Ndege mpya yafanyiwa majaribio. Yaenda Kigoma bila abiria na kugeuza bila abiria

Abiria watakaopanda hizo ndege ni lazima watahadhalishwe jiu ya hatari ya haya mapanga; msaidizi wa Rais Mwinyi aliyejulikana kwa jina la HABIB HALAHALA alipoteza maisha kwa kukatwa katwa na mapanga ya helicopter!!!

Ile ilikuwa helicopter na propeller zake ziko chini sana kwa kuwa helicopter nayo iko chini, haina matairi wala ngazi. Propeller za ndege kwa maana ya airplane hata ile yenye injini moja ziko juu sana na huwezi kupanda bila ngazi. Nenda uwanja wa ndege wowote ujionee kwani inaonekana uko kijijini.
 


Ndege mpya aina ya Bombardier Dash 8~Q400 iliyonunuliwa hivi karibuni imeenda leo Kigoma kwenda imeenda bila abiria na kurudi imerudi bila abiria.

Je huku ni kubana matumizi? na imetumia masaa mawili kutoka Dar to Kigoma awali ndege hii ilitegemea itapata abiria imekoswa abiria kutokana na sababu zisizojulikana raia wamesusia??

=======

NDEGE mpya ya Bombardier Dash 8- Q400, iliyonunuliwa hivi karibuni imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma ikiwa ni ukaguzi na majaribio ya mwisho kabla haijaanza kubeba abiria. Ndege hiyo ni kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali na kukodishwa ATCL.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua uwanjani hapo jana Mhandisi wa Ndege wa ATCL, John Chaggu amesema baada ya safari hiyo ndege hiyo itakuwa tayari kubeba abiria.

Amesema, katika majaribio hayo alikuwa na wakaguzi wawili wa ndege kutoka Canada wa kampuni iliyotengeneza ndege hiyo.

Chaggu amesema, safari yao kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma iliwachukua saa mbili angani.

Ilitua Kigoma saa 11:00 jioni na kuondoka saa 12:18 jioni .

Ndege hiyo ilitarajiwa kuendelea na safari ya ukaguzi kwa kwenda kutua Uwanja wa Ndege wa Mwanza na baadaye kurudi Dar es Salaam.

Chanzo: Swahili Times

mbona maelezo zako yapo tofauti na hiyo video au sijakuelewa vizuri?
 
Back
Top Bottom