Ni wakati wa Musonda kuondoka Yanga

Escotter20

JF-Expert Member
Jul 20, 2020
471
861
Yanga inapaswa kufikiria kuachana na Kennedy Musonda.

Tokea aje hapa nchini, Musonda hajatoa kile kilichotegemewa kwa 100%. Ni mchezaji mzuri sana, lakini yapo yanayofikirisha juu yake.

Musonda hana muendelezo mzuri. Ni michezo michache sana amecheza kwa kiwango cha juu, iliyosalia anakuwa wa kawaida tu au kushindwa kutoa kitu chenye tija.

Nadhani, Yanga SC inapaswa kufikiria kumleta mchezaji bora zaidi yake. Ili timu kama timu ipige hatua kwenda mbele. Sio dhambi. Al Ahly iliwasajili Ahmed Kendouci, Walter Bwalya, na wakawaondoa haraka.. baada ya kuonekana hawaisaidii timu kwenda mbele zaidi.

Yanga SC wanapaswa waangalie mchezaji bora zaidi ya Musonda. Ili aje akisogeze mbele kikosi kutoka hapa kilipo na kuwa tishio zaidi hapa AFRIKA.
 
Musonda abaki shehe, huwezi kumtimua musonda ili hali hauna mbadala wa kueleweka, huoni pacome alivyo umia imebidi musonda awe anacheza upande wa pacome wanapokezana na mzize, utamtoa wapi striker anaekaba na kushambulia kama musonda? Mfano wangemtimua alafu mbadala wake akawa konkon yangetukuta yale yale ya simba na akina bareke
 
Musonda Ana mchango , kasi yake ya kuanzisha mashambulizi , kuzuia , ni mchezaji anaejituma uwanjani , Hata asipofunga anaweza kutoa assist , angalia assist aliyotoa kwa Pacome goli la kusawazisha dhidi ya Al ahly .

Mtu wa kuondoka ni mwamnyeto , Hata goli la Fred mwamnyeto haku cover nafasi yake vizuri baada ya kutoka Yao .
 
Umeongea vizuri, kwanza huyo mshambuliaji mwingine anatoka wapi angetuambia.
 
Yanga inapaswa kufikiria kuachana na Kennedy Musonda.

Tokea aje hapa nchini, Musonda hajatoa kile kilichotegemewa kwa 100%. Ni mchezaji mzuri sana, lakini yapo yanayofikirisha juu yake.

Musonda hana muendelezo mzuri. Ni michezo michache sana amecheza kwa kiwango cha juu, iliyosalia anakuwa wa kawaida tu au kushindwa kutoa kitu chenye tija.

Nadhani, Yanga SC inapaswa kufikiria kumleta mchezaji bora zaidi yake. Ili timu kama timu ipige hatua kwenda mbele. Sio dhambi. Al Ahly iliwasajili Ahmed Kendouci, Walter Bwalya, na wakawaondoa haraka.. baada ya kuonekana hawaisaidii timu kwenda mbele zaidi.

Yanga SC wanapaswa waangalie mchezaji bora zaidi ya Musonda. Ili aje akisogeze mbele kikosi kutoka hapa kilipo na kuwa tishio zaidi hapa AFRIKA.
Zamani hata mm nilikuwa nawaza kama wewe. Ila baada ya kumfatilia nikagundua jamaa ni muhimu kuliko maelezo. Unahitaji jicho la 3 kujua umuhimu wa musonda. kwa jicho la kawaida utamchukulia poa.
 
Musonda Ana mchango , kasi yake ya kuanzisha mashambulizi , kuzuia , ni mchezaji anaejituma uwanjani , Hata asipofunga anaweza kutoa assist , angalia assist aliyotoa kwa Pacome goli la kusawazisha dhidi ya Al ahly .

Mtu wa kuondoka ni mwamnyeto , Hata goli la Fred mwamnyeto haku cover nafasi yake vizuri baada ya kutoka Yao .
Hata goli la Aziz K Vs Mamelodi ni juhudi za Musonda, na kwa wale watu wa Imani haijawahi kutokea Musonda akafunga goli Yanga ikapiteza hio mechi
 
Zamani hata mm nilikuwa nawaza kama wewe. Ila baada ya kumfatilia nikagundua jamaa ni muhimu kuliko maelezo. Unahitaji jicho la 3 kujua umuhimu wa musonda. kwa jicho la kawaida utamchukulia poa.
Musonda anatupa vitu vingi Kwa wakati mmoja mshambuliaji sio lazima afunge mkiwa na Musonda uwanjani mnakua na wachezaji kumi na moja kamili uwanjani sababu anakaba, anatengeneza nafasi kwa wengine na pia anaweza kufunga..
 
Musonda abaki shehe, huwezi kumtimua musonda ili hali hauna mbadala wa kueleweka, huoni pacome alivyo umia imebidi musonda awe anacheza upande wa pacome wanapokezana na mzize, utamtoa wapi striker anaekaba na kushambulia kama musonda? Mfano wangemtimua alafu mbadala wake akawa konkon yangetukuta yale yale ya simba na akina bareke
Nakubaliana nawe...kuna ile mechi na Mamelodi ya marudiano alijitoa mno
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom