Njooni tufikirie kidogo hapa

Dkt Mwijuma

Senior Member
Apr 9, 2023
199
568
Nimeona post ya Elon Musk huko X kuwa kampuni yake Starship itaanza kupeleka watu huko Mars.

Nikafikiria jinsi jamaa anavyopata hela kupitia teknolojia huku ana internet (Starlink), huku magari (Tesla), anatengeneza rocket (SpiceX) pia mambo ya ubongo (Neurobrain).

Nikawaza hiviii hata kama ni genius anawezaje kuwaza na kubuni vitu vyote hivyo?, ninavyojua mimi kila mtu ana angle yake ya ujuzi wa mambo inawezekana mtu akawa genius wa hesabu ukampeleka kwenye sanaaa akafeli.

Jibu likawa inawezekana jamaa alikuwa na hela akawakusanya vijana wenye mawazo chanya (ma-genius kweli kweli) ila hawana mitaji ya mawazo yao akawasajili kisha akawaweka sehemu.

Vijana kazi yao ikawa ni kubuni wazo tu jamaa (Elon Musk) anatoa mtaji ila likifanikiwa unapewa hisa kadhaa tu, mradi unakuwa wa jamaa.

Kisha sasa ndio nikawaza tena nimewahi kusikiliza mawazo mengi sana ya wahitimu wa vyuo vyetu vikuu lakini hawana mitaji ya kutumiza, kuna mmoja huyo sikumbuki anatoka chuo gani ila alikuja na wazo la kuweka trafic lights zenye kuhisi (Yaani hata kama inatakiwa kuhesabu sekunde sitini ila kama njia hiyo haina magari na kuna magari njia nyingine inajizima inawaka upande ambapo kuna magari mengi, najua hamtanielewa.

Wazo la kijana huyo kiukweli ni zuri sana lakini sasa kijana mwenyewe hana mtaji, hivi hakuna wafanyabiashara wadhamini kisha waje kupiga hela likifanikiwa? Vipi serikali yetu haiwezi tenga hela ikawalea vijana wote wenye mawazo chanya kisha wakavumbua vitu, mfano silaha jeshini, vifaa tiba, mifumo ya kiuongozi, michezo nk.

Au nyie mnasemaje? Tukijite hapo maana kuna wengine watajikita kufikiria uandishi wangu waone nilipokosea spelling.
 
Africa ni Africa tuu. Hayo mambo yanawezekana sana sema wazungu wana tukandamiza na mikopo ili tusiwe na muda wa kuwaza hayo mambo ya kibunifu badala yake tuwaze kukopa tena na tena na tena kulipa madeni kwa kwenda mbele.
 
Ndugu Yangu, Nchi za Kiafrika Ni za ajabu, Sana Kuna siku nilipata Bahati ya kuandika kitu Fulani kwenye ukurasa wangu wa Fb miaka mingi kuhusu Kija wa Kiafrika kua na uwezo wa kubuni Vifaa vya Kijeshi. Ebana nilishangaa napigiwa Simu. Unachofanya mjuaji.... duuu nilishangaa.
 
Ulitishwa, badala ya kusikilizwa?
 
Africa ni Africa tuu. Hayo mambo yanawezekana sana sema wazungu wana tukandamiza na mikopo ili tusiwe na muda wa kuwaza hayo mambo ya kibunifu badala yake tuwaze kukopa tena na tena na tena kulipa madeni kwa kwenda mbele.
Tunakandamizwaje na mikopo mkuu?
 
Back
Top Bottom