Wanaume kiasili ni wasiri na wasiopenda kuwa na urafiki au vikundi kama ilivyo wanawake. Pia wanaume wengi huweka vitu moyoni na sio rahisi kufunguka yanayowasibu, wengi hawaonyeshi hisia aidha za furaha au huzuni yaani ni stoic.
Lakini kwa upande mwingine mwanadamu ni kiumbe social anahitaji ile socialisation ili kuishi vizuri na kuweza kustawi hasa kisaikolojia na afya ya akili. Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na marafiki wenye common interest wa kujengana na kuweza kupeana motisha na ushauri mbalimbali katika maisha ya kila siku.
Kukosa hili husababisha upweke ambao athari zake hazina tofauti na uvutaji sigara. Hili linatokea hasa kwa wanaume kuanzia miaka 30 ambapo kila mmoja anakuwa bize na majukumu yake ya maisha.
Baadhi wanatumia vikundi vya unywaji, wengine vikundi vya michezo kama mpira, jogging, michezo ya magari katika namna ya kupata hiyo brotherhood ambayo husaidia utimamu wa mwanaume. Wengine hujiunga katika vikundi vya kifamilia n.k.
Lakini wengine duniani huko wapo kwenye vikundi vya siri (secret society) ambavyo vimekuwa vikubwa na powerful kiasi cha kuogopwa duniani.
Vile vile kuwa na umoja hurahisisha mambo mengi kwasababu ya mawazo tofauti na pia "network" ya watu mbalimbali. Wahindi wanatumia huu mfumo sana kwenye jamii yao na hata biashara ambapo asimilia kubwa ya biashara za wahindi wanatumia mfano benki ya exim ambayo ni ya wenzao vivyo hivyo kwa huduma nyinginezo.
Sasa je nawezaje kuanzisha Brotherhood, ya watu makini kwa ajili ya kupata ule ukomredi ( camaraderie) na kupeana changamoto na support katika maisha ya kila siku hapa nchini??
Je vikundi hivyo vipo tayari nchini?