Natafuta kazi/ kibarua

Babu wa Watu

Member
Oct 31, 2021
40
101
Kama kichwa Cha habari tajwa....

Sifa nlizonazo

a)Dereve wa Gari zote( kubwa na Ndogo) kama mabosi wa
Magari mpo humu nawakaribisha

b)kama wewe ni Dereve unahitaji conductor pia nipo tayari

C)kama wewe ni Dereva wa gari kubwa unahitaji tingo pia hizi kazi nazimudu vizuri tu

d)Mafundi Magari pia nipo hapa fundi waire japo sio expert sana ila niliwahi pitia huko kwaiyo kama unahitaji kijana wa kukusaidia pia nipo hapa hata watu wa Machanics pia...

e) Pia nipeni location za site zenye vibarua /Saidia fundi pia nipo tayari

f)Pia nahitaji kazi yoyote pia nje na hizo Ili kujipatia kipato i.e zisiwe nzito sana maana mimi Sina tank (Nipo Slim kiumbile)

NB: Daladala ,Uber, Bolt nanyi mnakaribishwa
Mawasiliano yangu ni
0763648843/0710194863

Location Dar es salaam ila popote mi natia timu

Naomba kuwasilisha...
 
Tafuta vijana 2 -3, nunua kikaangio Cha vitumbua chenye tundu 50.

Hao vijana wawe Wana ujuzi angalau wa kuchoma vitumbua, Sasa hivi kitumbua ni 200-300.

Kanunue chenga mashineni kwa Bei ya jumla, Kisha osha na usage unga.
Nunua mafuta lita 5 angalau.

Deli zile kubwa au kati 2, Kisha tafuta kijiwe asubui na mapema anzeni kuchoma mzigo.

Na uhakika mambo yata jipa tu.
 
Hili ngoja nilifanyie kazi mwenyewe sidhani kama dogo atahitajika

Ntakupigia hesabu nione faida yake Ikoje
Una karibishwa Sana, kikubwa kama uko dar ndo bwelele Sana.

Nenda masokoni kule ndani, ongea na wachinja kuku, huwa Wana yakusanya lumbesa.

Sasa wewe ongea kiume ukaze, iki bidi onyesha sura ya huruma😁, kuwa aku achie kwa Bei nafuu.
Hapa uta jikuta life goes on
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom