KWELI Mtu akikung'ata anaweza kukusababishia madhara makubwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimerudi tena kwenu wataalamu wa JamiiCheck,

Eti ni kweli mtu akikung'ata wakati akiwa na hasira basi anatengeneza sumu kama vilivyokuwa kwa wanyama (kama nyoka) na hivyo inaweza hata kukuua, kwa kutegemeana na jinsi hasira yake ilivyo kali?

1714520639798.png

Hii ni kweli wataalam?
 
Tunachokijua
Kung'ata kwa binadamu ni kitendo cha mtu mmoja kutumia meno yake kwa makusudi au bahati mbaya kugusa ngozi ya binadamu mwenzie na kusababisha jeraha au maumivu kwa mwenzie. Kitendo hili huweza kusababisha jeraha au maumivu kutegemea nguvu ya mtu aliyoitumia wakati wa kung'ata. Vitendo vya kung'ata hufanywa zaidi na watoto wadogo hasa pale wanapokuwa na hasira au kutaka kupambana na jambo linalomuudhi.



1714516805837-png.2977876

Kumekuwa na hoja ya kijamii inayoeleza kuwa kung'ata kwa binadamu ni kitendo hatari na chenye kuzalisha sumu nyingi ikiwa muhusika anayeng'ata akifanya kitendo hicho akiwa na hasira.

Upi ukweli kuhusu hoja hii?
JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali ikiwamo Tovuti ya Cleveland Clinic na Tovuti ya VeryWell Health ambao wote wanaeleza namna kung'atwa na binadamu kulivyo hatari. Maandiko yao yanafafanua kuwa kitendo cha binadamu mmoja kumng'ata mwingine kinaweza kuchukulia kawaida lakini kinaweza kuwa na madhara makubwa yasiyotarajiwa.

Cleveland Clinic
wakieleza madhara ya kung'atwa na binadamu wanafafanua kuwa meno na kinywa cha mtu hubeba bakteria wengi. Ikitokea binadamu mmoja kamng'ata mwingine na kusababisha jeraha, bakteria wa kwenye meno huweza kuingia ndani ya kidonda na kusababisha madhara makubwa bila kutarajia. Wanasema:

Maajeraha ya kuumwa na meno ya binadamu mwenzako yanaweza kuwa hatari zaidi kuliko unavyotarajia. Kuna vijidudu huishi katika mate ya mdomo wa binadamu vinaweza kuongeza hatari yako ya kupata maambukizi. Jeraha la kung'atwa linaweza kuonekana dogo, lakini maambukizi ya bakteria yanaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.
1714520284321-png.2977889

Picha: Mkono wa mtu ulioathiriwa na Bakteria baada ya kung'atwa (Chanzo kutoka Google)​
Takwimu zinaeleza kuwa nchini Marekani Watoa huduma za afya hushughulikia kesi takriban 250,000 za kung'atana kwa binadamu. Kati ya watoto wanaong'atwa na wenzao 10% kati yao hupata maambukizi kutokana na bakteria zilizopo kwenye mate ya binadamu. Hata hivyo, 3% ya kesi hizo hufikia kuhudumiwa kwenye vitengo vya uangalizi maalumu.
Nao, VeryWell Health hawatofautiani na Cleveland Clinic ambao katika makala yao wamehimiza watu kutopuuzia majeraha ya kung'atana binadamu kwa binadamu kwani japo yanachukuliwa kawaida lakini yamekuwa na madhara makubwa. Sehemu ya makala yao inaeleza:

Kung'atwa na binadamu ni hatari zaidi kuliko inavyochukuliwa. Hatari hii hutokana na idadi kubwa ya bakteria wanaoishi kinywani mwa mtu, kuumwa na binadamu kunaweza kusababisha maambukizi makubwa.
Baadhi ya dalili zinazoashiria jeraha la kung'atwa limeingia bakteria ni pamoja na kidoda kuwa na wekundu, kupata uvimbe, joto, maumivu, na kutoka kwa usaha. Namna ya kufanya huduma ya kwanza inapotokewa umepata jeraha la kung'atwa unapaswa kuosha eneo lililong'atwa kwa maji safi. Ikiwa jeraha likiwa linatiririsha damu au kuonesha dalili mbaya muone mtaalamu wa afya kwa matibabu zaidi.
Kwa ujumla maandiko yote mawili yanaeleza madhara yanayoweza kupatikana inapotokea mwenzako kakung'ata. Maandiko yanaonesha kuwa madhara ya kungata yanategemea zaidi kiwango cha bakteria kilichopo kwa mng'ataji haijalishi akiwa amefurahi au kuchukiaa

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom