Paul Makonda kuzungumza na waandishi wa habari muda wowote kuanzia sasa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,605
10,000
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa zinaeleza ya kuwa Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara Paul Christian Makonda atazungumza na waandishi wa habari muda na wakati wowote ule kuanzia sasa.ambapo kuna mambo ambayo atayazungumza kwa kifupi na waandishi wa habari.

Atafanya hivyo kutoa taarifa fupi na kwa ufupi juu ya wito alioitikia wa kufika mbele ya kamati ya maadili ya chama cha Mapinduzi ili kuwatoa hofu watu na kuleta utulivu na kumaliza maneno ambayo kila mtu kwa sasa anaongea na kuzungumza jambo lake..utaratibu ambao ni wa kawaida na hufanyika ndani ya chama cha Mapinduzi. Lakini awamu hii imeteka hisia za watu wengi na kuteka mijadala yote ya kisiasa na kubaki gumzo mitaani na katika kila kijiwe cha siasa kutokana na umachachali na makeke ya Mwamba Makonda.

Kwa kuwakumbusheni ni kuwa CCM Ina utaratibu wa kufanya mahojiano na wanachama wake pale inapoona kuna haja ya kufanya hivyo.imewahi kufanya hivyo kwa makatibu wakuu wake wastaafu mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti,kama vile Mzee Yusuphu Makamba,mzee Abdulhaman Kinana na Kolimba. lakini pia imewahi kuwahoji wajumbe wa kamati kuu na mawaziri wake wastaafu kama vile Hayati Edward lowassa pamoja na Frederick Sumaye. Wengine ni Marehemu Benard Membe , Sofia Simba na wengine wengi tu.

Kwa hiyo ni utaratibu wa kawaida ndani ya chama chetu cha Mapinduzi kuwaita na kuwahoji wanachama wetu panapohitajika kufanya hivyo bila kujali ukubwa wa jina la mtu, wadhifa au cheo alichowahi kushika au Umri wake.

Tuendelee kuwa watulivu kusubiri kitakacho jiri. Hii ndio maana ya CCM kuitwa chama kiongozi na chama kikubwa .ni chama kinachoendeshwa kwa kanuni na misingi ya katiba na kutoa haki ya kusikilizwa kwa wanachama wake .hakikurupuki katika kutoa maamuzi wala kumuonea mtu.

Ndio maana huwezi ukakuta mwanachama wake akiropoka hovyo hovyo akitoka kuhojiwa au baada ya maamuzi kutolewa.kwa kuwa asiye ridhika na maamuzi anayo nafasi ya kukata rufaa kwa ngazi za juu kupata nafasi ya kusikilizwa upya .

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

IMG-20240309-WA0012.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa zinaeleza ya kuwa Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara Paul Christian Makonda

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2971132
Hijasema tu katika huo utaratibu wa kawaida baada ya hivyo vikao kulikuwa na maazimio gani na sasa tutarajie nini kwa huyu kijana machachari kabisa duniani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom