Nashauri: Kuongea Kiingereza kwa unyoofu (fluency) ibaki kuwa kigezo cha kumpima Mtanzania mwenye Degree

Siku zote naamini ili mtu aweze kuendelea katika nyanja zote ni lazima atumie lugha yake. Ukitumia lugha ya mwenzako utabaki hapohapo na inakuwa rahisi kuwa na utumwa wa kifikra.

Kiswahili inapaswa itumike katika nyanja zote kuanzia vidudu hadi elimu ya juu. Tumefanya makosa sana kuruhusu lugha ngeni itumike hadi leo kwenye shughuli muhimu.

Tukitumia kiswahili kwa asilimia 100 tutaweza kujijenga wenyewe kwa mapana pasipo kuyumbishwa na tamaduni za wengine ambazo zinatufanya tuwe wanyonge pasipo kuwa na sababu.

Lugha inabeba utamaduni wako kwa kiasi kikubwa na ndani yake kunakuwa na uzalendo na kuthamini cha kwako. Tumefanya makosa kuruhusu lugha ya kikoloni hatima yake imekuwa kama hivi mtu anathamini cha wengine kuliko cha kwake.

Tusipobadilika kwa kujijenga wenyewe kulingana na utamaduni wetu tutabaki kuwa hivi tulivyo(masikini wa fikra na kiuchumi) milele.
 
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Kama unaongelea waliosomea degree ya lugha ya kiengereza sawa. Lkn kuna watu wanachukua degree hazihusiani kabisa na iyo lugha. Kwa mfano kama ukichukua degree ya lugha ya kiarabu itakuwaje
 
Mk
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Mkuu umewahi kuwa au kufanya kazi na wazungu ambao kwao sio uingereza,au marekani?
Nilichojifunza mimi ni kwamba,tunaohangaika na gramma kama kigezo cha usomi ni sisi watu weusi.
Mzungu anajali usome kilichoandikwa na uwe na uwezo wa kuelewa na kukifanyia kazi basi.
Ningekuelewa zaidi kama ungesema,kuelewa kilichoandikwa kwa kiingereza itumike kama kigezo ningeelewa.
 
Kiingereza hapa Tanzania Kama hujasoma gari la njano unabidi utenge 15 yrs hadi kuwa fluent
 
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Muongeaji mzuri wa lugha huwa hachanganyi changanyi lugha mbalimbali katika setting moja. Utaona mtu anahojiwa kwa kiswahili, halafu anajilazimisha kuweka maneno ya kiingereza " ... to me, mimi naona it is better ku-translate tafsri hii kutoka kiswahili kuwa english directly moja kwa moja."
 
Bahati mbaya sina elimu juu sana, ila nimekua nikisikia, watu wanasema, huyu ana digree ya uchumi ama ya sheria.

Hivyo mleta mada unataka, aliesomea digree ya sheria, hata kama amepass vizuri kwenye fani, ila kama kiingereza chake haongei kama mwingreza, huyo ameferi.

Ila anaengea vizuri, kiingereza ila kwenye fani hakufanya vizuri huyo ndiye apasishwe eti.

Maana unaamini usomi ni Kujua kuongea kwa usahihi kiingereza
 
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Kiswahili chenyewe bado hatujakaa sawa
 
umesahau hili mkuu yaani degree watu wasiwe wanasoma fani yoyote, hizi sijui sociology watu wasome wakiwa form five na six, mtu akifika chuo ni kusoma english course tu miaka mitatu tutafanikiwa sana, maendeleo hayana chama.
 
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Tuanze na wewe mwenyewe una kiwango Gani cha elimu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom