Ni kwanini waganga wa jadi wanazikwa wamekaa kwenye kiti au kigoda

GOLD BOY

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
388
472
Naombeni kujuzwa ni kwanini waganga wa kienyeji wanazikwa wakiwa wamekaa kwenye kiti pia makaburi yao ni mviringo kama kisima, mwenye uelewa ni kwanini anijuze.

Na je ikitokea amezikwa kawaida nini kitatokea?

Lakini pia kwanini wanatupa kaburini kinyesi cha ngombe kabla ya kumfukia
 
Ntuzu kule si waganga akina Mayuma tu bali hata watemi na mamanju wakubwa (nao huishia kuwa waganga) akina Ng'wanalūselele, Ng'uchayūlo, Chūlichūli, Lūkalasonda, Ng'wanabahaile, Pilipili, Tūlantwe, Magūlūmangū, Ng'hwebele, Kamongo, Kejekeje; na wengineo - karibia wote walizikwa wakiwa wamekaa.

Sababu yake ni kwamba uganga, umanju na utemi vinarithishwa; na inaaminika kwamba mkimzika marehemu kwa kumlaza basi mnakuwa mmelaza kila kitu na hiyo inaashiria kwamba hakuna mtoto wala mjukuu atakayerithi huo uganga, utemi na umanju. Ukikuta mganga, mtemi au manju amezikwa kwa kulazwa basi hiyo ni ishara kwamba uganga, utemi na hata umanju wake ndiyo umefikia kikomo na hakuna atakayemrithi!

Kuzikwa akiwa amekaa pamoja na matambiko yanayoambatana na mazishi hayo ni ishara ya mamlaka kwamba kila kitu bado kiko sawa na umanju, uganga na utemi huo utaendelea kurithishwa katika ukoo huo kwa vizazi vijavyo.

Na haishii hapo tu bali mganga au manju akifa, waganga na mamanju wengine hawaruhusiwi kuhudhuria mazishi yake maana mazishi hayo huambatana na matambiko na hekaheka nyingi kiasi kwamba mhudhuriaji anaweza kuacha kila kitu pale na uganga/umanju wake ukafia pale pia. Inasemekana hata mganga au manju awe na madawa makali ya kinga kiasi gani, kwenye mazishi ya mwenzake hizo kinga huwa hazifanyi kazi (sigatabūlagwa) na anaweza kuuliwa na waganga, mamanju wenzake na hata wachawi wanaomuwinda kwa urahisi tu. Hivyo waganga na mamanju wengi huwa hawahudhurii mazishi ya wenzao!

Kuhusu kaburi kuwa duara nadhani dhana ni ile ile. Kama alivyosema Archimedes, duara ni umbo timilifu na halina mwanzo wala mwisho bayana. Ni mwendelezo usio na kikomo wala kona kona; na mikunjo - kiashiria kwamba uganga, umanju na utemi/uchifu huo utaendelea bila kipingamizi.

Kinyesi cha ng'ombe sijui ila nadhani ni ishara tu ya utajiri na fahari aliyokuwa nayo marehemu - na kwa wale watakaokuja kurithi mikoba yake. Ndiyo maana mbali na kinyesi tu wengine hupulizia (gūhuha) maziwa mabichi ya ng'ombe (mabele masūnga) kaburini ili marehemu aende vizuri na kwa furaha. Kumbuka kuwa kwa Wasukuma, kama ilivyo kwa makabila mengine mengi ya Kiafrika, maisha hayana kikomo. Ukifa unakuwa mzimu na bado utaendelea kuhusiana na walio hai kwa kuendelea kuwabariki, na hata kuwatesa. Vitu kama pombe za kienyeji, maziwa, mavi ya ng'ombe, nyama n.k. hutumiwa sana katika matambiko ili kuifurahisha mizimu ili ifurahi na kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wanajamii (mf. Ukame, ugumba, magonjwa, umasikini, mikosi n.k)

Kuna tasnifu ya umahiri katika Theolojia ya Kiafrika (Masters in African Theology) inagusia mambo haya. Nikilikumbuka jina la mtafiti na title yake kamili nitakuja kuiweka hapa. Iliandikwa na mtafiti kutoka Ujerumani kama sikosei. Hii niliisoma zamani sana (mid 60s)!

Hata kitabu mashuhuri cha mmishenari wa Kibelgiji Placide Tempels kiiitwacho Bantu Philosophy kinagusia baadhi ya haya mambo japo utafiti wake ulihusisha jamii za Kongo lakini mambo mengi ni yale yale tu maana mwafrika ni mwafrika tu. Hekaheka zake nyingi zinafanana!😁😁😁

Screenshot_20240518_215957_Samsung Internet.jpg
 
Ntuzu kule si waganga akina Mayuma tu bali hata watemi na mamanju wakubwa akina Ng'wanalūselele, Ng'uchayūlo, Chūlichūli, Lūkalasonda, Ng'wanabahaile, Pilipili, Tūlantwe, Magūlūmangū, Kamongo, Kejekeje; na wengineo - wote walizikwa wakiwa wamekaa.

Sababu yake ni kwamba uganga, umanju na utemi vinarithishwa; na inaaminika kwamba mkimzika marehemu kwa kumlaza basi mnakuwa mmelaza kila kitu na hiyo inaashiria kwamba hakuna mtoto wala mjukuu atakayerithi huo uganga, utemi na umanju. Ukikuta mganga, mtemi au manju amezikwa kwa kulazwa basi hiyo ni ishara kwamba uganga, utemi na hata umanju wake ndiyo umefikia kikomo na hakuna atakayemrithi!

Kuzikwa akiwa amekaa pamoja na matambiko yanayoambatana na mazishi hayo ni ishara ya mamlaka kwamba kila kitu bado kiko sawa na umanju, uganga na utemi huo utaendelea kurithishwa katika ukoo huo kwa vizazi vijavyo.

Na haishii hapo tu bali mganga au manju akifa, waganga na mamanju wengine hawaruhusiwi kuhudhuria mazishi yake maana mazishi hayo huambatana na matambiko na hekaheka nyingi kiasi kwamba mhudhuriaji anaweza kuacha kila kitu pale na uganga/umanju wake ukafia pale pia. Inasemekana hata mganga au manju awe na madawa makali ya kinga, kwenye mazishi ya mwenzake hizo kinga huwa hazifanyi kazi (sigatabūlagwa) na anaweza kuuliwa na waganga, mamanju wenzake na hata wachawi wanaomuwinda kwa urahisi tu. Hivyo waganga na mamanju wengi huwa hawahudhurii mazishi ya wenzao!

Kuna tasnifu ya umahiri katika Theolojia ya Kiafrika (Masters in African Theology) inagusia mambo haya. Nikilikumbuka jina la mtafiti na title yake kamili nitakuja kuiweka hapa. Iliandikwa na mtafiti kutoka Ujerumani kama sikosei.
Kumbe aiseee aiseee
 
Kuhusu kaburi kuwa duara nadhani dhana ni ile ile. Duara haina mwanzo wala mwisho. Ni mwendelezo usio na kikomo wala kona kona - kiashiria kwamba uganga huo utaendelea bila kipingamizi.

Kinyesi cha ng'ombe sijui ila nadhani ni ishara tu ya utajiri na fahari aliyokuwa nayo marehemu - na kwa wale watakaokuja kurithi mikoba yake. Ndiyo maana mbali na kinyesi tu wengine hupulizia (gūhuha) maziwa mabichi ya ng'ombe (mabele masūnga) kaburini ili marehemu aende vizuri na kwa furaha. Kumbuka kuwa kwa Wasukuma, kama ilivyo kwa makabila mengine mengi ya Kiafrika, maisha hayana kikomo. Ukifa unakuwa mzimu na bado utaendelea kuhusiana na walio hai kwa kuendelea kuwabariki, na hata kuwatesa. Vitu kama pombe za kienyeji, maziwa, mavi ya ng'ombe, nyama n.k. hutumiwa sana katika matambiko ili kuifurahisha mizimu ili ifurahi na kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wanajamii (mf. Ukame, ugumba, magonjwa, umasikini, mikosi n.k)

Kuna tasnifu ya umahiri katika Theolojia ya Kiafrika (Masters in African Theology) inagusia mambo haya. Nikilikumbuka jina la mtafiti na title yake kamili nitakuja kuiweka hapa. Iliandikwa na mtafiti kutoka Ujerumani kama sikosei.
Wabeja sana,barikiwa sana kwa huu muongozo
 
Naombeni kujuzwa ni kwanini waganga wa kienyeji wanazikwa wakiwa wamekaa kwenye kiti pia makaburi yao ni mviringo kama kisima, mwenye uelewa ni kwanini anijuze.

Na je ikitokea amezikwa kawaida nini kitatokea?

Lakini pia kwanini wanatupa kaburini kinyesi cha ngombe kabla ya kumfukia
Nilivyosikia story za vijijini machifu ndio wanazikwq hivyo
 
Back
Top Bottom