Jesus37
Member
- Feb 9, 2023
- 80
- 82
uongo na vitisho hizo story zahovyo tu.! yesu alikua mtu wa taifa gani.? kwani hakuna naabii mswahili kwenye hivyo vitabu vyadini.? kwanin manabii wote watoke eneo moja tu.?mwanadamu ni roho, hiyo ndiyo itakayohukumiwa, mwili huu ni mavumbi tu, hivyo hata mwili huu ukifa roho huwa haifi, huwa inaenda mahali pale unapostahili,kama ulimpa Yesu Maisha utaenda mbinguni kama haukumpa Yesu maisha ni motoni. Nakushuhudia hii leo kwamba, mimi sio mchungaji, wala nabii wala yeyote, ni mtu wa kawaida kabisa, ila Mungu amenifanya niyasema yale ambayo yatawafanya wengi wapone, ni sauti ya Mungu, anaweza kutumia yeyote hata mtu asiyefaa kama mimi, mtu aliyehurumiwa kama mimi, mtu aliyekuwa mwenye dhambi, aliyekuwa mzinzi, aliyekuwa zurumati aliyekuwa wa ajabu ajabu kama mimi, ananitumia kuwaletea hii habari njema.
ya kwamba Yesu Kristo alikufa akalipa garama ya dhambi na ukombozi kwa ujumla kwa mwanadamu, akaweka hiari mbele yetu, ukitaka kupona mwamini na kabidhi maisha kwa Yesu aliyelipa deni la dhambi sasa, na kama hautaki, ni hari yako, baki katika dhambi ila kuna siku atakuwa kuihukumu hii dunia, watu wataungua moto.
wale waliopotosha wengi wataungua moto pia, manabii wa uongo mliosababisha hadi watu hawaokoki kwa sababu ya utapeli wenu, mtakunywa kikombe cha haki sawasawa na yale mliyoyatenda. pia hata ninyi mnaolisikia sauti ya wokovu na mnakuwa na mioyo migumu, hamtakuwa na la kujitetea kwasababu mlishasikia mkakataa kwa kisingizio ati wapo manabii wa uongo duniani. sasa manabii wa uongo hata Yesu alisema watakuwepo, kwahiyo unataka ukaungue moto pamoja nao au wewe unataka uokoke binafsi? mimi sihitaji sadaka, huwa sipokei sadaka, sina kanisa sina chochote, ila ujumbe huu nashukuru kwamba umekufikia na nimenawa mikono. unamhitaji Mungu zaidi ya vile unavyoelewa, usisubiri upate shida ndio umrudie, sasahivi wakati amekujalia uzima mrudie yeye, muda ungalipo,nafasi ingalipo. ukiona mtumishi yeyote amefanya dhambi, usimfuate yeye fuata Neno la Mungu kwasababu kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, wewe utabeba wa kwako, na manabii wa kwao, ila Neno la Mungu linakutaka uokoke, mpe Yesu Maisha ili upone hukumu ya milele. Mungu akusaidie.