Nawezaje kujitetea mahakamani kwa makosa haya ambayo nimewekewa

xprogram

New Member
Mar 29, 2024
2
1
Nimeshitakiwa kwa makosa ya kuwazuia TRA. Kufanya kazi yao na pia kuhari mali ya serikali ambayo ni gari, inayodaiwa kupigwa kwa mawe japo haijapasuka hata kio ila pia wakati tukio limetendeka sikuwepo eneo la tukio. Nimekutana na opereshen ya kamata kamata iliyokuwa ikiendelea nami nikaingizwa humo. Msaada wakuu namna ya kujitetea mahakamani
 
Nimeshitakiwa kwa makosa ya kuwazuia TRA. Kufanya kazi yao na pia kuhari mali ya serikali ambayo ni gari, inayodaiwa kupigwa kwa mawe japo haijapasuka hata kio ila pia wakati tukio limetendeka sikuwepo eneo la tukio. Nimekutana na opereshen ya kamata kamata iliyokuwa ikiendelea nami nikaingizwa humo. Msaada wakuu namna ya kujitetea mahakamani
Aise pole sana mdau, kwa situation yako kama unauhakika hukuwepo katika eneo la tukio, basi huo ndio utetezi wako kisheria inaitwa (defense of alibi). Lakini namna ya kutumia utetezi huu inategemea na mahakama kesi yako inaposikilizwa. Ikiwa ni mahakma ya mwanzo utajitetea hivyo tu mda wako wa utetezi ukifika.

Lakini ikiwa kesi yako ipo katika mahakama ya wilaya/ hakimu mkazi ama mahakama kuu, basi utatakiwa kutoa taarifa ya nia ya kutumia utetezi huo kwa mahakamani na kwa upande wa mashtaka kabla kesi aijaanza kusikilizwa. (Imeelekezwa na kifungu cha 194(4) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai yaani CPA).

Na iwapo haukutoa taarifa ya nia hiyo na kesi tayari imeannza kusikilizwa basi utatakiwa kuupatia upande wa mashtaka maelezo ya utetezi huo kabla ya kesi ya upande wa mashtaka kufungwa (imeelezwa katika kifungu cha 194(5) cha CPA).

N.B: Ukishindwa kufanya hivyo basi mahakama itakuruhusu kujitetea lakini haita upa uzito utetezi wako, kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 194(6) cha CPA. Hivyo ni muhimu kufata utaratibu huo.

Kwa faida ya wasiofahamu; Kosa la kumzuia afisa wa TRA kufanya kazi yake ni kinyume na kifungu cha 34(C) cha Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, na adhabu yake ni faini isiyozidi laki 5 pamoja na kifungo kisichozidi miaka miwili. Tukija kitika kosa la kuharibu mali yeyote, kosa hili ni kinyume na kifungu cha 326 (1) cha sheria ya Kanuni za Adhabu na adhabu yake ni kigungo cha miaka 7.

hapa chini👇 nitashare sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kwa maelezo zaidi.
 

Attachments

  • SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf
    688.5 KB · Views: 6
Back
Top Bottom