Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Hakuna kitu maana Waislam, Wakristo na Wayahudi ni watu wa vitabu na wanaamini Mungu
Ukichukua kisu kikali na kumchinja shingoni moja kwa moja kwa kutamka kwa kuanza na jina la Mungu basi hiyo nyama wote wanaweza kula
Ila asiwe kibudu au kumuuwa kwa njia tofauti na hivyo
Dini sio ngumu hivyo kama ukisoma na sio vibaya kusoma na za wengine kuongeza maarifa
Ila naona kuna watu wanapotosha wakati sheria zipo
Umepotosha
 
Kuna siku jamaa alikuja home ndo tuko mezani tunapata msosi na kulikuwa na kuku. Mimi nikamkaribisha mwana na nikampakulia kabisa na vipande vya kuku, alishukuru tu ila alikula mboga za majani hakugusa kabisa ile nyama ya kuku. Sikumuona wakati akila so sikujua kama hakula badae naangalia mezani nakuta ile mboga iko vilevile ilibidi nimuulize vipihutumii kuku siku hii ndo akanishtua suala la kuchinja aisee nilistaajabu
 
Waislam ni watu wa ajabu sana,wenyewe hawataki kula nyama iliyochinjwa na Mkristo,sasa sijui wanadhani wakristo ndio wanapenda kula mnyama aliye chinjwa na Muslims?
Wapi imekatazwa nionyeshe kweny maandiko? Mzogo na kibudu ni haramu
 
Nyama ambayo imechinjwa kwa njia sahihi haina tatizo , ila kuna ile mifumo kama wanavyochinja nguruwe wanamuua kwanza kwa magongo halafu ndio anachinjwa kifupi ni kibudu :D .

Kunyanyasa wanyama kwa kuwaua kwanza ndio uchinje yaani washakufa hata damu haitembei, wale kuku wa sigida wengi wanakuwa wamekufa yaani kibudu halafu ndio wanachinjwa hii haifai kwa mtu wa dini yoyote ile.
 
Jibu swali kwanza, mkienda hotelini kabla ya kuletewa MENU huwa mnauliza kwanza Mchinjaji ni wa dini ipi?
Nakuuliza wewe kibudu na mzogo ni halali kula? Hata wale hadzabe wanajua huu mzogo ni wa fisi na hiki ni kibudu
 
Kibudu ni nini? Naomba tuanzie hapo
kibudu ni mnyama aliyekufa ..Hakuna dini inayoruhusu kula kibudu wala wanyamapori labda Fisi tu.


Nyamafu ni nyama ya mnyama aliyekufa (kibudu) bila kuuliwa kwa asili (yaani kuchinjwa). Mungu aliwakataza wana wa Israeli katika agano la kale wasile nyama ya mnyama yoyote aliyekufa bila kuchinjwa..

Walawi 17: 15 “Tena kila mtu atakayekula NYAMAFU, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.
16 Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake”.
 
Je ukimpiga risasi mnyama pori kama Mbogo akafa ndio ukachinja hii nayo ni kibudu ?.......maana kumpata akiwa hai ndio umkate shingo sio rahisi.
Unatakiwa umuwahi kumchinja kabla hajafa, hata hivyo kama muwindaji ni muislamu na alipiga Bismillah kabla ya kumtandika risasi huyo mnyama basi ni Hali kumla
 
Kidini ipi?
Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
 
Back
Top Bottom