Nashughulikia mambo mbalimbali Dodoma bila wewe kulazimika kufika hapa

Kama una ujanja na manunuzi pia ungetaja maana kuna vitu vizuri vinauzwa lakini tunapoteza imani kuwatumia pesa bila hata bidhaa kukaguliwa.

Fikiria kufungua ofisi kwaajili ya hilo
Nashukuru sana kwa ushauri,nitalifanyia kazi ndugu yangu.Ofisi ntaifungua siku zijazo kadri huduma inavyokua,siyo siku nyingi.Asante
 
Mimi ni mkazi wa Dodoma, nimekuwa nikiagizwa sana na baadhi ya wafanyakazi hasahasa wa Serikali pia na wa sekta binafsi kwa uchache, kuwatatulia matatizo mbalimbali ambayo hayawalazimu wao kufika huku (Dodoma).

Kwa kufanya hivyo, huwa wanaokoa gharama za usafiri na malazi na badala yake, huchangia kiasi cha fedha, nikishamaliza kuwashughulikia hayo matatizo na kuridhika na huduma niliyoombwa kuifanya.

Mfano wa huduma ambazo mara kadhaa huambiwa niwashughulikie ni kama kwenda kwenye Wizara mbalimbali kama Wizara ya Mambo ya Ndani, kupeleka barua ya kuomba uanzishwaji wa viwanda vya vilipuzi, pia kwenda bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuomba statements za mikopo yao, kwa wale wanaokuwa na lengo la kumaliza madeni yao(loan liquidation), kufuatilia barua za wale walioachishwa kazi na wameomba kurudishwa kazini n.k

Endapo wewe ni mmoja wa wale wanaohitaji huduma zenye kushabihiana na nilizotolea mfano hapo juu na hata kuuliza tu, karibu PM au hapahapa, kama utakuwa na la kuuliza.

Asanteni.
Mawasiliano:0765920855
nice one. All the best
 
Back
Top Bottom