NEC, kwanini hamkumchukulia hatua Babu Tale kujitangaza mshindi kabla ya mapingamizi hayajatolewa uamuzi na Tume?

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
3,599
8,553
NEC nihalali mgombea kujitangaza kapita bila kupingwa kabla hajathibitishwa na tume?

Tumeona Clouds FM & tv wakiadhibiwa kwa kutangaza matokeo kabla yakuthibitishwa na tume.

Je, ni halali kwa mgombea kujitangaza kashinda kabla hajathibitishwa na tume? Na hata uamuzi wa mapingamizi haujatolewa? Hii sio uchochezi kwa wapiga kura nakuleta taharuki katika jamii?

Nilitegemea pia police wamkamate nakumfungulia kesi ya uchochezi. Vipi leo Zitto &Mbowe wajitangaze wamepita kabla ya matokeo ya tume, hawatoadhibiwa na tume na kufunguliwa kesi ya za uchochezi?

Nategemea kama tume inatenda haki kumchukulia hatua kali Babu Tale hata kumuengua katika kinyang'anyiro ili kulinda sheria na taratibu za tume.

Note:

Maalim Seif alifutiwa matokeo 2015 baada yakujitangaza mshindi kabla ya tume haijatangaza matokeo.

2499794_Screenshot_20200828-101804.jpg
 
Wabongo wanaoamini ushirikina, wanaweza kuunganisha kifo cha mke wake(kilichotokea miezi kama miwili tu kabla ya kuchukua fomu za ubunge kule CCM) na utoaji wa kafara ili akubalike na iwe ndiyo tiketi ya mjengoni.

First appointment, direct bungeni bila hata kuwa na ushindani.

Mawazo mfu ya kishirikina, usiyachukulie siriyazi kiviiiiile.

Au mkuu Mshana Jr unasemaje kwa maoni haya yaliyojaa ushirikina.
 
NEC ndo walitangaza hivyo, Tale hakuweza kujivunga, ni wa kwetu tutamlinda.
 
Ukiwa CCM hata ukinya hadharani watasema umepiga chafya tu. NEC ni janga lingine kwa Taifa letu.
 
Mkuu tume siwanasema wanatenda haki?. Tunawakumbusha ili baadae yakija kutokea sisi tuwe tulitimiza wajibu wetu.
Kwa muda huu wangekuwa wame nullify uhuni wote uliofanyika kwenye hayo majimbo... yaani karne hii mtu atapitaje bila kupigwa kama si uhuni na hujuma za waziwazi.

wengi wao wameporwa forms..... kwanza hizi form baada ya kujazwa zilitakiwa kuwa scanned kisha kuwa uploaded kwenye website ya Tume. huu uhuni uhuni wa kunyanganyana form majimbani ama njiani ungekuwa haupo kabisa.
 
Unachosema nikweli ilitakiwa zoezi lifanyike kwa uchaguzi wa mtu either online au mtu apeleke form ,mgombea mwenyewe ndio aamue njia ipi afate, tatizo tume bado inaishi zama za mawe au wanaona hii njia wanayotumia ndio itainufaisha ccm.

Nawangeweka utaratibu wa ujazaji form online Kama mtu amekosea system inagoma kupokea ,namuonyesha wapi panahitajika marekwbisho.
 
ni kweli yaani mtu kumwambia umekosa haki yako ya kuchaguliwa Ubunge ama Udiwani kwa sababu eti umeporwa form wakati wa kurejesha ama umekuta Msimamizi wa kituo akakuzingua zingua au kafunga office hadi muda unakwisha.

Kama hivyo ndivyo basi bado tunaishi karne ya kale mno. kibaya zaidi akishaporwa hiyo form original huna namna tena pa kuipata kwingine.
 
Wabongo wanaoamini ushirikina, wanaweza kuunganisha kifo cha mke wake(kilichotokea miezi kama miwili tu kabla ya kuchukua fomu za ubunge kule CCM) na utoaji wa kafara ili akubalike na iwe ndiyo tiketi ya mjengoni.

First appointment, direct bungeni bila hata kuwa na ushindani.

Mawazo mfu ya kishirikina, usiyachukulie siriyazi kiviiiiile.

Au mkuu Mshana Jr unasemaje kwa maoni haya yaliyojaa ushirikina.
Haya umeyazua mwenyewe
 
Back
Top Bottom