Ni sahihi Serikali kutumia viwanja na kumbi za CCM kufanya mikutano ya kiserikali? Hii siyo kinyume na sheria za manunuzi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,249
Viwanja vya mpira vilivyojengwa na wananchi miaka mingi vilibadilika na kuwa mali ya chama cha mapinduzi. Baadhi ya viwanja hivyo ni Karume stadium Arusha na CCM kirumba Mwanza.

Serikali imekuwa na kawaida ya kutumia viwanja hivi kwa shughuli za serikali ikiwemo Mei Mosi. Lakini katika maeneo ya mikoa yapo maeneo ya wazi yanayomilikiwa na serikali ambayo yangeweza kutumika.

Kwa upande mwingine pia zipo kumbi za watu binafsi na makampuni ambayo yangeweza kushindanishwa na wakishinda basi kumbi zao zikatumika.

Kwa hali napenda kufahamu ni sahihi serikali kukodi viwanja hivi kwa shughuli za serikali bila kuzishindanisha? Ni sahihi kuacha kutumia maeneo ya wazi yasiyohitaji gharama za kukodi na kwenda kulipia viwanja vya chama?

Je, sheria ya manunuzi inaruhusu hiki kinachoendelea?

Au chama cha mapinduzi huwa wanavitoa hivi viwanja vitumike bure? Nimeona baadhi ya viwanja ufanyiwa ukarabati kwa gharama za serikali; je uidhinishaji wa gharama hizo ufuata taratibu gani?

Kwanini fedha za walipa kodi zikakarabati viwanja vya chama? Mikataba ya ukarabati na uwekaji wa nyasi usainiwa na nani?
 
Baadhi ya viwanja hivyo ni Karume stadium Arusha na CCM kirumba Mwanza.
Viwanja vya mpira vyote ukiondoa vya watu binafsi ni vya CCM hadi Open space ukiondoa za watu binafsi za kupaki Magari ni Mali za CCM
 
Back
Top Bottom