Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
Kwa mwislam anae jiekewa wala hawezi kula hata ukimkaribisha
 
Muislam anaruhusiwa kula alichochinja asiyekuwa Muislam. Ila tu mchinjaji awe amechinja kweli. Wasio waislam wana tabia ya kuwapiga wanyama au kuku wanamtumbukiza kwenye maji moto anakufa kisha wanaanza kumkata kata. Muislam hali kibudu tu, kitu ambacho hakikuchinjwa. Kama umechinja vizuri kabisa yafaa kula.
Mgh, sio kweli acha kupotosha
 
Kwani huwa wanamwua kwa kutumia rungu? Nafikiri wanaotumia rungu ni kwa ajili ya kuwafanya kuwa wapole ili wawakate shingo kirahisi.

Mimi nimeshuhudia mara moja nguruwe amichinjwa. Hawakutumia rungu. Alikatwa nyuma ya shingo kwa panga hadi kichwa kikatenganishwa na kiwiliwili.
Nimeshashuhudia nguruwe anapigwa bonge la rungu kichwani, akishatepeta anakatwa katwa.
 
Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
Bila picha huu Uzi Ni batili..
 
Muislam anaruhusiwa kula alichochinja asiyekuwa Muislam. Ila tu mchinjaji awe amechinja kweli. Wasio waislam wana tabia ya kuwapiga wanyama au kuku wanamtumbukiza kwenye maji moto anakufa kisha wanaanza kumkata kata. Muislam hali kibudu tu, kitu ambacho hakikuchinjwa. Kama umechinja vizuri kabisa yafaa kula.
Si hivyo tu, muislam anatakiwa kula nyama iliyo chinjwa kwa jina la Allah mkristo hana hivyo.🤔
 
Kuna mmoja alikuja kwangu akatengewa ugali na nyama ya Bata halafu akaanza kuhoji ooh samahani bro kwani nani kachinja huyu Bata nikamwambia Mimi akasema basi Mimi nimeshiba naomba maji tu ninawe nikamwambia jaba lile pale na kikombe kipo hapo nawa tu maana alishafinyanga tongue mbili halafu nikamsindikizia na Aya moja ya suratul qaafiroon
LAKUM DEENUKUM WALIYA DEENI.
😂😂😂😂
Sielewi upumbavu mimi
 
Back
Top Bottom