Ni sawa kupostiwa na MC bila ridhaa yako ukiwa unaburudika kwenye sherehe?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,860
Nilienda kwenye mualiko wa sherehe ya rafiki yangu kuna dada yake alikuwa anaolewa, nikiwa najimwagia moyo na bia kadhaa ukafika muda wa kwenda kusakata rumba, mzuka niliokuwa nao ulikuwa fire 🔥💥 bum shakarakah! 💥🔥Nikajivuta hadi sehemu ya tukio na nikaanza manjonjo yangu kujiachia kwa 'confidence' kama yote. Uchezaji wangu uliibua shangwe kwa namna ya kipekee nilivyolisakata.

Nimerudi kwangu najua tayari yashapita hayo, sasa naja kushangaa kuna MC wa tukio nimeambiwa kanipost kwenye kurasa yake ya Insta, nimeingia huko na kweli nimejiona! Najiuliza kulikuwa na umuhimu gani kunipost huko bila ridhaa yangu muhusika?

Hata bar, club ama pub watu huwezi kuwakuta wanapostiana hovyo hovyo wakiwa wanafurahia starehe zao, iweje hawa ma MC wanatupost hovyo hovyo?
 
Pole sana ila mimi mwenyewe ni confess napenda kutazama page za ma-mc kuna warembo wa kila aina wanapostiwa wakiserebuka miziki. Ila kumpost mtu kutangaza biashara yako bila idhini yake ni kuingilia faragha na kumtumia mtu kibiashara bila idhini yake, ukiumizwa sana mshitaki akulipe fidia.
 
Kumbe ulikonga nyoyo za watu ndio maana jamaa akaamua kukupaisha. Kwenye jumuiya epuka kufanya kitu tofauti zaidi ya wengine la sivyo unajianika na kuwa man/woman of the event
Yeah mkuu unakuwa tayari umejipambanua from the rest, kwenye hizi public events usijisahau kuwa kuna maisha baada ya hapo, always enjoy na fanya hivyo within line, kinyume cha hapo utageuka na kuwa public figure!
 
Kumbe yule ni wewe. Mzee unakata mauno na una kiuno laini kuliko hata cha Ray C. Nimeiona ile Video. Ulikuwa umevaa suruali ya jeans imekutaight huku imechanika chanika magotini na imeandikwa "Konde boiii" halafu umevaa fulani ina picha ya "Daimond" kwa mbele na Mgongoni imeandikwa "Wasafi beibiii". Nimekuona kwa yule MC, ulijifunga kanga kiunoni na ukaanza kumwaga mauno balaaaaaaa.
 
Kuna video moja nimesave pisi inakatika zaidi ya umeme wa TANESCO kwenye hizo harusi. Ma-MC kazi iendelee
 
Jibu ni siyo sawa. Na hiyo siyo public event kama wanavyosema. Maana shughuli iko resteicted kwa watu fulani tu. Ndo masna watu wanaingia kwa kadi.

Next time unafanya shughuli atangaza kabisa kuwa ni marufuku mtu kupiga picha isipokuwa ma camera man walioandaliwa. Pia mwambie MC ni marufuku kupost picha za tukio kwenye social media.

Shubamit.
 
Kumbe yule ni wewe. Mzee unakata mauno na una kiuno laini kuliko hata cha Ray C. Nimeiona ile Video. Ulikuwa umevaa suruali ya jeans imekutaight huku imechanika chanika magotini na imeandikwa "Konde boiii" alafu umevaa fulani ina picha ya "Daimond" kwa mbele na Mgongoni imeandikwa "Wasafi beibiii". Nimekuona kwa yule MC, ulijifunga kanga kiunoni na ukaanza kumwaga mauno balaaaaaaa


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ulikonga nyoyo za watu ndio maana jamaa akaamua kukupaisha...! Kwenye jumuiya epuka kufanya kitu tofauti zaidi ya wengine la sivyo unajianika na kuwa man/woman of the event
Ukute bosi wako anapenda kuangalia yalojiri mitandaonii, mara vuuu bin vuuu anakuona unavyoserebuka ili hali kazini we ni kilaza fulaniii iviiiii
 
Back
Top Bottom