Nilichobaini kwa watu wa Njombe

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,968
6,741
Mimi siyo mrefu wala mfupi, lakini naweza nikawa mrefu kwa watu wengi wa Njombe!

Kwa siku chache nilizokaa Njombe, nilibaini ukweli kuwa ukubwa wa mwili hauamui "ukubwa" wa mtu. Anaweza akawa na umbo dogo sana lakini akawa ni mtu "mkubwa" sana.

Watu wengi wa Njombe wana maumbo madogo, unaweza kusema ni watu wafupi. Lakini akili zao na utu wao si "mfupi".

Kwa niliyoyashuhudia, nilihitimisha kama ifuatavyo kuhusu watu wa Njombe:

1. Ni watu wanaojikubali! Wamerkdhikia na maumbo yao ya kuzaliwa. Hawahangaiki kuwa kama "wengine" kimwonekano.

2. Ni watu wastaarabu sana, na wakarimu pia. Hata ukimwuliza mtu njia, anakuelekeza kwa upendo utafikiri unamlipa.

3. Ni wajasiri sana. Si wanaume wala wanawake. Wanajua kusimamia kile wanachokiamini.

Nakumbuka, tukiwa stendi kuu ya mabasi tukiwa tunataka kwenda Ludewa, wamama fulani waligoma kulipa nauli kabla gari halijaanza safari. Walikuja kulipa baada ya gari kutoka stendi. Si kama wamama wa mikoa fulani ambao wakikoromewa tu kidogo na konda "wanahanya" utafikiri huo usafiri wamepewa msaada.

Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.

Walitoa sababu mbili za kukataa kwao:
A). Wamelipa nauli hivyo ni jukumu la watoa huduma kutafuta namna ya kuwafikisha wanakoenda kama tiketi inavyoonesha

B). Pale kuna vijana wanaoweza kuifanya hiyo kazi hivyo kondakta awalipe vijana waliopo eneo hilo ili waitie hiyo huduma.

Walisimama na huo msimamo mpaka wahudumu wa basi walipojiongeza na hatimaye basi kukwamuliwa.

Lakini hao watu si wakatili. Wana upendo mno. Siku iyo hiyo, wakati tukiendelea na safari, mmoja wa abiria aliugua njiani. Abiria walionesha ushirikiano wa hali ya juu katika kumpatia huduma ya kwanza hadi alipofikishwa hospitalini kwa basi ilo hilo.

4. Ni wachapa kazi sana. Kule kuna wenyeji wenye mashamba makubwa ya parachichi na miti ya mbao na nguzo. Inaonekana kuna mabilionea japo hawapigi kelele.

5. Ni watunzaji wa mazingira. Hata stendi yao ya mabasi, ukiiangalia, inavutia sana. Ina ukijani mzuri ambao umetokana na kupata matunzo stahiki.

Kwa kifupi, watu wa Njombe ni wajasiri, wakarimu, wastaarabu, wanajikubali, wachapa kazi na matajiri wasio na makelele.

Aliyewahi kuwa Mbunge maarufu kipindi cha utawala wa Kikwete, marehemu Deo Filikonjombe alikuwa Mbunge wa Ludewa. Ni zao la Njombe.

Sishangai kwa nini alikuwa jasiri! Ni asili ya watu wa Njombe.

Hongereni watu wa Njombe👏👏👏

Keep it up!
 
umesahau kitu kimoja, njombe kuna ushirikina balaa.
Mwenzako ameandika vitu vinavyoonekana wewe unaleta habari za kufikirika.

Ni wajinga wachache kama wewe ndio wanaamini mambo ambayo ukiambiwa thibitisha unaishia kutoa macho kama mjusi kabanwa na mlango.

Mimi ni mzawa wa Njombe huwa nashangaa wajinga wanaokomaa kuongelea habari ambazo kiuhalisia hazipo.
 
Nimewahi kufika huko

Jamaa ni kawarimu sana

Halafu chakula sio shida kule, ukifika na njaa zako za DSM utakula hadi upasuke tumbo 😅🙌

Usisahau pana maambukizi makubwa sana ya HIV/ Ukimwi

Hivyo ukiopoa vaa Kondomu, tumia kilainishi piga kimoja cha Afya ujilalie zako Usingizi

Ukijifanya unajua sana romance, hata kama utakuwa umevaa Kondomu lazima uondoke na mgeni wa Kaptaini Komba
 
Back
Top Bottom