Ni jinsi gani naweza kupata matunzo ya mtoto aliyetelekezwa kutoka serikalini au ustawi wa jamii?

Mar 25, 2021
94
226
Habari zenu wanajamvi,

Naomba msaada kwa anayejua taratibu za kudai matunzo na huduma za mtoto kwa mwanaume aliyetelekeza mtoto, ambaye ni mwajiriwa wa serikali.

1. Je, stahiki hizi zinaweza kupatikatikana kwa kupitia mwajiri wake? Mfano kumuandikia mwajiri kwaajili ya madai ya matunzo ya mtoto?

2. Je, taratibu za kupata msaada kama huu ustawi wa jamii zikoje?

Mwenye ushauri wowote juu ya jambo hili nakaribisha tumsaidie rafiki yangu huyu aliyeachiwa mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka minne, na anaanza shule bila msaada wowote kutoka kwa baba yake ambaye ni mfanyakazi wa Wizara moja nyeti hapa nchini.
 
Habari zenu wanajamvi,
Naomba msaada kwa anayejua taratibu za kudai matunzo na huduma za mtoto kwa mwanaume aliyetelekeza mtoto, ambaye ni mwajiriwa wa serikali, Je stahiki hizi zinaweza kupatikatikana kwa kupitia mwajiri wake? Mfano kumuandikia mwajiri kwaajili ya madai ya matunzo ya mtoto?

2. Je taratibu za kupata msaada kama huu ustawi wa jamii zikoje?

Wanawake mnahangaika Sana yaani mtoto mmoja unashindwa kumtunza na kumsomesha ,

Kwanini uzae wakati huna pesa?

Pesa ya kulazimisha ni hatari mtu alikataa kukupa unakaa kimya
 
Nenda Mahakama ya Wilaya iliyopo karibu nawe, Kuna Mahakama maalumu kwa ajiri ya watoto(Juvenile Court).

Fungua maombi ya matunzo ya mtoto, Kama kweli ni baba yake mzazi. Itatolewa amri ya matunzo na fedha ya matunzo italipwa kila mwezi bila mbambamba
 
Wanawake mnahangaika Sana yaani mtoto mmoja unashindwa kumt
Mkuu wewe una watoto wangapi?? Emu acha kureply bila kujali hisia za mwenzako.

Iko ivi dada yangu! Nadhani kwa muajiliwa wa serikali inawezekana kabisa kama utafuata taratibu, uwezekano upo ukifatilia katika ofisi za utumishi.

Kama ni mwajiliwa sekta binafsi basi atapewa options katika maafsia ustawi wa jamii kutoa kiasi ambacho ni affordable kwake, usishangae kwa wiki akawa anatoa buku tano tu, kwasbab ndio kipato chake .

Ushauri wangu! Sasa..
Wewe ni mwanamke shujaa sana thus why umepata mtoto na unadai haki zake.

Ila suala la kutakana msaada kutoka kwa mwanaume ni kujenga dhana kubwa sana ya utegemezi..

Emu sikia pambana usiku na mchana kujenga future ya mwanao, ili huyo bwege aje kukuona ni wa thamani sana hapo baaadae

Jikubali pambana usikubali msaaada wa makubaliano katika kumlea mtoto wako.
 
Nenda Mahakama ya Wilaya iliyopo karibu nawe, Kuna Mahakama maalumu kwa ajiri ya watoto(Juvenile Court).
Fungua maombi ya matunzo ya mtoto, Kama kweli ni baba yake mzazi. Itatolewa amri ya matunzo na fedha ya matunzo italipwa kila mwezi bila mbambamba
Juvenile court sio ya watoto wenye mashitaka, yaani waliofanya uhalifu, au ninaelewa sivyo?

Aanzie ustawi wa jamii, watamuelekeza nini cha kufanya.
 
Habari zenu wanajamvi,
Naomba msaada kwa anayejua taratibu za kudai matunzo na huduma za mtoto kwa mwanaume aliyetelekeza mtoto, ambaye ni mwajiriwa wa serikali, Je stahiki hizi zinaweza kupatikatikana kwa kupitia mwajiri wake? Mfano kumuandikia mwajiri kwaajili ya madai ya matunzo ya mtoto?

2. Je taratibu za kupata msaada kama huu ustawi wa jamii zikoje?

Mwenye ushauri wowote juu ya jambo hili nakaribisha tumsaidie rafiki yangu huyu aliyeachiwa mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka minne, na anaanza shule bila msaada wowote kutoka kwa baba yake ambaye ni mfanyakazi wa Wizara moja nyeti hapa nchini.
Ni either ulizaa na mume wa mtu au ulikuwa kicheche wakati unadate na jamaa. Sio rahis mwanaume kukataa mtoto kama hakuna chochote kinachokupa mashaka
 
Ohoooo nchi hii kumbe hatuna maintenance court!!,safari yetu kama nchi tumepotea, ulizia kama tuna hii court, wenzetu hizi court unapata remedy within 5 working days na wanapiga garnish kwa kipato cha mzazi mwenzako na kila mwezi unafuata matumizi ya mtoto kwa court, hope waziri wa sheria atapeleka mswada bungeni wa kuundwa kwa mahakama hizi kama hatunazo
 
Habari zenu wanajamvi,
Naomba msaada kwa anayejua taratibu za kudai matunzo na huduma za mtoto kwa mwanaume aliyetelekeza mtoto, ambaye ni mwajiriwa wa serikali, Je stahiki hizi zinaweza kupatikatikana kwa kupitia mwajiri wake? Mfano kumuandikia mwajiri kwaajili ya madai ya matunzo ya mtoto?

2. Je taratibu za kupata msaada kama huu ustawi wa jamii zikoje?

Mwenye ushauri wowote juu ya jambo hili nakaribisha tumsaidie rafiki yangu huyu aliyeachiwa mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka minne, na anaanza shule bila msaada wowote kutoka kwa baba yake ambaye ni mfanyakazi wa Wizara moja nyeti hapa nchini.
Nenda hapo pugu road, jirani na kamata, uliza Depot la jiji, ingia ndani hapa, uliza askari atakuelekeza unyooshe moja kwa moja kwa mbele huko sasa utapata msaada kwa %100. (niliwahi pelekwa hapo) sipasahau hata kidogo...
 
Back
Top Bottom