April 8, 2024
Arusha
⦁ Mapokezi yamenitia moyo wa kuwa mtumishi mwema na mtetezi wa wanyonge. Kamwe sitaungana na fisadi kukandamiza haki zenu, nitakuwa sauti yenu mpaka ukamilifu wa dahali
⦁ Nawashukuru kwa maombi. Kwa dua njema mlionifanyia. Nimekoswa koswa mara tatu kupoteza maisha, na nawaambia, sitakufa bali nitaishi. Niyasimulie matendo makuu ya Mungu.
⦁ Nina mambo au mawazo sita. Lakini lazima nifanye kwanza ziara mniambie, ili yale tunayowaza sisi yafanane na majibu ya changamoto zenu. Nakuja kwenye wilaya zote sita tukutane. Ili kusudi tupate sauti moja.
⦁ La Pili: Hakuna maendeleo bila umoja. Tukishikamana bila kujali dini, kabila, chama, tutapiga hatua. Mkoa usiwe wa malumbano ya kisiasa, bali mkoa wa kujenga uchumi imara, na wa biashara kwa watu wake.
⦁ Sijaja kukandamiza wanasiasa. Sijaja kutangua torati. Wapinzani mkitaka kunishirikisha mnishirikishe. Mkitaka hata mafuta kama tunaweza tutachangia.
⦁ Jambo la tatu, najua Arusha ni mji wa kitalii. Rais Samia ameipendelea Arusha, hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje aungane nanyi. Takwimu za serikali za sekta ya utalii zinatofautiana kati ya Maliasili, na RAS wa Mkoa, na Bodi ya Utalii. Unajiuliza, hawa watu si ni serikali moja ? Which means vyumba hakuna! Kumbi za mikutano hakuna. Tutajenga kumbi mbili kubwa za mikutano. Tutajenga apartment ya vyumba 400, na kiwanja cha mpira cha watu 30,000. Tuache siasa za kunyoosheana vidole, hazituingizii pesa.
⦁ Jambo la nne. Ninalo tangazo jema kwa yeyote anaedai haki yake: Kwa neema na mapenzi ya Mungu utaipata. Kama niko nimekanyaga mahali hapa, na nina kibali cha Rais, basi haki yako utaipata. Hujui kusoma, hujui kuongea ukaeleweka, huna hela, nitakulinda na kukupigania!
⦁ Jambo la tano. Watendaji na watumishi wote Arusha popote ulipo, funga mkanda! Mkurugenzi, RPC, Mkuu wa Idara, DC, Uhamiaji, kaa kwenye kiti chako ueneee. Habari ya kutumia madaraka kuwakandamiza wanyonge, kupendelea wenye pesa imefika mwisho. Kwenye idara yako kama huwakudumii wananchi, cha mtema kuni utakiona.
⦁ Arusha tembeeni kifua mbele. Ya Kwamba Mtaheshimika kwa utu wenu, sio pesa, elimu wala connection. Wanaosema niketolewa uenezi, nimeletwa u RC, sasa CCM nilikuwa nasema wafanye wengine, huku nafanya mwenyewe. Ofisi yeyote ukienda wakikuhudumia vibaya njoo kwangu. Hospitali ukijibiwa vibaya, Polisi wakikunyima dhamana, njoo kwanguuuu... Silogeki! Hofu iliondoka na kitovu waliponikata...
⦁ Jambo la sita: Kamishna wa ardhi NJOO HAPA! Una miezi mitatu kumaliza migogoro ya ardhi. Mnongoza kwa rushwa! Na msijioendekeze kwangu kwa kunipa kiwanja, Arusha viwanja ninavyo. Ardhi ni kilio namba moja...
⦁ Afisa Mipango Miji NJOO HAPA! Mnazalisha squatter! Hakuna mipango miji, mmeshuhudua inajengwa bypass lakini hamkwenda mkapanga na kupima viwanja kuwe na barabara zinazopitika. Mnashinda kule Bulka na Sanawali kwa sababu kuna rushwa. Sasa una miezi mitatu tutakuita utoe ripoti umekuta migogoro mingapi, umetatua mingapi, umekuta watu wangapi hawana hati, umetoa hati ngapi. Na, umejipangaje kuhakikisha migogoro mingine isitokee... Migogoro ya ardhi inasababishwa na nyinyi wataalam wa ardhi! Mtendaji, Mtumishi, usipojipanga tunakupanga!
⦁ Uhamiaji: Mtu ana nyaraka zote, kwa nini passport ichukue siku 14? Na foleni ya Namanga foleni masaa matatu. Natka iwe mwisho dakika 60!
⦁ Mabango kila mahali, mara masaji, mara dawa za kienjeji, hapana. Tunataka screens. Watu wanatushangaa.
⦁ Sisi ni matajiri kuliko wanaokuja kutuhurumia! Maji Arusha yanatoka matope, na kuna suala la bili kubambikizwa. Zinakuja kufungwa mita za pre-Paid.
⦁ Ndugu zanguni, mambo ni mengi. Tutakaa mtanambia mnataka RC wa aina gani lakini kamwe sitawasaliti. Maombi yenu ndio yananiweka hapa. Wajane, vijana, wazee wananambia endelea. Sitawaangusha. Sitalumbana na mtu. Mwenye wazo la kutengeneza ajira, mwenye wazo la kujenga uchumi, kuboresha Arusha, mlango uko wazi.
⦁ KIla anaekuja Arusha apokelewe na kikombe cha kahawa. Ni mji unaotupatia pesa nyingi sana, hatuwezi kuuacha bure. Lets make Arusha Great Again.
⦁ Najua Yapo mambo ya Stendi. Ya soko. Ya boda. Ya dala dala. Ya Tatu Mzuka. Ya bajaji. Ya Wadudu. Nipeni muda.
⦁ Tarehe 12 tutampokea Rais katika tukio kubwa la kumuenzi Hayati Sokoine aliyefanya kazi ya heshima katika taifa hili. Ndio maana mimi ni mchanganyiko wa mtoto wa masai, wa jeshi, wa kisukuma... Sieleweki kwa sababu Mungu amejaa ndani yangu. Nimechukua combination zote nzuri ndo maana pa kunyooka tunanyooka kweli kweli.
⦁ Nimeongea na RPC tunaenda kuongeza nguvu ya ulinzi Arusha, maduka hayafungwi saa 11, saa 12 mbili. Zinakuja camera, taa za kutosha, patrol za baskeli za polisi, pikipiki, rescue team, mpaka helicopter za patrol. Kuhakikisha mnalindwa barabara.
⦁ Mungu wangu na awabariki sana