Ni wakati sasa Makaburi ya Kinondoni yawe Makumbusho

Baraka DSM

Member
Sep 12, 2017
68
74
Habari waungwana!

Sisi tuliowapumzisha wapendwa wetu hivi karibuni makaburi ya Kinondoni tumeona ni jinsi gani ilivyo ngumu hata kupita katikati ya makaburi mengine. Kiufupi eneo lile limejaa halipaswi kuendelea kuwa sehem ya kupumzisha wapendwa wetu.

Ushauri wangu-
1. Serikali ifunge eneo Lile na kuwa makumbusho.
2. Serikali ipanue eneo kwa kuwalipia fidia majirani Ili lipatikane eneo kubwa zaidi la kuwapumzisha ndugu zetu. Kuanzia ghorofa la Abasi Tarimba kushuka mpaka chini walipwe fidia lipatikane eneo kubwa la kuzikia kwa miaka kumi ijayo.
 
Mleta mada kama sijakuelewa vizuri, yaani kutoka ghorofa la Tarimba kushuka chini kuja makaburini, nyumba zote zibomolewe halafu serikali ilipe fidia kwa kila nyumba kwasababu ya makaburi?

Yaani serikali iingie hasara ya mabilioni kwa sababu ya makaburi? Kwani mapori yote hayo yaliyowazi hamuyaoni?
 
Back
Top Bottom