Nyaisuka Chacha Mohono auawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Serengeti

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
776
2,404
FB_IMG_1713591120390.jpg

Marehemu Nyaisuka Chacha Mohono.

Aliuawa na askari wa wanyamapori 11/03/2024 kwa kupigwa risasi saa nne asubuhi nyumbani kwao kitongoji cha Jerumani, Machochwe, Serengeti.

Askari walifika nyumbani na kutaka kupora ng’ombe ambao walidai kwamba waliingia katika hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park - SENAPA)

Nyaisuka Chacha Mohono akajaribu kuzuia ng’ombe wao wasitolewe zizini (wafugaji watanielewa), ndipo akapigwa risasi na kufariki papo hapo.

Askari wakaubeba Mwili wake na kuupakia katika gari yao na kuondoka nao hadi leo haujapatikana. Muhono alikuwa ni kijana mdogo sana wa miaka 21.

Chanzo: Chadema in Blood
 
Marehemu Nyaisuka Chacha Mohono.

Aliuawa na askari wa wanyamapori 11/03/2024 kwa kupigwa risasi saa nne asubuhi nyumbani kwao kitongoji cha Jerumani, Machochwe, Serengeti.

Askari walifika nyumbani na kutaka kupora ng’ombe ambao walidai kwamba waliingia katika hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park - SENAPA)

Nyaisuka Chacha Mohono akajaribu kuzuia ng’ombe wao wasitolewe zizini (wafugaji watanielewa), ndipo akapigwa risasi na kufariki papo hapo.

Askari wakaubeba Mwili wake na kuupakia katika gari yao na kuondoka nao hadi leo haujapatikana. Muhono alikuwa ni kijana mdogo sana wa miaka 21
Shida sio ikatili, Shida n Elimu tu.
Ipo siku itakuja kutokea vita kali kati police wanyama pori na Raia.
Waziri mwenye Dhamana fanya kazi yko. Kama Alinavyofanya mama yetu #dorithygwajima
 
Sheria haisemi hivyo wewe jua hivyo labda ndio maana Mahakama inadharauliwa sababu ya udogo wa uelewa km wako, yaan uue alafu uubebe mwili alafu ufiche Gari alafu hakuna kesi?
Unathibitishaje kama wameua.

murder weapon

Body.

Motive.

These three things is used to make up the solid case. Otherwise circumstantial cases depends on chain of events and witness narration of the events.

Sasa Namba ya Gari haijulikani, Askari waliouwa hawajulikani, mwili haujapatikana, hiyo kesi unaifunguaje??

Kwa rejea ya Kesi ya Zombe na wenzake, mahakama ilimwachia huru Zombe kwa kuwa aliyetajwa kuua (koplo Sad) hakupatikana kuthibitisha kama kweli alitumwa na Zombe kuua.

Kesi huwa hazifunguliwi Kwa kuegemea tuhuma tu, bali lazima kuwepo na ushahidi usioacha shaka kabisa.

SIJASEMA MAUAJI HAYAJAFANYIKA.
 
Hawa askari wa wanyama pori ni makatili Sana nkikumbuka kipindi cha Operation tokomeza ujangili umafia waliufanya sio powa
Kipindi cha opereshen tokemeza walikuwa wana deal na adui ambae kwa kias kikubwa hawakuwa watz na walikuwa majangili pro max. wengine were caught kwneye fight it was collateral damage, it happens
ila matokeo ya opereshen tokomeza ndio yalikomboa hifadhi ya tarangire, na zingine maana wanyama walikuwa wanaisha kwa kasi
 
Unathibitishaje kama wameua.

murder weapon

Body.

Motive.

These three things is used to make up the solid case. Otherwise circumstantial cases depends on chain of events and witness narration of the events.

Sasa Namba ya Gari haijulikani, Askari waliouwa hawajulikani, mwili haujapatikana, hiyo kesi unaifunguaje??

Kwa rejea ya Kesi ya Zombe na wenzake, mahakama ilimwachia huru Zombe kwa kuwa aliyetajwa kuua (koplo Sad) hakupatikana kuthibitisha kama kweli alitumwa na Zombe kuua.

Kesi huwa hazifunguliwi Kwa kuegemea tuhuma tu, bali lazima kuwepo na ushahidi usioacha shaka kabisa.

SIJASEMA MAUAJI HAYAJAFANYIKA.
Ndio maana nakwambia wewe bado mdogo kwenye Shule ya Sheria, maelezo mengi Ila unachoeleza hakina logic endelea kujifunza mpo field sasa hivi au?
 
Ndio maana nakwambia wewe bado mdogo kwenye Shule ya Sheria, maelezo mengi Ila unachoeleza hakina logic endelea kujifunza mpo field sasa hivi au?
Natumia mantiki tu.... Mimi ni LY.

Unafungua kesi kienyeji tu. Lazima kuwe na msingi wa Kesi. Hapo maelezo hayajitoshelezi.

Unajua ni kwa nini siku hizi inasemwa "ameuawa na kitu chenye kali"?

Nani alikuwepo wakati Nyaisuka anapigwa risasi?? Ilikuwaje akapigwa risasi?

Ni askari yupi hasa aliyempiga risasi Nyaisuka, anafahamika?

Waliuchukua mwili wa Nyaisuka na kuupakiza kwenye gari lenye namba zipi?

Wakati wanauchukua huo mwili kulikuwa na kiongozi yeyote wa serikali ya Kijiji??

Tukio lilitokea muda Gani?

Kesi hazifunguliwi kienyeji.
 
Back
Top Bottom