Nina nyumba uswahilini inatengeneza Tsh. 40,000/- kwa mwezi, niendelee au napoteza muda?

Tuo Tuo

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
627
1,088
Najua kuna mnaofanya hii biashara na inawalipa sana. Kama inakulipa basi ni ether;

1. Unapangisha fremu za maduka (kama location n nzuri au barabarani)
2. Wenye apartment katikati ya mji
3. Wenye biashara ya guest/lodge au hoteli

Kwa upande wangu, nina nyumba ndogo sana vyumba 2 na sebule na kimoja cha nje. Nilikinunua hiki kibanda mwaka 2019 kwa milioni 5.

Kipindi hiko sina nyumba nilikurupuka kutaka kumiliki atlest kijumba mjini. Kina sehemu ndogo sana. Yaani huwezi kujenga wala kuendeleza kitu kingine kimebanana sana mahali ilipo imezungukwa na majirani ambao nao kila mmoja amejenga hadi mwisho wa uwanja wake.

Nikaanza kupangisha. Bei za huku kwasababu hamna umeme hamna maji basi bei ni elfu 10.
Sasa kwa hii elfu 10 nawaza hadi sasa 2023 sijafikisha hata laki 3 au 5 niliopokea kwene hiki kijumba.

Natamani kukiuza lakini hakiuziki. Naona hata uvivu kukikarabati maana nitapoteza hela tena.

Nawezaje kuongeza thaman ya hiki kijumba muda unaenda?

Mawazo yanayonijia;
1. Nikifanye guest (changamoto ni kadogo, kako katikati ya uswazi labda nilale mwenyewe).
2. Niweke hata mashine? Sielewi!

Toa ushauri jinsi wewe ulivyoongeza thamani ya nyumba yako, au unavoweza kupiga hela kupitia kijengo.
 
Najua kuna mnaofanya hii biashara na inawalipa sana.Kama inakulipa basi ni ether
1.unapangisha fremu za maduka (kama location n nzuri au barabarani)
2.Wenye apartment katikati ya mji
3.wenye biashara ya guest/lodge au hoteli


NYUMBA YANGU
Nina nyumba ndogo sana vyumba 2 na seble na kimoja cha nje. nilikinunua hiki kibanda mwaka 2019 kwa milion 5.

Kipindi hiko sina nyumba nilikurupuka kutaka kumiliki atlest kijumba mjini. Kinasehemu ndogo sana. yaan huwezi kujenga wala kuendeleza kitu kingine kimebanana sana mahali ilipo imezungukwa na majiran ambao nao kila mmoja amejenga had mwisho wa uwanja wake.

Nikaanza kupangisha. Bei za huku kwasababu hamna umeme hamna maji basi bei ni elf 10.
Sasa kwa hii elf 10 nawaza had sasa 2023 sijafikisha hata laki 3 au 5 niliopokea kwene hiki kijumba.

Natamani kukiuza lakini hakiuziki.
Naona hata uvivu kukikarabati maana nitapoteza hela tena.



Nawezaje kuongeza thaman ya hiki kijumba muda unaenda??


Mawazo yanayonijia
1.nikifanye guest ( changamoto ni kadogo, kako katikat ya uswazi labda nilale mwenyewe)
2.Niweke hata mashine….?? sielewi


TOA USHAURI JINSI WW ULIVOONGEZA THAMAN YA NYUMBA YAKO. au unavoweza kupiga hela kupitia kijengo
Geuza guest bubu ya Short time utanishukuru badae
 
Na wengi wanakurupuka sana.

Uwekezaji kwenye mijengo yahitaji akili.

Kuna watu wanapambana na mikopo wamalizie nyumba wapangishe.

Kama mtu una pesa nyingi na huna pa kuzipeleka zitunze kwenye majumba ila walala hoi wenzangu, usijaribu hii kama ni nyumba yako ya kuishi haina shida ila sio uteseke ujenge nyumba ya kupangisha.

Hesabu za uwekezaji wa nyumba gharama zake zinarudi kwa muda mrefu sana.

Ukijenga nyumba kwa milioni 90 leo hiyo nyumba kuzalisha pesa za kujenga nyumba ingine ya milion 90 itachukua si chini ya miaka 20 au 30. (nazungumzia nyumba za kuishi kwa frame za biashara kama ipo eneo centre ni uwekezaji mzuri).
 
Kama ni eneo kuna watu wengi na wanaendelea kuongezeka haiwezi kukutupa.

1. Nakushauri usiwe na haraka ya kuuza, fanya kama vile hiyo m5 ilipotea hivyo haipo tena.

2. Ipangishe hata kwa hiyo hiyo elfu 10 halafu subiri muda utakupa majibu. Ukarabati mruhusu mpangaji afanye mtakatana kwenye kodi, hata akifanya ukarabati wa kukaa bure miaka 5 usihofu muache ila fanya ukaguzi wa mara kwa mara usiitelekeze.

Nimefanya sio mara moja na mwishoni nilicheka kwa furaha kwa kuwekeza kwenye ardhi.

Unless eneo liwe huko nyantumbi ambapo hapakui pamedumaa.
 
Na wengi wanakurupuka sana.

Uwekezaji kwenye mijengo yahitaji akili.

Kuna watu wanapambana na mikopo wamalizie nyumba wapangishe.

Kama mtu una pesa nyingi na huna pa kuzipeleka zitunze kwenye majumba ila walala hoi wenzangu, usijaribu hii kama ni nyumba yako ya kuishi haina shida ila sio uteseke ujenge nyumba ya kupangisha.

Hesabu za uwekezaji wa nyumba gharama zake zinarudi kwa muda mrefu sana.

Ukijenga nyumba kwa milioni 90 leo hiyo nyumba kuzalisha pesa za kujenga nyumba ingine ya milion 90 itachukua si chini ya miaka 20 au 30. ( nazungumzia nyumba za kuishi kwa frame za biashara kama ipo eneo centre ni uwekezaji mzuri).
Tatizo wengi wakipata hela huwaambii kitu ukimshauri anaona kama unamchawia tuu hela zake.
 
Back
Top Bottom