Nataka nimfungulie kesi aliyejitambulisha kama Customer care wa Halotel kwa kunitukana bila sababu

beatboi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
457
1,125
Habari zenu watoto wa mama (SSH)

Nimejikuta wiki nzima imeharibika baada ya kupokea matusi kutoka kwa mtu ambaye amejitambulisha ni mtoa huduma kwa wateja (customer care).

Nilikuwa nimepumzika zangu majira ya asubuhi ghafla nikapokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa anatoka kitengo cha halopesa hivyo akaomba nimtajie kiasi cha pesa kilichomo kwenye account yangu sababu kuna mtu amekosea bahati mbaya ikaingia kwangu.

Nilimtajia kiasi kilichopo tena akasisitiza hadi visenti vyote kisha akakata simu. baada ya hapo ikaingia sms ya kupokea huo muamala, nilivyomaliza kusoma tu jamaa akanipigia akawa ananipa maelekezo jinsi ya kurudisha hiyo pesa ya watu.

cc: unatumia simu gani?

Mimi: Samsung j2

cc: OK rudi hadi sehemu ya kupiga hapo mwanzo

Mimi: tayari.

Kuna namba akawa ananitajia niandike ila kutokana na maeneo niliopo mtandao ukawa unasumbua, sasa nikamwambia hpa nilipo mtandao unasumbua kidogo! dah nikawa nimefungua mvua ya matusi coz yule jamaa alimtukana mama yangu, mimi mwenyew na ukoo mzima na kunikatia simu kwa ghadhabu. nimefikilia nikaona kabla sijafungua kesi niwashirikishe ndugu zangu wanajfm kwa ushauri maoni nk.

Nimeambatanisha na ushahidi wa picha namba zake

Screenshot_20220601-122837_Messages.jpg
Screenshot_20220601-122936_Phone.jpg
 
Matapeli ungejiroga tu kuandika zile namba ndo ingekuw ntolee halaf huyo siyo customer care.
customer care wana namba maalum na zinajulikana
 
VODACOM wameanza wizi wa hela za MPESA wameninyofolea buku 5 bila aibu naombeni jinsi ya kuwapata
Hahah Voda Majuzi walifanya Operation ya watu wote waliokopa afu hawakulipa hata Kama ulikopa 2016 huko.Na walichomoa hela bila kutoa taarifa kwa waungwana,case zimekua nyingi kwny ofisi za Voda.Ukienda utaonyeshwa Deni ulilokopa.
 
Usikubali kutapeliwa mkuu, message za makampuni zinakuja na jina la kampuni na siyo namba. Huyo nitapeli.
Mfano message kutoka NBC bank itaandika ni NBC, vilevile kwa makampuni yote.
 
Habari zenu watoto wa mama (SSH)

Nimejikuta wiki nzima imeharibika baada ya kupokea matusi kutoka kwa mtu ambaye amejitambulisha ni mtoa huduma kwa wateja(customer care)...
Huyo ni tapeli tu.Halafu utamfunguliaje kesi mtu usiyemjua? Hiyo namba ilikuwa kwa ajiri ya kupiga halafu inazimwa au inatupwa.
 
Hahah Voda Majuzi walifanya Operation ya watu wote waliokopa afu hawakulipa hata Kama ulikopa 2016 huko.Na walichomoa hela bila kutoa taarifa kwa waungwana,case zimekua nyingi kwny ofisi za Voda.Ukienda utaonyeshwa Deni ulilokopa.
Sijawahi kukopa na wala sina deni nao kabisa zaidi ya songesha ambayo huwa nalipa kwa wakati. Mpaka kufikia juzi sikuwa na deni lolote.
 
Sijawahi kukopa na wala sina deni nao kabisa zaidi ya songesha ambayo huwa nalipa kwa wakati. Mpaka kufikia juzi sikuwa na deni lolote.
Basi wafuate ofisini kwao chief.Lkn pale Kuna case za watu waliokopa mpk huko 2015.
 
Back
Top Bottom