI Pele ni mchezaji pekee Duniani aliyeshinda Kombe la Dunia mara 3

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari JamiiCheck,

Nimeona taarifa mtandaoni inayosema Pele ndiye mchezaji pekee duniani aliyeshinda Kombe la Dunia mara 3. Naona kama wanapotosha, inawezekana vipi asiwepo mchezaji mwingine zaidi yake?

Screenshot 2024-05-08 092353.png
 
Tunachokijua
Edson Arantes do Nascimento (Pele) anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wakubwa na maarufu waliowahi kucheza mpira wa miguu. Alizaliwa Oktoba 23, 1940 nchini Brazil na huko ndiko aliamza kucheza mpira mtaani tangu akiwa kijana mdogo.

Alijiunga na klabu ya Santos ya Brazil akiwa na miaka 15 na alidumu kwenye klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 20.

Ni mchezaji pekee aliyeshinda kombe la Dunia mara 3?
Kama ambavyo Heparin amebainisha, ameona mtandaoni taarifa zinazodai kuwa Pele ndiye mchezaji pekee Duniani aliyeshinda komba la dunia mara 3.

Hata hivyo, ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini madai haya yana ukweli. Edson Arantes do Nascimento (Pele) ndiye binadamu pekee kwa sasa aliyeshinda kombe la dunia mara 3, alifanya hivyo akiitumikia timu ya taifa ya Brazil mwaka 1958, 1962 na 1970.

_110989990_peleworldcupgettyimages-96464299.jpg

Edson Arantes do Nascimento (Pele).
Pamoja na kushinda kombe la Dunia mara 3, Pele alifunga alikuwa ndiye mchezaji mdogo zaidi kushinda kombe hilo, amefunga magoli 1283 kwenye maisha yake ya soka huku 77 kati yake akiwa anatumikia timu ya taifa ya Brazili.

Mwaka 1999, Pele alichaguliwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kuwa mwanamchezo wa karne.

Disemba 29, 2022, Pele alifariki Dunia akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua Saratani ua utumbo kwa muda mrefuambapo pamoja na kufariki kwake anaendelea kubaki kwenye mioyo ya Wabrazili kama mchezaji mwenye mafanikio zaidi kwenye timu ya taifa.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom