Patcho Mwamba alalamika kusingiziwa kamloga Malou

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,751
2,444
Screenshot_20240427-175439_1.jpg

Baada ya msiba mzito ulioikumba bendi ya FM academia baada ya kuondokewa na mpendwa wao marehemu Malou Stonch, mengi yameibuka.

Akizungumza kwenye chombo kimoja cha habari, kiongozi wa kundi hilo Patcho Mwamba amelalamika kwamba baadhi ya wanamuziki wacongoman wanazusha kwamba yeye ni mchawi na alimloga Malou stonchi.

Pia amelalamikia familia ya marehem, haswa mkewe ambae amekuwa akieneza habari kwamba mumewe alipoanguka, hakupatiwa huduma yoyote ya kwanza bali wanamuziki wenzake waliendelea kuimba na kutoa burudani jukwaani. Jambo hilo Patcho amelipinga vikali huku akisema kwamba mashabiki pia wasingekubali kuona burudani ikiendelea huku mwanamuziki akiwa chini taabani.

Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba, siku ya tukio marehemu alipoanguka chini alipatiwa huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo na kisha kupelekwa hospital na kwamba Patcho hakuwepo jukwaani siku hiyo.

Patcho pia amemlalamikia mke wa marehemu ambae alienda ktk bar ya target kuulizia mumewe alifariki vipi na hata alipoambiwa ukweli hakuukubali, huku akisisitiza mumewe alianguka na wanamuziki hawakujali na waliendelea kutoa burudani.

Tuwaombee Patcho na familia ya marehemu wapatane Ili wafanye 40 ya marehemu salama
 
Kuna mambo yasikie tu maana likitokea jambo halafu watu wakaanza kukunyooshea kidole wewe hata ukijaribu kujitoa inakuwa ngumu sana watu kukuamini japo watakuwepo wachache watapuuza lakini wengi hawatokuelewa na ukizingatia waafrika wengi hatupendani hapo ndiyo kabisa.
 
Unaikumbuka 'Tamaa mbaya "utunzi wa kichwa Alfe Kabeza kichwa kabisa,ila naskia nae alilogwa akawa kichaa kabisa na kiongozi mmoja wapo wa fm akademia,Sijui hawa wakongo wanapata nn Kwa kuwaloga wenzao ukiangalia maisha Yao Bado ya unga unga mwana
 
Uchawi unafanyika kisiri na mambo ya siri, inawezekana walifanya utafiti kisiri wakaja na majibu ya sirini.
 
Kuna mambo yasikie tu maana likitokea jambo halafu watu wakaanza kukunyooshea kidole wewe hata ukijaribu kujitoa inakuwa ngumu sana watu kukuamini japo watakuwepo wachache watapuuza lakini wengi hawatokuelewa na ukizingatia waafrika wengi hatupendani hapo ndiyo kabisa.
Patcho anapitia kipindi kigumu mno, mchizi wako anafariki na bado tuhuma unapewa wewe
 
Hata Nyoshi El Saadat alisingiziwa kumloga aliyeimba wimbo 'Acha Tamaa.
Wakongo akiwemo hayati Franco na Maseke ya Meme yake wanamini upuuzi huu sana.
 
Wanabodi, nautafuta sana wimbo mmoja wa FM Academia unamhusu yatima (siukumbuki jina) ila una mashairi yafuatayo; "🎼 Heri kwa wale wazazi waliondoka wakawaachia mali, sisi wazazi waliondoka wakatuacha mikono tupu🎵🎶 "

Rhumba moja kali sana bila shaka Malou Stonch akiwa ndani yake.
 
Nyoshi anamtuhumugi Pacho kwa uchawi...na inasemekana pacho anapotoka congo nzima inapaogopa kwa uchawi...siwezi kumsemea mtu ni kweli au si kweli ila nilishangaa!
 
Unaikumbuka 'Tamaa mbaya "utunzi wa kichwa Alfe Kabeza kichwa kabisa,ila naskia nae alilogwa akawa kichaa kabisa na kiongozi mmoja wapo wa fm akademia,Sijui hawa wakongo wanapata nn Kwa kuwaloga wenzao ukiangalia maisha Yao Bado ya unga unga mwana
Hata yule first lady wao alipata kichaa. Somebody Florah
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom