ORODHA YA WATUMISHI WALIOPATA VIBALI VYA UHAMISHO WA KUBADILISHANA VITUO VYA KAZI KUANZIA NOVEMBA,2021 – JANUARI,2022 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Prof.Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa watumishi 1544 wa kubadilishana vituo vya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za MItaa.
Prof.Shemdoe amesema kuwa Ofisi ya Rais –TAMISEMI inaendelea kufanyia kazi uhamisho wa kubadilishana tu kwa sasa na kwa wale walioomba uhamisho usiokuwa wa kubadilishana kuanzia Julai,2021 – Januari,2022 kwenda Halmashauri za Wilaya waendelee kusubiri wakati tathmini kwenye halmashauri zote ikiendelea kufanyika ili kufanya msawazo.
Pia, amewataka watumishi wote wa Mamlaka za Serikali za MItaa waliowasilisha maombi yao ya uhamisho OR-TAMISEMI kwa kipindi cha Januari 2018 – Juni,2021 kuomba upya kuhamia kwenye maeneo hayo ila isiwe kwenye Majiji,Manispaa na Halmashauri za Miji.
Maombi hayo ya uhamisho yazingatie taratibu zote za uhamisho kama ilivyoainishwa kwenye Waraka wa Uhamisho No.2 wa mwaka 2018.
Aidha, amewataka watumishi waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kuja Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo na kuwa orodha ya majina ya watumishi waliopata vibali vya uhamisho inapatikana kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz
Endapo mtumishi atakua na changamoto yeyote asisite kupiga simu kwenye Kituo cha huduma kwa mteja kwa namba za simu: +255735-160210, +255262-160210 ama kuandika barua pepe kwenye anwani yetu ya huduma@tamisemi.go.tz
Imetolewa na Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
30.01.2022
👇👇👇👇👇👇